Lembeli: CCM ni chama kizuri ila baadhi ya watu wake wana roho mbaya sana

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,571
Mwanachama wa CCM mzee Lembeli anasema CCM ni chama kizuri ila baadhi ya viongozi na wanachama wake ni waongo, wanafiki tena wana roho mbaya sana.

Lembeli anasema aliondoka CCM na kuhamia Chadema baada ya kushindwa kuvumilia matusi aliyotukanwa na wabunge wa CCM baada ya kuwasilisha ripoti ya operesheni Tokomeza.

Amemalizia kwa kusema aliamua kurejea CCM baada ya kuona Mwenyekiti wa sasa anakibadilisha chama na kusimamia ukweli. Alifanya hivyo pia baada ya kuombwa na wakazi wa Kahama, mama yake pamoja na Rais Magufuli mwenyewe.

Source Clouds 360

Maendeleo hayana vyama!
 
Vp ametoa dawa ya wale wenye roho mbaya?? Nafkliri Mzee Lembeli alipoamua kurejea ccm alitegemea kitu fulani (cheo). Sasa muda unayoyoma na Jamaa kampotezea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu nae anang'ata na kupuliza hapo juu kashasema baadhi ya 'viongozi' na wanachama na maneno yake huku chini anasema kiongozi wao ni mzuri sasa hapo tumweleweje.
 
Anamaanisha Report ya CAG 2017/2018 ndio Operation Tokomeza ya awamu ya tano
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom