Lema: Watanzania wengi wanaandamana lakini hawaonekani sababu wanaandamana mioyoni, ipo siku

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,742
40,873
Wadau,

Leo mbunge Lema ameongea kwa uchungu mkubwa sana bungeni akimlilia Ben Saanane na Mawazo..

Sina hiyo video kama kuna mwenye hiyo video aiweke hapa watu waisikilize..nimeisikiliza kwa Millardy.
Ninaungana na Lema kuomba vyombo vya usalama ndani ya kaya yetu vituambie Ben Saanane yupo wapi.

Tanzania ni nchi ya amani na utulivu hatujafika mahali mtu apotee tu bila kujulikana yupo wapi.inauma sana ila uvumilivu ni jambo la msingi tushirikiae wote, viongozi wa chama chake, viongozi wa kaya yetu na vyombo vya usalama tujue huyu mtu yupo wapi...

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema amesema Watanzania wengi wanaandamana lakini hawaonekani sababu wanaandamana mioyoni, ipo siku watatoka kuandamana barabarani-

Hayo hayatuhusu sisi,huyo Ben alitumwa na nani kumsemasema mkuu? Mtu huna hata mazoezi ya viungo namna ya kujidefence unaanzisha beef na wakubwa what do u expect? Na huyo Roma aache kuimba mambo ya kuikosoa serikali kila siku,watu wanataka burudani siku hizi na sio elimu,,kama elimu tulishapewa na akina SUGU,PROF JAY,KIKOSI enzi hizo
 
Amesema au amesema.iliyokweli??Tatizo vyeti hakuna tunaogopa mpaka vivuli vyetu.
 
Uncle Freeman alishasema hakuna haja ya kupaniki sababu vyombo vya dola vipo kazini na yeye binafsi ana imani navyo...wiki mbili baadae Kubenea naye akatufungua macho zaidi...au Lema hakusikia?

Ndiyo maana hakumjibu yule mpuuzi wa CCM aliongea kama hizi sentensi zako.
 
Uncle Freeman alishasema hakuna haja ya kupaniki sababu vyombo vya dola vipo kazini na yeye binafsi ana imani navyo...wiki mbili baadae Kubenea naye akatufungua macho zaidi...au Lema hakusikia?
Itakua wakati kubenea anaandika habari za saanane lema alikua jera kisongo
 
m
Wadau:
Leo mbunge Lema ameongea kwa uchungu mkubwa sana bungeni akimlilia Ben Saanane na Mawazo..sina hiyo video kama kuna mwenye hiyo video aiweke hapa watu waisikilize..nimeisikiliza kwa Millardy.
Ninaungana na Lema kuomba vyombo vya usalama ndani ya kaya yetu vituambie Ben Saanane yupo wapi.
Tanzania ni nchi ya amani na utulivu hatujafika mahali mtu apotee tu bila kujulikana yupo wapi.inauma sana ila uvumilivu ni jambo la msingi tushirikiae wote,viongozi wa chama chake, viongozi wa kaya yetu na vyombo vya usalama tujue huyu mtu yupo wapi...
msituletee uhuni. familia yake bila shaka wanajua yuko wapi mbona wamekaa kimya. labda mumempeleka kujifunza ugaidi halafu mnauliza serikali imtoe wapi.
 
Back
Top Bottom