Lema waombe radhi Diaspora na DW-Swahili

Ni kweli taarifa ya Lisu, ya mambo aliyoongea na Mje. Rais Samia inaonekana ni maagizo ili Rais atekeleze. Hili ndiyo tatizo la Lisu la kujikweza na kuonyesha kuwa yuko juu ya kila mtu.

Mdogo akiongea na mkubwa, ni mkubwa ndiyo anatoa taarifa ya kilichoongelewa; kinyume chake ni kuukosa adabu.

Huku ndiko kukoroga mambo kulivyo.
Kuna watu wanamsifia sana Lissu, namimi pia naamini kuna smartness anayo Lissu lakini kitu busara hana kabisa. Yaani uongee na Rais halafu wewe ndio utoea taarifa ya mmezungumza nini?

Mi nilijua tu, kawaida ya viongozi huwa sio kutekeleza matakwa ya wanasiasia kwa amri bali kwa maridhiano. Yaani umpe Rais maagizo halafu unakuja unasema bila masharti,jamaa kakwama sana.
 
Haki ha
Haki haiombwi hata kenge habembelezi kuiomba anayoamini ni haki yake, hapo hana akili vipi kwa wanaouza mbongo zao pale mtaani kwao? SI watazidiwa na kenge Kwa uelewa na kunitambua?
Kwanini asichukue kama haki haiombwi? Kama kitu ni chako si uchukue??
 
Diaspora wanahitaji kuhamasishwa mambo ya msingi
Uwekezaji na kusaidia maboresho katika elimu, afya, huduma za kijamii n.k
Siyo wao kuhimiza siasa nyuma ya keyboard front waende wengine

Watanzania walishajifunza, watakaopatwa mihemko hawali cake ya taifa, wao na familia zao watakuwa on aribu na polisi na mahakama na jela, siyo wao wenye kimbelembele ndiyo watakaopatiwa ubunge wala wake zao kuwa viti maalum.

Mange alishajifunza! Diaspora wanatokea paka, panya na mbwa watano kuandamana!
 
Ni kweli taarifa ya Lisu, ya mambo aliyoongea na Mje. Rais Samia inaonekana ni maagizo ili Rais atekeleze. Hili ndiyo tatizo la Lisu la kujikweza na kuonyesha kuwa yuko juu ya kila mtu.

Mdogo akiongea na mkubwa, ni mkubwa ndiyo anatoa taarifa ya kilichoongelewa; kinyume chake ni kuukosa adabu.

Huku ndiko kukoroga mambo kulivyo.
Kweli kabisa mkuu,ilimpasa awe mvumilivu kabla ya kutafuta political mileage kwa wahisani wake.

Pia asingekubali ushauri wa kina Maria Sarungi kule the Space.na kuanza kutoboa yote.
 
Ni halali pia asiyeshiriki siasa asimlaumu mwanasiasa, utamu wa ngoma ingia uicheze, Lema yuko sahihi watanzania ni mazezeta sana hasa hao diaspora ni utopolo kabisa. Kama haiwahusu wasishaddie siasa waendelee na upupu wao huko waliko
Walifika huko kwa jitihada zao binafsi.

Wanao ndugu zao huku wanaopenda kusikia wakiishi kwa amani tele.

Diaspora ndio wanajuwa thamani ya kuishi nyumbani ukiwa na Amani,maana wamekutana na kila aina ya wakimbizi huko.

Lakini pia wanaweza kufanya siasa bila kuishabikia Chadema na wakashabikia chama kingine cha upinzani.

Msiwapangie cha kufanya.wameelimika vya kutosha na ndio maana wapo hapo walipo.
 
Habari Member's JamiiForums.

Habari Moderators JamiiForums.

Kama kawaida naomba niende kwenye Mada.

Nimemsikiliza God bless Lema akiongea kwenye moja ya mitandao kupitia YouTube.

Anawalaumu sana Diaspora wa Tanzania walioko Ulaya (EU).
Na walioko pia America .

Kwamba hawajitokezi kuunga mkono jitihada za kuipinga CCM na serikali ya Tanzania.

Kwa kuandamana,kwenda kwenye balozi za kimataifa.
Hasa pale inapotokea rais amefanya ziara huko mataifa ya nje.

Anawashangaa kwa kujisahau(maoni yake Lema).
Huku wao kina lema na wenzake wakihenya kuipinga CCM na serikali yake huko majuu.

Pia amewadhalilisha wale waliojitokeza kumlaki Mh Rais Samia Suluhu Hassan,kwa kuwatuhumu kwamba, wanafanya hivyo kwa kupewa $30 na $20 toka kwenye balozi zetu.(bila kutaja uthibitisho wowote).

Pia lema kupitia Clip hiyo amesikika akimlaumu soud Mnette wa @DW-Kiswahili.

kwamba amekula njama na serikali ili kuchelewesha kwa makusudi ile taarifa ya mahojiano kati yake soud Mnette na Mh Samia.

Tumekuwa tukiandika humu kuisema CHADEMA kwa kutotumia busara katika baadhi ya maamuzi ya viongozi wake wa juu.

Na huu ndio mojawapo ya mifano halisi.

lema alipaswa kuelewa kwamba Diaspora wa Tanzania walioko huko wamekwenda kwa juhudi zao binafsi na wanao utashi wa kuamua nini kinawafaa au hakiwafai.kutokana na mazingira ya huko walipo.

lema anapaswa kuelewa kwamba Diaspora wa Tanzania walioko huko wamekwenda kutafuta riziki za kuwasaidia wao na familia zao kwa ujumla.

lema hapaswi kuwalaumu Diaspora hao kwa sababu wao sio wanasiasa wala wanaharakati.na ikitokea wakapoteza ajira zao kwa kufanya siasa na kwenda kinyume na mikataba yao.

Sio lema wala CHADEMA wala mtu yeyote zaidi yao wenyewe watakaopata shida.
Tena wasiweze hata kupata msaada wowote toka kwa lema na taasisi yake.

@DW-SWAHILI nao wanao utaratibu wao wa kuratibu vipindi na hivyo sio lazima waendane na ratiba za CHADEMA na Lissu.

Lissu mwenyewe ndie alikosa busara ya kusubiri baada ya kuwasilisha maombi yake kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Kwamba...kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari kusema yoote waliyoongea faragha na Raisi Samia.bila subira.

Angevuta subira ili Mh Rais arejee nyumbani na walau apate muda wa kuyafanyia kazi maombi ya Lissu.

Badala ya kumaliza Media zote ndani ya masaa 48 tangu waongee.
Huku akiyageuza kama maelekezo au amri kwa Rais Samia.

Tunajua kwamba alikuwa anafanya hivyo kwa makusudi ili kujionyesha uzito alio nao kwa wafadhili wake huko @EU.
Na ili pengine wampe nguvu zaidi.

Lakini akasahau kwamba anajaribu kujijenga nje huku akijibomoa ndani nyumbani.

Ni vema lema ukatumia busara na kuwaomba radhi hao Diaspora wa Tanzania.

Pia ukatowe tena press release ukiwaomba na @DW-Swahili radhi.
Maana itafika mahali Chadema mtagombana na kila kundi.

Maana pia kwenye clip yako umesikika ukiwalaumu viongozi wa taasisi za kidini nchini.

Enezeni sera nzuri ili muwavutie wafuasi zaidi.badala ya kulazimisha kila mtu awe mwanaharakati.

Huko USA na European watu wako busy kupambania life zao zaidi.

Walitumia akili na nguvu zao wenyewe hivyo usiwapangie.
Sasa hii ni taarifa au ni malalamiko yako ka mema? Mama acha kujificha nyuma ya keyboard, sema hadharani wewe ni rais japo wa mchongo
 
Kuna watu wanamsifia sana Lissu, namimi pia naamini kuna smartness anayo Lissu lakini kitu busara hana kabisa. Yaani uongee na Rais halafu wewe ndio utoea taarifa ya mmezungumza nini?

Mi nilijua tu, kawaida ya viongozi huwa sio kutekeleza matakwa ya wanasiasia kwa amri bali kwa maridhiano. Yaani umpe Rais maagizo halafu unakuja unasema bila masharti,jamaa kakwama sana.
@platos
Tena bila hata subira ya kwamba ngoja walau amalizie ziara yake na kurejea nyumbani,halafu nimsikilizie.

Wanapaswa kuelewa kwamba hata Rais ni binadamu kama wengine.

Maombi yale yanahitaji aweze kukaa na washauri wake mbalimbali kabla ya kuyatolea maamuzi.
 




Hii tabia ya watanzania kufikiria vitu kenywe vichwa vyao na kudhani watu wote wanafikiria kama wao ni tatizo kubwa sana nilijua ni akili za dada zangu tu yaani wanaweza kukwambia vitu ambavyo havipo kabisa kwenye kichwa chako. Au wanatafsiri situation tofauti kabisa na uelewa wa mtu mwingine halafu anakulazimisha na wewe umetafsiri ivyo.

Lema anadhani DW au BBC ni sawa na TBC contrary to the fact mtangazaji anajifanyia tu propaganda za ovyo ovyo mjomba hao watu wapo regulated kulaumu baadhi ya wafanyakazi ni ignorance.

Hizo taasisi zinafuata utaratibu wa sheria na balancing story ni kipaumbele kwenye kazi, kama ni story za upande mmoja utasikia jitihada za kumpata muhusika wa upande wa pili zilishindikana na waweke huo ushahidi wakiulizwa, kuna producer wa kipindi ukija mziki yeye ndio anaucheza sio reporter so kulaumu watangazaji wa nje ni shallow.

Pili raisi wa nchi usimchukulie poa maza akisafiri kuna wapambe kibao wanatangulia ata chakula cha hoteli anayo fikia kuna mtu anasimamia kinavyotayarishwa mpaka kinamfikia kama apiki mpishi wake mwenyewe.

So ukisikia watu wanaenda kukutana na raisi moja kwa moja jua ubalozi umeandaa na wanaenda wapambe wao tu sio kila mtu atajua halipo unless ile mikutano ambayo alikuwa akifanya J.K ya kukutana na watanzania na msafara wake sikia tu kuna watu luluki wanatangulia na wanakuwepo kwenye hiyo mikutano yake utadhani mpo Tanzania ulinzi wenyewe vinginevyo kama msafara mdogo umuoni wala hujui alipofikia asipoamua.

Mfano Samia alipoenda Glasgow hakuna mtanzania alijua alipofikia na wala kukutana nae zaidi ya watu wake wa serikali waliotoka Tanzania mapema na watu wa ubalozini ndio waliopo kwenye ile clip ya kumpokea hoteli ni, lakini hakukuwa na diaspora ata mmoja pale.

Usidhani raisi akitoka nje ya nchi status yake na ulinzi unabadilika kwa kiasi kikubwa ngoja siku aende Canada ndio atajua Lissu alipewa heshima tu ya kukutana na Samia na ndio maana akawa mnyenyekevu ulinzi wake sio wa mchezo na kukutana nae ni mission kweli kweli.

Malalamiko yake ni vitu anavyofikiria tu kichwani kwake tofauti na uhalisia dunia inavyozunguka.
 
Huna hoja unalaumu tu mwanzo mwisho, hizo ni hulka za kike, wewe kama sio yule chifu basi ni wakala wake
Je Lema amelalamika au ametoa hoja au sera?

Je wewe binafsi umeisikiliza hata hiyo clip.

Chadema siku zote hamna hoja zaidi ya vihoja.

Mnapaswa kujenga sera zenye ushawishi kwa wananchi.

Badala yake kila kada anatafuta umaarufu binafsi na matokeo yake mnalikoroga wenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
@mdudu
Nimekula kabisa na hata sasa niko naandika nikiwa na kahawa mezani mkuu.
Kuna mvua kubwa huko nje.tuwe na utamaduni wa kuambiana ukweli wa hoja bila ugomvi wala matusi.
Sisiemu imeanza kuwa na vijana wastaarabu ..hii Ni ajabu kabisa au huwenda kiama kipo karibu..
 


Hii tabia ya watanzania kufikiria vitu kenywe vichwa vyao na kudhani watu wote wanafikiria kama wao ni tatizo kubwa sana nilijua ni akili za dada zangu tu yaani wanaweza kukwambia vitu ambavyo havipo kabisa kwenye kichwa chako. Au anatafsiri situation tofauti kabisa na uelewa wa mtu mwingine.

Lema anadhani DW au BBC ni sawa especially BBC ni sawa na TBC mtangazaji anajifanyia tu propaganda za ovyo ovyo analaumu baadhi ya wafanyakazi.

Hizo taasisi zinafuata utaratibu wa sheria na balancing story ni kipaumbele kwao kama ni story za upande mmoja utasikia jitihada za kumpata muhusika wa upande wa pili zilishindikana na waweke huo ushahidi wakiulizwa, kuna producer wa kipindi ukija mziki yeye ndio anaucheza sio reporter so kulaumu watangazaji wa njee ni shallow.

Pili raisi wa nchi usimchukulie poa maza akisafiri kuna wapambe kibao wanatangulia ata chakula cha hoteli anayo fikia kuna mtu anasimamia kinavyotayarishwa mpaka kinamfikia.

So ukisikia watu wanaenda kukutana na raisi moja kwa moja jua ubalozi umeandaa na wanaenda wapambe wao tu sio kila mtu atajua halipo unless ile mikutano ambayo alikuwa akifanya J.K na msafara wake sikia tu kuna watu luluki wanatangulia na wanakuwepo kwenye mikutano yake vinginevyo umuoni wala hujui alipofikia asipoamua.

Mfano Samia alipoenda Glasgow hakuna mtanzania alijua alipofikia na wala kukutana nae zaidi ya watu wake wa serikali waliotoka Tanzania na watu wa ubalozini ndio waliopo kwenye ile clip; lakini hakukuwa na diaspora ata mmoja pale.

Usidhani raisi akitoka nje ya nchi status yake na ulinzi unabadili kwa kiasi kikubwa ngoja siku aende Canada ndio atajua Lissu alipewa heshima tu ya kukutana na Samia na ndio maana akawa mnyenyekevu ulinzi wake sio wa mchezo na kukutana nae ni mission kweli kweli.

Malalamiko yake ni vitu anavyofikiria tu kichwani kwake tofauti na uhalisia dunia inavyozunguka.
@Kilatha

Umeongea ule UKWELI halisi 100%.

Sina la kuongeza....Big up.

Ahsante sana.
 
Zito alipomuombea Mbowe msamaha walisema kuwa Mbowe hastahili kuomba au kuombewa msahamaha ili aachiwe kwa kosa ambalo hakulifanya. Wakati huo huo Lisu anamuombea msamaha Mbowe kwa raisi Samia ili amsamehe kwa kosa ambalo eti hakulifanya. It doesn't make sense.
 
Back
Top Bottom