Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema ameonya wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ukimya ulioonyeshwa na jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya makamu wa mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu alipowasili nchini.
Lema ameonya hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, amesema wapinzani wanapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wa kawaida.
“Sina amani kwa tabia nzuri walioonyesha Jeshi la Polisi jana wakati wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu. Ninapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari, kuna kitu kinafikiriwa na sisi tunapaswa kufikiri zaidi” ameandika Lema.
Hapo jana Julai 27, 2020 mamia ya wanachama wa chama hicho wamejitokeza kwa wingi kumlaki makamu mwenyekiti wao, Tundu Lissu aliyerejea nchini baada ya miaka mitatu ya kupatiwa matibabu nchini Ubeligiji.