Lema: Uchaguzi wa Viongozi wa CHADEMA ni mwakani na Kuanzia Januari 2024 tunajipanga kwa Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
66,900
102,158
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema mh Lema amesema CCM wamemaliza Kipanga safu yao ya uongozi pale Dodoma juzi wakiusubiri Uchaguzi.

Chadema itafanya Uchaguzi wa Viongozi wake mwakani na Kuanzia January 2024 tutaanza mikakati ya kutafuta Ushindi kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu, amesisitiza Lema

Katika nyakati hizi tunatazama Mbele hatutarajii kupotezeana muda, amesema Nabii Lema huko space
 

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,487
10,838
Lema naye apunguze kuropoka. Uchaguzi gani?. Hakuna uchaguzi bila katiba mpya.
 

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
57,659
69,833
Jambo jema kabisa, uchaguzi tushiriki.
Ukiwa na kitu mkononi ni rahisi kufanya mazungumzo
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
15,137
55,337
Hawa sasa wanaonekana kila mmoja ni msemaji wa chama, huyu anasema hiki, mwingine anasema kile, bora sasa wakae kinya wafanye mkutano wao watoke na kauli moja kama chama, kwani hiki alichosema Lema kinaweza kuja kupingwa na mwingine.

Haya ndio madhara ya kukaa muda mrefu nje ya nchi, co ordination imekufa, sasa hivi wanajisemea tu kila mmoja na lake, Chadema imekuwa kama haina msemaji tena.

Haya yanayoendelea sasa yanaonesha udhaifu wa idara zilizopo ndani ya chama, na vile Mbowe anakaribia kustaafu 2023, naona mambo sasa ndio yameachwa yajiendee tu, viongozi wakae chini wapange mambo yao, waache huu utoto wa ku-post twitter kila linalowajia kichwani.
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom