Lema: Ubaguzi katika msiba wa kuaga wanafunzi waliofariki katika ajali ni ishara mbaya

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,205
Leo katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki ktk ajali . Mimi kama Mbunge mwenyeji niliyefiwa Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo hayo, ilikuwa ni itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor watapaswa kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili ya kutupa pole .

Nilisikia toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi wa Chadema watapaswa kutokuongea , nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro Mh Ole Nasha , nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili muhimu la kuaga watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais hasingeweza kukubaliana na ujinga huu.

Kwenye ratiba nilipoingia uwanjani , jina langu lilikuwepo kwenye ratiba kwa ajili ya salamu za rambirambi, lakini baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhiwa itifaki, mambo yalibadilika na ilionekana dhahiri kuwa sitakiwi kabisa kutoa pole kwa watu wa jimbo langu waliofikwa na msiba huu mbaya. M/kiti Mbowe aliandika meseji kwenda kwa M/ Rais kukumbusha umuhimu wa wenyeji kutoa salamu , Makamu wa Rais baada ya kupokea meseji hiyo, alimwita Mkuu wa Mkoa , ndipo ilionekana kama kuna ushindani unatokea kati yao , lakini hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kutoa salamu kwa wapendwa wetu.

Wabunge wa CCM waliokuwepo ambao ni mawaziri wote waliweza kutoa pole ,huu ni ubaguzi uliojaa ujinga na chuki mbaya kisiasa, nitaeleza madhara yake kwenye hotuba yangu kesho , lakini nafikiri watoto mara nyingi huwa wanafuata walichofundishwa na wazazi , pengine ingekuwa ni usaliti Mbunge Lema kusalimia na kuwapa pole watu wake mbele ya Makamu wa Rais. Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama nchi na Syria ni wakati.

Nawashukuru wote waliotukimbilia kwa matatizo yaliyotokea Arusha, Mungu awabariki sana. Msiogope , Mungu hadhiakiwi apandacho mtu ndicho avunacho

LEMA
 
Wakuu Nimeshangaa Mheshimiwa Godbless J Lema analalamika kwa kila jambo tena Kitu Kidogo Kabisa kwenye U busy wa shughuli nzito ya Leo hebu tuwe wastaarabu siyo lazima vitu vidogo tuu tukawekana ndani ni kweli Mbunge Lema hajatajwa na Alikua kakaa Karibu kila
IMG_20170508_145159_828.JPG
 
Mkuu wananchi wako hatuna shida mbona hata wakiwabagua ila sie twawapenda tu na tumeonyesha ushirikiano wa dhati na tunatambua uwepo wenu Kamanda, sijui ni lini hawa wenzetu wataacha siasa za maji taka, ni aibu kweli tena isiyo na kifani.Huyu Gambo huyu anyway wacha nikae kimya tu ila Mungu anamuona
 
Kamanda hao wajinga wala wasikuumize kichwa, hakuna wa kukutoa ndani ya mioyo ya watu wa Arusha..

Siku zote misiba na sherehe ndio huunganisha watu waliotofautiana mahala fulani, lakini ukiona mtu anatumia msiba kuendeleza tofauti zilizopo huyo ni mpuuzi wa kumpuuza tu..
 
Back
Top Bottom