Lema: Ubabe siyo dhambi, inategemea ubabe huo unaufanyia wapi

zinc

JF-Expert Member
May 24, 2013
1,392
1,066
Ndugu wana JF,

Katika kongamano la BAVICHA tulijadili miaka 52 ya uhuru pale eneo la Landmark hotel, Kamanda Lema alitoa hotuba yake fupi na yenye ujasiri na ya kuvutia sana.

Alitusihi na kutuhasa sana vijana wa leo kutokuwa na uwoga, Kamanda Lema alitueleza kwamba hata kama ni mtoto wake anamwosia kabla hajaondoka duniani hawezi kumueleza mtoto wake asome sana, bali atamueleza kwamba "HAKUNA DHAMBI MBAYA NA KUBWA DUNIANI KAMA WOGA".

Vijana wengi tulifurahi sana kwani kuna wasomi wengi ambao wamefanya mambo mabaya na ya kufedhehesha katika taifa, pia akatoa angalizo kuhusu Red brigade na Chadema vijana kwamba ni wakati wa kumlinda katibu mkuu wetu wa Chadema ambaye ni Dr Slaa, alihitimisha kwa kusema huu ubabe wa kijinga tunaofanyiwa na magamba tumechoshwa nao, sasa hatuwezi kuuvumilia kwa kuwa hata sisi (Chadema) tunaweza ubabe kwani "UBABE SIO DHAMBI INATEGEMEA UBABE HUO UNAUFANYIA WAPI".

Hapa ndipo napozidi kumkubali Kamanda Lema.
 
To be honest, mie pia ni mwanaCDM lakini lema cmkubali kabisa - infact ni mwanaharakati tu na wala c mwanasiasa! tazama hata kauli zake zimekaa kisharishari tu, ningependa kuona mwanasiasa kijana akiibua hoja flani na kuitetea kwa facts.

Mtoa mada, naomba unitajie hoja moja tu iliyoibuliwa na lema kwa manufaa ya eidha wana AR au hata TZ yote toka amekuwa mbunge.................... (n.b - usimlinganishe na mwingine yeyote coz mada mezani ni lema).
 
to be honest, mie pia ni mwanaCDM lakini lema cmkubali kabisa - infact ni mwanaharakati tu na wala c mwanasiasa! tazama hata kauli zake zimekaa kisharishari tu, ningependa kuona mwanasiasa kijana akiibua hoja flani na kuitetea kwa facts. mtoa mada, naomba unitajie hoja moja tu iliyoibuliwa na lema kwa manufaa ya eidha wana AR au hata TZ yote toka amekuwa mbunge.................... (n.b - usimlinganishe na mwingine yeyote coz mada mezani ni lema).

Uoga ni dhambi... hii fact inasaidia kulitibu taifa na kulinusuru
 
Mtu asiyethamini kisomo kipindi hiki huyo hana maana kabisa badala ya kushawishi kisomo cha kimapinduzi anasema eti watu wasiwe waoga bila hata kusema woga unatokaje wala kusema tofauti ya ujasiri wa critical mind na vurugu zisizo na tija!!!!!

Anahamasisha ubabe na mtoa mada anasema ni hotuba ya kuvutia sana na ukumbi ukakubali maneno haya ya kamanda????!!!!!!

Hivi BAVICHA ndio cream ya vijana wa chama,ndio tanuri la damu changa na fikra chipukizi???!!!!

I am disapointed with you guys!!!!!!
 
CCM wameishiwa na hoja, wamebaki kufanya maigizo, CHADEMA tuendelee kutangaza ukombozi wa fikra 2015 kitaeleweka tu
 
Nani anaemfuatilia huyu empty skull!

Nabii hakubaliki nyumbani,hata kipindi Lema alivyoongea kuhusu Zitto bado mlimponda,endelea kutumia utumbo mpana kifikiri.
Jaribu kuangalia Mapinduzi sehemu nyingi hayakuja kama wewe unafikiri.
 
to be honest, mie pia ni mwanaCDM lakini lema cmkubali kabisa - infact ni mwanaharakati tu na wala c mwanasiasa! tazama hata kauli zake zimekaa kisharishari tu, ningependa kuona mwanasiasa kijana akiibua hoja flani na kuitetea kwa facts. mtoa mada, naomba unitajie hoja moja tu iliyoibuliwa na lema kwa manufaa ya eidha wana AR au hata TZ yote toka amekuwa mbunge.................... (n.b - usimlinganishe na mwingine yeyote coz mada mezani ni lema).

Be honest is longer used my dia Open your eyes.
Lema ni kamanda wa ukweli kuliko unavyofikiri.Badilisha mtazamo wako,Usifikiri kuibua hoja pekee yake ndo solution vyitendo navyo ninahitajika kuweza kusukuma siasa.Usipende sana kutumia concept za wazee."leta hoja"ili kesho wakupoteze kimya kimya.
 
To be honest, mie pia ni mwanaCDM lakini lema cmkubali kabisa - infact ni mwanaharakati tu na wala c mwanasiasa! tazama hata kauli zake zimekaa kisharishari tu, ningependa kuona mwanasiasa kijana akiibua hoja flani na kuitetea kwa facts.

Mtoa mada, naomba unitajie hoja moja tu iliyoibuliwa na lema kwa manufaa ya eidha wana AR au hata TZ yote toka amekuwa mbunge.................... (n.b - usimlinganishe na mwingine yeyote coz mada mezani ni lema).

Hakuna mtu aliyekwishawahi kumuumbua waziri mkuu kwa kusema Uongo hadharani.
Bila Lema, Wasaliti ndani ya chama wangeendelea kuwepo mpaka leo na kufanikisha malengi ya CCM ya kukiua chama, bila Lema, tungeendelea kuwa na Madiwani mapandikizi Arusha, bila ya Lema, viti vinne vya Udiwani Arusha, CCM kwa wizi wao wangeweza kuambulia japo kimoja.
Bila Lema........
 
Respect kwako hon. GODBLESS Lema sababu ufahamu na siasa zako vimevuka viwango vya siasa za zidumu fikra,

Umeonyesha njia kwetu vijana kuwa " Inawezekana kupambana na serikali yeyote dhalimu hata kama serkali hiyo ina nguvu kiasi gani, na nyie wapambanaji mna udhaifu kiasi gani ila muhimu UJASIRI na kutokuwa WAOGA ndiyo kipimo na pishi la kimapinduzi katika harakati na zama zozote za kiukombozi,

Ujasiri wako umetufundisha kuwa "KUTOKUWA MWOGA ni zaidi ya degrees na PHDs, kwani hii ndiyo silaha kuu ya kutokomeza udhalimu na injustice katika jamii yeyote ile.

PEOPLE ADMIRES YOU LEMA.

HASTA LA VICTORIA SIEMPRE.
 
Last edited by a moderator:
Mh Lema ni alama ya ukombozi wa fikra, yeye ni nuru kwetu, amekuwa kioo angavu kwa waaminio kweli na kweli iwawekayo huru,

Nikimsikiliza Mh Lema hujihisi namsikiliza Steve Biko ama Sanz Ki,

Taifa linahitaji wenye mioyo na uoni kama wa Lema ili litamalaki kuelekea nchi ya ahadi yenye maziwa na asali
 
Mtu asiyethamini kisomo kipindi hiki huyo hana maana kabisa badala ya kushawishi kisomo cha kimapinduzi anasema eti watu wasiwe waoga bila hata kusema woga unatokaje wala kusema tofauti ya ujasiri wa critical mind na vurugu zisizo na tija!!!!!

Anahamasisha ubabe na mtoa mada anasema ni hotuba ya kuvutia sana na ukumbi ukakubali maneno haya ya kamanda????!!!!!!

Hivi BAVICHA ndio cream ya vijana wa chama,ndio tanuri la damu changa na fikra chipukizi???!!!!

I am disapointed with you guys!!!!!!

kwani KAPUYA siniprofesa, wewe unajifunza nn kutoka kwa kapuya? akili yako inafanana kabisa na mavi yako!!
 
  • Thanks
Reactions: mij
Nabii hakubaliki nyumbani,hata kipindi Lema alivyoongea kuhusu Zitto bado mlimponda,endelea kutumia utumbo mpana kifikiri.
Jaribu kuangalia Mapinduzi sehemu nyingi hayakuja kama wewe unafikiri.

WanaMAPINDUZI wote tuliowajua Duniani walioeleweka kwa kile walichokiamini na kukipigania maishani mwao haya niambie kuhusu huyu mtu wako msimamo wake nini?Kama ni posho anapokea na kama demokrasia yenye kujali haki ya kila mtu hata ya yule asiyepatana naye kitambo alishaitupa...Rejea aliyomfanyia Mwigamba kule Arusha.In short Lema wako huubiri kile asichokitenda,He is a big phoney of all time!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom