Lema: Serikali inapaswa kuanza kutoa ajira za mikataba baadhi ya maeneo

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
513
1,000
Kutokana na kukua kwa tatizo la ajira nchini na kushuka kwa uwezo wa serikali kuajiri, Mhe. God bless Lema kupitia space ya Maria Sarungi anashauri serikali kuanzisha mfumo ajira za mikataba ya miaka miwili ili watu waweze kupata kazi na kuendesha maisha kuliko kuendelea kung'ang'ania mfumo wa ajira za kudumu ambazo uwezo ni mdogo.

Nakubaliana na wazo hili kwa msingi kwamba kila budget ya serikali inapotengwa kuwepo fedha kiasi flan za ajira za mkataba ambapo nafasi na maeneo ya kimkakati yatapewa ajira hizo. Mfano unaweza ajiri waalimu wa vyuo kwaajili yakuwajengea uwezo kada flani, au ukaajiri Wataalamu wa afya wa kuwafunza watu flani.

Huu mfumo ndio unatumiwa na private sector n umeonyesha ufanisi mkubwa, lakini mfumo huu unasadia kupata Wataalamu wazuri ambao tunaweza kuwapa ajira za kudumu kulingana na uwezo wao wa kudelover na wale wasio na uwezo kuwaacha. Lakini pia mfumo huu utasaidia wahitimu kupata uzoefu nakukidhi takwa la uzoefu linalosumbua wahitimu wetu wengi sokoni.

Mwisho baadhi ya walio kwenye ajira za kudumu wataamua kuingia kwenye ajira za mkataba na hivyo kufungua milango ya replacement kutoka wasio na ajira.

Nini maoni yako kwenye wazo hili?
 

utah jazz

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
875
1,000
Kwa sekta binafsi ni rahisi kwasababu inaajiri watu wachache ila serkalini itakuwa ni hasara juu ya hasara kwani kulipa mafao kila baada ya muda mfupi ni mzigo kwa serikali.

Kumbuka nchi nyingi hata za dunia ya kwanza zinaongeza muda wa kustaafu kutoka 60 to 65 hadi 70 kutokana na mzigo wa kulipa mafao kuwa mkubwa huu ni mtazamo wangu sijafanya research
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom