Lema: Niko tayari kujiuzulu ubunge kama nilimtukana Dr. Burian

ZALEOLEO

Senior Member
Oct 11, 2011
116
18
Jana Leo alimwambia jaji Gabriel Rwakibasila kuwa Malalamiko ya dr Buriani kwa tume yalikua ya uongo kwani agosti 28,2010 aliyodai kuwa Lema alitoa matusi na kauli za kejeli na udhalilishaji hakufanya mkutano katika kata ya sombelini kama alivoeleza kwenye malalamiko yake bali alifanya mkutano sokoni 1. "Hakuna matusi yaliyotukanwa,ukinionesha matusi najiuzulu ubunge leo kukupunguzia kazi,kama kumwambia hakuweka dustbin(makasha ya taka) na kuwa alimshauri rais vibaya kuhusu ujenzi wa barabara ya serengeti ni vijembe hiyo ni sawa" katika hatua nyingine jana chadema waliahirisha mikutano yao ya kampeni baada ya mgombea wao joshua nassari kufiwa na baba yake mdogo anayeitwa Elisha nassari!
 
Maandishi mekundu> Hayo maneno aliyatamka akiwa wapi? kama siyo kujichanganya huko.
 
EL amesema amerudi fiti na yuko tayari kwa mapambano. Isije ikawa kumpora ubunge kamanda wetu ikawa ni sehemu yake ya mapambano??
 
batlida na wafuasi wake wote wana njaa ,tena kali.Wanahitaji maombi.....................
 
Japo mimi kisheria ni mweupe...kesi kama hii naiona ni misuse of national resources.
 
Mimi nilikuwepo kwenye hizo kampeni za Mhe Lema, ukweli wa mwenyezi Mungu Lema hakuwahi kumtukana Batilda hata kidogo zaidi ya kusema asichaguliwe kwakuwa amekuwa mbunge wa viti maalum kwa miaka kumi na waziri wa mazingira miaka mitano je alishindwa nini kuweka hata dustbin Arusha ili hali alikuwa kwenye position nzuri, leo akichaguliwa kuwa mbunge wa Arusha hatakuwa na mabadiliko yoyote kwakuwa ameolewa zanzibar na atarudi kwa mumewe zanzibar. Mimi sioni kama haya malalamiko yana mantiki yoyote wala sioni tusi hapo.... kwanza sijui hata kuna sababu gani ya kufuatilia hiyo kesi BATILDA mwenyewe wala hayupo hao mapopo bawa waliofungua kesi inaelekea hawana kazi za kufanya. ALWAYS PEOPLE'S POWER 4 EVER IN ARUSHA......
 
Back
Top Bottom