Lema na Nassary Walitikisa Bunge kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu..

Kwa wale mnaoendelea kutaka kujua ilivyokua, Kwa kifupi:
Alipewa nafasi Nassar kabla ya Lema. Swali la msingi lilikua kama mkakati wa serikali ni kubambikizia watu kesi. Anasema hilo wameligundua kutokana na wao kua watembeleaji wa magereza. Jibu: Serikali haiwezi kua na kazi hiyo; kama una specific issue ongea.
Ndipo Nasar akaongezea 'specific issue'. Akaelezea kijana aliyekamatwa Nzenga, akapelekwa Khm, akateswa Mwanza kwa kubinywa 'sirini' na kuvunjwa mkono; kabla ya kupelekwa Arusha ili akiri Lema kumtuma alipue bomu Olasit.
Jibu: w/mkuu hawezi kujibu swali la namna hii. But take from me, swala la Arusha ni nyeti na serikali itafuta waliohusika na kwanini walihusika.

Spika akamwita Lema. Lema akaanza ku-sound Olasit. Akaambiwa kaa chini, kanuni haziruhusu kurudia swali. Lema: Mlipanga kuniua, na Kisha mnapanga kunibambikizia kesi; niko emotional, na siwezi kuuliza swali jingine. Kijana mliyemtuma yupo hapo juu.


tragedy of the commons
 
upuuzi mtupu, kijana yupo tayari kutoa ushahidi bungeni kwani yeye ni mbunge?? kwani bunge ni mahakama?? ujinga mtupu, ni show off isiyokuwa na maana yoyote wala tija kwa watz

Kwani wachezaji wa Yanga walipoingia Bungeni walikuwa ni wabunge? Pia kwani Lema alidai anao ushahidi wa "kimahakama?"
 
Mwigullu hawezi kuchomoka kwenye hili! Kama poli-ccm wangekuwa makini walitakiwa wawe wamesha mkamata yeye na Nape kwa kauli zao za kuashiria mauwaji siku moja kabla ya mauwaji yenyewe.

Mtu yotote makini ataunganisha nukta na kuona ushiriki wa ccm kwenye kulipua bomu. Kwani hata wakisema wana kana kuwa hawaja lipua halafu tukalinganisha ripoti ya serikali iliyofichwa juu ya mauwaji ya Januari 5 wataweza kurukia wapi wakati ripoti imesema kabisa kuwa polisi walihusika na walidhamiria kuuwa?!!
 
Yupo kijana ambaye kwa zaidi ya miezi minne amekuwa katika mikono ya Polisi Shinyanga,Mwanza na Arusha akiteswa na kudhalilishwa huku akilazimishwa aseme Lema ndiye aliyemtuma kulipua bomu la Kanisani Arusha na pale kwenye Mkutano wa Soweto. Pamoja na kuteswa sana kijana huyu alikataa katakata mpango huo. Hadi Polisi walipogungua kuwa tarehe hizo mtuhumiwa wao alikuwa mahabusu kwa kesi nyingine ndio wakamuachia juzi.
swali la Nassari lilikuwa jee ni jukumu l serikali kubambika kesi raia wema? Kakosa jibu na Lema alipotaka kuuliza Makinda kasema anataka swali jipya naye kamjibu " siwezi uliza jipya maana nina mshtuko kwa vile mmetaka kuniua na sasa mnataka kunipa kesi ya mauaji "
AIBU YA SERIKALI NI KUWA HUYO MTUHUMIWA LEO YUPO HAPO BUNGENI KWENYE VISITORS GALLARY NA YUKO TAYARI KUSEMA YOTE MBELE YA WAZIRI MKUU. STAY TUNED KUJUA NINI KITATOKEA BAADAE.
JF siyo sehemu ya porojo mkuu weka ushahidi wa jina la huyo kijana.
 
Kijana? Huyo mnywa gongo kibaka WA Ngalelo nani hajui huo mchongo wa Lema?
 
mbona wameweweseka tu mkuu, lipi la maana waliloongea

Walioweweseka ni Serikali kuanzia kwa mkuu.
Bomu la Soweto limewafanya watanzania kuichukia serikali ya ccm kutokana na Rais kushindwa kuunda tume huru ya kuchunguza tukio lenyewe.
Bomu la Olasiti badala ya kumkamata mhusika polisi walichokifanya ni kumkamata dereva boda boda ambaye maskini ya mungu alikuwa hajui chochote.

CHADEMA wamesema wana ushahidi, lakini hawapo tayari kuukabidhi kwa watu ambao wao wanadhani ni sehemu ya mlipuko.
Rais aunde tume huru ya kijaji, kumwuliza pinda ni kumwonea, sana sana atasema ngoja ambeep rais ampigie
 
997008_786522868030329_2041137907_n.jpg
 
Mwigullu hawezi kuchomoka kwenye hili! Kama poli-ccm wangekuwa makini walitakiwa wawe wamesha mkamata yeye na Nape kwa kauli zao za kuashiria mauwaji siku moja kabla ya mauwaji yenyewe.

Mtu yotote makini ataunganisha nukta na kuona ushiriki wa ccm kwenye kulipua bomu. Kwani hata wakisema wana kana kuwa hawaja lipua halafu tukalinganisha ripoti ya serikali iliyofichwa juu ya mauwaji ya Januari 5 wataweza kurukia wapi wakati ripoti imesema kabisa kuwa polisi walihusika na walidhamiria kuuwa?!!
Polisi hawafanyi kazi kwa mapenzi yako wewe au ya Mbowe, wanafanya kazi kwa utaratibu wao, mnatuma watu wanalipuwa mabomu halafu mnatafuta huruma.
 
Mwisho wa ccm umefika, nawashangaa sana hawa watu wazima lakini wanafanya vitu ambavyo haviedani na umri wao wala dhamana waliyopewa na wananchi.
 
Nimewasikia Wote walipokua wanauliza Hilo swala na majibu ya PM!
Kwa mtazamo Wa haraka Hilo swala Bado ni gumu pamoja na Huyo Kijana kuwepo na majibu ya PM Bado Hilo Jambo gumu!
 
Polisi hawafanyi kazi kwa mapenzi yako wewe au ya Mbowe, wanafanya kazi kwa utaratibu wao, mnatuma watu wanalipuwa mabomu halafu mnatafuta huruma.

hAWAFANYI KWA UTARATIBU WAO; WANAFANYA KAZI KWA KUAMRISHWA NA VIONGOZI WA CCM WASIO WAADILIFU. YALIYOMKUTA MSHKAJI WA KISESA - MWANZA HAYATAISHIA HUKO TU.
 
Mwigulu Nchemba ndio muhusika wa matukio ya kulipua mabamu ya soweto na Olasit kwanini Waziri Mkuu anakuwa na kigugumizi na hilo kwanini vyombo vya dola havimuiti kumuhoji uhusika wake? Kwanini vijana wanakamatwa ovyoo na kuteswa ili kuwalazimisha kukiri kuwa Viongozi wa Chadema ndo wahusika wa matukio ya mabomu? Serikali ya CCM imeshindwa kuongoza ni wakati wake wa kufungashiwa virago!
 
Last edited by a moderator:
mbona wameweweseka tu mkuu, lipi la maana waliloongea

Jaribu kujisumbua kidogo fikra zako. Kitu muhimu ktk maswali yao kwa Waziri Mkuu sio majibu ya serikali bali kufikidha ujumbe kwa umma juu ya udhaifu wa serikali ktk masuala ya usalama wa nchi na watu wake, na kuendeleza shinikizo kwa serikali kushughulikia suala la mabomu ya Arusha.
 
JF siyo sehemu ya porojo mkuu weka ushahidi wa jina la huyo kijana.

Mwigulu anafahamu story za bomu la soweto, kuanzia jinsi bomu lilivyoingia nchini bila kustukiwa na usalama, ilivyosafirishwa kutoka Dar hadi Arusha bila kustukiwa na usalama, mpaka ilipotekeleza.
Mwigulu can precise that to you! Talk to him wacha kutafuta ushahidi humu
 
Hawakujipanga kuwasilisha hoja zao, nimewasikiliza, wanaonekana hawana mshauri. Nassary hajui kutofautisha kati ya swali, maelezo au hotuba. Waziri Mkuu kashindwa amjibuje, Lema naye kapewa nafasi ya kuongea akaanza kumwaga pumba zake, Ikabidi Spika amkatishe. Kanuni za Bunge ni Janga la kitaifa kwa wabunge wengi wa CHADEMA.

Hata kama mnajua kanuni msiunge mkono hoja za kuwatesa na kuwaua raia. Mambo ya vyama na siasa ni sehemu ndogo tuu ya maisha. Kumbuka tuwapo miskitini, makanisani, sokoni, vyuoni, mashuleni, kwenye vyombo vya usafiri, magereza na kwingine kwenye makusanyiko huwa hatukai kiitikadi za kivyama bali huwa tunakusanyika kama wanandugu au watanzania.
 
Back
Top Bottom