Lema na Nassary Walitikisa Bunge kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu..

M2.

Senior Member
Nov 27, 2013
160
53
Swala la Mabomu ya Soweto na Olasit laibuka tena bungeni, baada ya Kijana aliyebambikizwa kesi na kuteswa akilazimishwa kumtaja Lema kuwa ndo aliyemtuma kulipua mabomu hayo! Kijana yupo Bungeni tayari kumwaga ushahidi wake. Waziri mkuu amekosa majibu asema wampelekee katika maandishi.

Baada ya mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kukoswakoswa na bomu la Soweto yeye na Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe na kuua Watoto wadogo (3) na kiongozi wa chadema (1) na kuacha makumi bila viungo kama miguu, mikono. Sasa jeshi la polisi kwa kushirikiana na Mwigulu Nchemba liko kwenye harakati za kumubambikia Mhe. Lema kuwa yeye ndiyo aliyetuma mtu kwenda kulipua bomu kwenye kanisa la Olasti (St. Joseph Moyo safi) bahati mbaya sana kwa CCM na jeshi lake na bahati mzuri Kwa mhe. Lema na Chadema ni kuwa kijana huyo aligoma kabisa kusema/kutenda dhambi hiyo ya kusema uongo licha ya kwamba aliwahi kugombana na Mhe. Lema na akawaambia nina ugomvi na Lema lakini siwezi kumsingizia kitu kama hicho kijana huyo aliminywa sehemu za siri na kutishwa lakini alisimamia msimamo wake huo na akawaambia wakati wa mlipuko huo kijana(Nico) alikuwa gerezani kwa kesi nyingine.. Ndipo jeshi la polisi kwa aibu wakamwachia kijana huyo kwasasa yuko bungeni na alikuwa tayari kutoa maelezo hayo...

Lakini Waziri mkuu alimtaka Nasari akaandike maelezo ili ampelekee, kasimama Godbless Lema kukazia swali hilo Makinda akamwambia hairuhusiwi kurudia swali Lema akasema ana masikitiko makubwa kuwa yeye baada ya kukoswakoswa sasa anaandaliwa kesi ya kulazimishwa kuwa yeye alituma watu kuja kulipua bomu kanisani na baadae kwenye mkutano wa chadema soweto.
 
Haya sasa na huyo waziri mkuu na aendelee kudanganya bunge tu.

Safi sana Wabunge wangu tunawaamini na tunawajali. Mungu na awaongoze daima!
 
Swala la Mabomu ya Soweto na Olasit laibuka tena bungeni, baada ya Kijana aliyebambikizwa kesi na kuteswa akilazimishwa kumtaja Lema kuwa ndo aliyemtuma kulipua mabomu hayo! Kijana yupo Bungeni tayari kumwaga ushahidi wake. Waziri mkuu amekosa majibu asema wampelekee katika maandishi.

ndugu embu nyambua kidogo taarifa yako niielewe.
 
Tunaelekea pazuri sasa,watu kuwajibika ka kauli na matendo yao!!!!!
Watanue wigo mpaka elimu,afya na uchumi sio kukomalia siasa tu!!!!

Bravo kwa hili
 
Hivi Pinda kweli ni kiongozi mkuu wa serikali?anashindwaje kujibu swali ambalo ushahidi upo mbele yake?du! Serikali hii ni janga kwa Taifa.
 
Swala la Mabomu ya Soweto na Olasit laibuka tena bungeni, baada ya Kijana aliyebambikizwa kesi na kuteswa akilazimishwa kumtaja Lema kuwa ndo aliyemtuma kulipua mabomu hayo! Kijana yupo Bungeni tayari kumwaga ushahidi wake. Waziri mkuu amekosa majibu asema wampelekee katika maandishi.

Hebu eleza vizuri wametikisa je?
 
ndugu embu nyambua kidogo taarifa yako niielewe.

Nikwamba Nasaari alimuuliza swali PM kuhusu ubambikizaji wa wa kesi kwa wananchi, na akatoa scenario ya kijana aliyekamtwa akateswa akaswekwa ndani kwa muda mrefu akilazimishwa aseme ni Mh. Lema ndo aliyemtuma kulipua bomu la soweto na Olasit...
 
andika kwa kituo, ongezea minofu tuifaidi stori.

Baada ya mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kukoswakoswa na bomu la soweto yeye na Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe na kuua watanzania wanne. Sasa jeshila polisi liko kwenye harakati za kumubambikia Mhe. Lema kuwa yeye ndiyo aliye tuma mtu kwenda kulipua bomu bahati mbaya sana kwa CCM na jeshi lake na bahati mzuri Kwa mhe. Lema na Chadema ni kuwa kijana huyo pamoja na puminywa mapumbu aligoma kabisa kusema/kutenda dhambi hiyo licha ya kwamba kijana huyo alitumwa na Lema na akawaambia wakati wa mlipuko huo kijana huyo alikuwa gerezani kwa kesi nyingine..Ndipo jeshila polisi kwa aibu wakamwachia kijana huyo kwasasa yuko bungeni na alikuwa tayari kutoa maelezo hayo.
 
Mungu atawaumbua watenda maovu hao, huwezi kufanya uhalifu halafu ukaanza kufanya unyama kumshinikiza tena mtoto ili kusingizia wengine!
 
Pinda ameshindwa kujibu swali baada ya Lemapia kushidilia kuwa alitaka kuuwawa na na kumbe tena kuna watu wanalazimishwa waseme ni yeye aliyelipua hayo mabomu!
 
Back
Top Bottom