Lema na Nassary Walitikisa Bunge kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu..

Mungu atawaumbua watenda maovu hao, huwezi kufanya uhalifu halafu ukaanza kufanya unyama kumshinikiza tena mtoto ili kusingizia wengine!

Unafiki unaanzia kwa yule kiongozi mkuu sana wa nchi hii aliyejidai kukatiza ziara yake Oman ili kuja kuwapa pole wahanga wa bomu la Olasiti wakati mchezo mzima aliufahamu kabla
 
Pinda ameshindwa kujibu swali baada ya Lemapia kushidilia kuwa alitaka kuuwawa na na kumbe tena kuna watu wanalazimishwa waseme ni yeye aliyelipua hayo mabomu!

Nadhani alimaanisha kushindilia.. ujumbe si umeupata lakini..
 
padre aliejeruhiwa na mwingine kuuawa Zanzibar, sakata la Ulimbona na kibanda mbona hatujasikia polis wanakamata watuhumiwa ??!!!!
 
Baada ya mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kukoswakoswa na bomu la soweto yeye na Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe na kuua watanzania wanne. Sasa jeshila polisi liko kwenye harakati za kumubambikia Mhe. Lema kuwa yeye ndiyo aliye tuma mtu kwenda kulipua bomu bahati mbaya sana kwa CCM na jeshi lake na bahati mzuri Kwa mhe. Lema na Chadema ni kuwa kijana huyo pamoja na puminywa mapumbu aligoma kabisa kusema/kutenda dhambi hiyo licha ya kwamba kijana huyo alitumwa na Lema na akawaambia wakati wa mlipuko huo kijana huyo alikuwa gerezani kwa kesi nyingine..Ndipo jeshila polisi kwa aibu wakamwachia kijana huyo kwasasa yuko bungeni na alikuwa tayari kutoa maelezo hayo.
Mkuu nani ''aliwatoya'' hii ishu ya kuundwa mshtaka aisee babangu yeleuwiiiiiii
 
Hadithi njoo uongo njoo utamu koleaaa! Muheshimiwa mbona hii hadithi umeikatishia sifa yake moja ya utamu? Ongezea manyama basi tufaidi mkuu, mapicha mkuu
 
Swala la Mabomu ya Soweto na Olasit laibuka tena bungeni, baada ya Kijana aliyebambikizwa kesi na kuteswa akilazimishwa kumtaja Lema kuwa ndo aliyemtuma kulipua mabomu hayo! Kijana yupo Bungeni tayari kumwaga ushahidi wake. Waziri mkuu amekosa majibu asema wampelekee katika maandishi.

Baada ya mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kukoswakoswa na bomu la Soweto yeye na Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe na kuua Watoto wadogo (3) na kiongozi wa chadema (1) na kuacha makumi bila viungo kama miguu, mikono. Sasa jeshi la polisi kwa kushirikiana na Mwigulu Nchemba liko kwenye harakati za kumubambikia Mhe. Lema kuwa yeye ndiyo aliyetuma mtu kwenda kulipua bomu kwenye kanisa la Olasti (St. Joseph Moyo safi) bahati mbaya sana kwa CCM na jeshi lake na bahati mzuri Kwa mhe. Lema na Chadema ni kuwa kijana huyo aligoma kabisa kusema/kutenda dhambi hiyo ya kusema uongo licha ya kwamba aliwahi kugombana na Mhe. Lema na akawaambia nina ugomvi na Lema lakini siwezi kumsingizia kitu kama hicho kijana huyo aliminywa sehemu za siri na kutishwa lakini alisimamia msimamo wake huo na akawaambia wakati wa mlipuko huo kijana(Nico) alikuwa gerezani kwa kesi nyingine.. Ndipo jeshi la polisi kwa aibu wakamwachia kijana huyo kwasasa yuko bungeni na alikuwa tayari kutoa maelezo hayo...

Lakini Waziri mkuu alimtaka Nasari akaandike maelezo ili ampelekee, kasimama Godbless Lema kukazia swali hilo Makinda akamwambia hairuhusiwi kurudia swali Lema akasema ana masikitiko makubwa kuwa yeye baada ya kukoswakoswa sasa anaandaliwa kesi ya kulazimishwa kuwa yeye alituma watu kuja kulipua bomu kanisani na baadae kwenye mkutano wa chadema soweto.[/QUOTE


wadau ogopeni kumwaga damu zisizo na hatia kisa siasa au maslahi ya kundi fulani. ukimwaga damu isiyo na hatia ni laana juu ya ardhi. damu ina uhai na inalia hata kama huyo mtu mtakuwa mmemuondoa duniani lakini ataendelea kulia juu ya ardhi someni habari ya kaini na abeli. nchi yetu ilikuwa inafanikiwa kila nyanja lakini baada ya hii tabia ya kuuana tena kwa kutumia dola kila kitu hakiendi sababu ya damu zinazomllia MUNGU. kila mahali serikali inapojaribu kukwamua jambo inakwama na hata katika michezo wewe anagalia tunakwenda hatumalizi tunakwama. mapaka mabadilliko na matazamo wa walio madarakani ubadilike tena kwa toba ndipo tutajikwamua.
 
Tumieni akili zenu japo kidogo basi msikurupuke kwa kuwa mmezaliwa zamani, eti kwa kuwa tu mtuhumiwa kaletwa bungeni Pm akamhoji kwani kazi zake ni pamoja na za upelelezi au na mahakama pia anaruhusiwa kuingilia, ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi mnakurupuka mnachagua vilaza wanaenda kuwaaibisha bungeni hovyo kabisa nyie cdm.
Tumia akili. Lengo si kumwita ili aulizwe Bungeni, bali kuufahamisha umma kuwa mtu huyo yuko hapo Dodoma na akihitajika kutoa maelezo anapatikana. Pinda angeonekana kiongozi straight kama angemwambia Lema kuwa baada ya shughuli za Bunge mlete tuonane. Kama hujui huo ndio ulikuwa utendaji wa Marehemu Sokoine,hakuna kulaza jambo.
Nimemtaja Sokoine ila nina mashaka kama umenielewa maana yaweza kuwa mpaka anafariki ulikuwa hujazaliwa hivyo huelewi kitu.
 
Back
Top Bottom