Lema na Nassari sasa toeni ushahidi uliobaki ikiwemo "print out" ya mazungumzo ya simu

Mnyeti alishakubali haina haja tena. Game imekwisha
Magu akiwatumbua akina mnyeti hawa watakuja na mapambio kumpongeza
 
Mpaka sasa DC Mnyeti na madiwani wawili wamekanusha tuhuma mlizozielekeza kwao huku madiwani wawili wakiwatuhumu nyinyi kwa kutengeneza hizo video huku diwani mmoja akiziita hizo clip kuwa ni za kitoto.

Hivyo ili kukata mzizi wa fitina, nawashauri ikiwezekana hata kesho mtoe video ambazo awali hamkuzitoa pamoja na hiyo print out ya mazungumzo maana kejeli zimenza na zikisemwa sana bila nyinyi kuonyesha ushahidi wa ziada zitageuka kweli kwa baadhi ya watu hasa wale ambao sio wafuatiliaji wa mambo hivyo ni rahisi kudanganywa na hizi propaganda za baadhi ya wana-CCM.

Hatari ninayoina ni wanapropaganda hawa kuwageuzia nyinyi kibao kwa kujifanya wana mapenzi na CHADEMA na kuanza kuwazushia maneno kuwa mnakiweka chama pabaya licha ya wao mpaka sasa kushindwa kujibu tuhuma hizi pasipo kuacha shaka yoyote.

Kwa sasa hamna haja tena ya kumsitiri yoyote yule hata awe nani maana hii sasa ni sawa vita ambayo siku zote haina macho
Mkuu kisu kimeshakita mfupa, ndio vilio vitasikika toka kila sehemu.
 
Kesi tayari iko PCCB na ushahidi wote uliusikia na unaoutaka uko pale. Waambie PCCB waufanyie kazi haraka kama unavyotaka iwe. Na wasisite kutangaza walichobaini na hatua watakazochukua.
 
Naona wanatoa ushahidi kidogo kidogo kimkakati,hii naifananisha na kumkimbiza mwizi kimya kimya bila kupiga yowe,na mwizi mwenyewe akigeuka nyuma anaona uko hatua moja kutoka alipo,

Vijana wanahakikisha pressure ya kuwawajibisha hawa watoa rushwa haishuki,hapa ni anguko la serikali hii iliyojaa watoa rushwa

Nadhani tukio hili ni mfanano wa tukio la lipumba,nadhani lipumba naye yuko kwenye payroll ya mtu fulani ili kuivuruga CUF,tukio la Arusha na la Lipumba kuisumbua CUF yanafanana sana
Wamesema hii ni kama tamthilia ya isidingo, inatolewa kidogo kidogo.
 
Sasa mzigo si upo TAKUKURU....?? Mbn mnalialia..?? Wao Takukuru ndo watasema huo mzigo ni wa kitoto au kikubwa.

Nyie ni GREAT THINKERS bana. Msiyumbishwe na maneno ya kujitetea ya hao madiwani. Wat if ikija kuthibitika ni kweli..?? Mtaficha sura zenu wapi, kwny makalio au..??

Acheni Takukuru wafanye kazi yao.
 
Haisaidii chochote. Cha msingi wakae chini wajipange kujenga chama chao. Waelekeze fikera zao katika kuhudumia wananchi, waache siasa za mipasho.
Kujenga chama ni pamoja na Kuzuia Madiwani wao kuhama ikiwamo kugundua sababu na mbinu chafu ianayowafanya wahame
 
Kujenga chama ni pamoja na Kuzuia Madiwani wao kuhama ikiwamo kugundua sababu na mbinu chafu ianayowafanya wahame
Madiwani wanahama kufuata siasa safi. Kama chama chao kinegekuwa kina siasa safi madiwani wasingedhubutu kuwasaliti. Angalia CCM baada ya uchaguzi wa mwaka juzi, nani kahama? Wanazidi kujizolea wanachama lukuki.
 
Watahamaje wakati ndiko kwenye hela zote za Nchi ziko hapo??
 
Watahamaje wakati ndiko kwenye hela zote za Nchi ziko hapo??
Wahenga walisema ukitaka kumla nguruwe chagua aliyenona. Kwa nini basi hao madiwani wasiende kwenye hela? Ni nani nchi hii hapendi pesa? Waambieni hata hao akina Lema wajiunge na chama tawala watapata pesa.
 
Mpaka sasa DC Mnyeti na madiwani wawili wamekanusha tuhuma mlizozielekeza kwao huku madiwani wawili wakiwatuhumu nyinyi kwa kutengeneza hizo video huku diwani mmoja akiziita hizo clip kuwa ni za kitoto.

Hivyo ili kukata mzizi wa fitina, nawashauri ikiwezekana hata kesho mtoe video ambazo awali hamkuzitoa pamoja na hiyo print out ya mazungumzo maana kejeli zimenza na zikisemwa sana bila nyinyi kuonyesha ushahidi wa ziada zitageuka kweli kwa baadhi ya watu hasa wale ambao sio wafuatiliaji wa mambo hivyo ni rahisi kudanganywa na hizi propaganda za baadhi ya wana-CCM.

Hatari ninayoina ni wanapropaganda hawa kuwageuzia nyinyi kibao kwa kujifanya wana mapenzi na CHADEMA na kuanza kuwazushia maneno kuwa mnakiweka chama pabaya licha ya wao mpaka sasa kushindwa kujibu tuhuma hizi pasipo kuacha shaka yoyote.

Kwa sasa hamna haja tena ya kumsitiri yoyote yule hata awe nani maana hii sasa ni sawa vita ambayo siku zote haina macho
Ninaamini sasa makamanda vijana watalipua bomu kuu kuliko yote wait tick---tick --tick--
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom