Tetesi: Lema na lisu ndio wapinzani wa kweli!!

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
885
Heshima yenu wakuu wa jukwaa hili, pia heri ya krismass na mwaka mpya.

Nchi zetu za kiafrica, zinazoongozwa na viongozi ambao kwa hiyari yao hawako tayari kuachia madaraka kwa amani. Ni nchi ambazo viongozi wake wamegeuka kuwa miungu watu, wana kibuli, wanatibu haja ya njaa zao kwa kujilimbikiza mali za umma, wala rushwa na mafisadi waliokubuhu.

Katika nchi hizi neno demokrasia imekuwa ni msamiati mgeni. Kupitia mwamvuli huu wa demokrasia wamekuwa wakirithishana madaraka kwa kujuana. Na uongozi umegeuka kuwa zawadi ama fadhira kwa jamaa zao huku wananchi wanyonge na masikini wakiishi kwenye lindi la umaskini na huduma za jamii zikisuasua au kusinzia kabisa.

Nchi yetu Tanzania tangu imepata uhuru mwaka 1961 imeongozwa na chama kimoja ndicho kimekuwa madarakani hadi leo, sanjali kwamba mwaka 1992 nchi iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi na mfumo huo ukaanza kutumika mwaka 1995, ambapo ilisemekana kuwa chama tawala kilishindwa kwenye uchaguzi huo ila kilitumia mabavu yake kukibakisha madarakani. Ni chaguzi kadhaa ambazo zimekuwa na dalili za wazi za kushindwa kwa chama tawala kushika dora, ikiwepo uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya kampeni tu ingetosha kuhukumu kuwa chama tawala kilikuwa ICU kikipumulia mipira, ila kilishinda kwa mazingaombwe na figisu za watawala walioweka mizizi ndani ya serikali.

Tunahitaji wapinzani wa kweli siyo waigizaji na wachumia tumbo watakaoendesha movement ya kukitoa hiki chama kikongwe kilichojichokea.

Wapinzani ambao watakabiliana na watawala iwe mahakamani, polisi, kwenye majukwaa ya kisiasa ama mbele ya watanzania. Godbless Lema ameonyesha siasa za upinzani wa kweli. Huyu ni mwanasiasa chipukizi mwenye ushawishi mkubwa na asiyekuwa na chembe ya uoga. Lema amekuwa mpambanaji, mwanamapinduzi na anayeitetea haki.....
Hajali madhara anayoyapata katika harakati za kuidai haki bali ameyatoa maisha yake na ya familia yake kupigania haki ya umma! Huyu ni mpinzani wa kweli anayefuata nyayo za kina Martin Luther King, Nelson Mandela na Marianne Angelle. Lema, waarusha wote na watanzania kwa ujumla wanakuunga mkono, haki ya kweli siku moja itapatikana.

Tundu lisu ni mwanasiasa nguli wa siasa za upinzani wa Tanzania. Harakati zake hazina woga, pia amekuwa mpambanaji na mwenye kupaza sauti. Hatishwi, ni mtaalamu, msomi na mahili wa vifungu vya sheria. Umahili huu wa sheria umempa umaarufu mkubwa wa kuweza kuikabili serikali mahakamani na mara kadhaa kuibuka mshindi.

Nawasihi wapinzani wenzangu, tuwape nafasi watu hawa watuvushe katika mapambano ya hizi serikali dhalimu.

Nawasilisha!!
 
Mkuu hawa uliowataja umemsahau Msigwa ambao kwa sisi wenye akili timamu tunawaona kama mambumbu wa siasa na si wapinzani wa kweli kama unavyotaka tuamini bali ni kati ya watanzania wanaotumia majukwaa ya siasa kudhihirisha ukosefu wa hekima na busara katika kujadili na kutafakari masuala muhimu ya taifa letu.
 
Mbumbu ndo nn?
 
Ilo liko wazi kabisa tunakaa tunasumbuliwa na wanasiasa uchwara kama Lowassa eti alete mabadiliko.........

Toka lini fisadi akaleta mabadiliko kokote duniani?.......

Ndiye alitaka kwenda Ikulu kwa katiba mbovu tuliyonayo ili ale nchi na kuimaliza........

Naamini watu kama Lema na Lissu hata kama hamtawaelewa sasa ila kuna siku mtakuja kuwaelewa tu tuendako........
 
Uko sawa mkuu, wengine mapoyoyo tu wanatupotezea muda.

Siku zote huwa nasema wapigania haki wa ukwel wakiibuka niko tayari kuwaunga mkono. Sio mijitu isiyoeleweka tulioyonayo sasa.
 
Mkuu hawa uliowataja umemsahau Msigwa ambao kwa sisi wenye akili timamu tunawaona kama mambumbu wa siasa na si wapinzani wa kweli kama unavyotaka tuamini bali ni kati ya watanzania wanaotumia majukwaa ya siasa kudhihirisha ukosefu wa hekima na busara katika kujadili na kutafakari masuala muhimu ya taifa letu.
Wewe una ukata wa mawazo, unapenda siasa za kubembelezana na kusujudiana. Kwa mtindo huu tutegemee ccm kuongoza miaka mia mbele
 
Heshima yenu wakuu wa jukwaa hili, pia heri ya krismass na mwaka mpya.

Nchi zetu za kiafrica, zinazoongozwa na viongozi ambao kwa hiyari yao hawako tayari kuachia madaraka kwa amani. Ni nchi ambazo viongozi wake wamegeuka kuwa miungu watu, wana kibuli, wanatibu haja ya njaa zao kwa kujilimbikiza mali za umma, wala rushwa na mafisadi waliokubuhu.

Katika nchi hizi neno demokrasia imekuwa ni msamiati mgeni. Kupitia mwamvuli huu wa demokrasia wamekuwa wakirithishana madaraka kwa kujuana. Na uongozi umegeuka kuwa zawadi ama fadhira kwa jamaa zao huku wananchi wanyonge na masikini wakiishi kwenye lindi la umaskini na huduma za jamii zikisuasua au kusinzia kabisa.

Nchi yetu Tanzania tangu imepata uhuru mwaka 1961 imeongozwa na chama kimoja ndicho kimekuwa madarakani hadi leo, sanjali kwamba mwaka 1992 nchi iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi na mfumo huo ukaanza kutumika mwaka 1995, ambapo ilisemekana kuwa chama tawala kilishindwa kwenye uchaguzi huo ila kilitumia mabavu yake kukibakisha madarakani. Ni chaguzi kadhaa ambazo zimekuwa na dalili za wazi za kushindwa kwa chama tawala kushika dora, ikiwepo uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya kampeni tu ingetosha kuhukumu kuwa chama tawala kilikuwa ICU kikipumulia mipira, ila kilishinda kwa mazingaombwe na figisu za watawala walioweka mizizi ndani ya serikali.

Tunahitaji wapinzani wa kweli siyo waigizaji na wachumia tumbo watakaoendesha movement ya kukitoa hiki chama kikongwe kilichojichokea.

Wapinzani ambao watakabiliana na watawala iwe mahakamani, polisi, kwenye majukwaa ya kisiasa ama mbele ya watanzania. Godbless Lema ameonyesha siasa za upinzani wa kweli. Huyu ni mwanasiasa chipukizi mwenye ushawishi mkubwa na asiyekuwa na chembe ya uoga. Lema amekuwa mpambanaji, mwanamapinduzi na anayeitetea haki.....
Hajali madhara anayoyapata katika harakati za kuidai haki bali ameyatoa maisha yake na ya familia yake kupigania haki ya umma! Huyu ni mpinzani wa kweli anayefuata nyayo za kina Martin Luther King, Nelson Mandela na Marianne Angelle. Lema, waarusha wote na watanzania kwa ujumla wanakuunga mkono, haki ya kweli siku moja itapatikana.

Tundu lisu ni mwanasiasa nguli wa siasa za upinzani wa Tanzania. Harakati zake hazina woga, pia amekuwa mpambanaji na mwenye kupaza sauti. Hatishwi, ni mtaalamu, msomi na mahili wa vifungu vya sheria. Umahili huu wa sheria umempa umaarufu mkubwa wa kuweza kuikabili serikali mahakamani na mara kadhaa kuibuka mshindi.

Nawasihi wapinzani wenzangu, tuwape nafasi watu hawa watuvushe katika mapambano ya hizi serikali dhalimu.

Nawasilisha!!
Sio "wapinzani wa kweli"..ni "wapiga kelele za kweli"
 
Nashindwa kukuelewa,hivi mpinzani wewe unaeona anafaa ni yule asiogopa tu au?siasa za kiafrika haziwezi kubadilika kama akili ndiyo hiyo,mpinzani wa maana karne ya 21 siyo asiyo ogopa na kutukana,mpinzani wa kweli ni yule mwenye kujua maslahi ya wapiga kura wake na mwenye kushindania maendeleo kwenye jimbo lake,lazima uonyeshe maendeleo kwenye jimbo kabla hujafikiria kupewa nchi,hivi ukiota au kumtukana rais kwa watu wenye akili inatosha kuwa mwanasiasa mahiri?kwa mimi mpinzani ni yule mwenye kupinga hoja mbovu za serikali kwa kutumia lugha ya kistaarabu na kuungamkona hoja yenye maslahi na watu wake,mfano ni nasari anajuwa kerokubwa kwa wapiga kura wake ni ardhi na anaisukuma serikali kutatua kero hizo,ikifika wakati wa uchaguzi yeye ndiyo aliotatua hiyo kero,lakini leo unasema lowasa hafai kesho anafaa na wale wenye msimamo ambao huona bado hafai ni adui,mimi nilidhani ungesema Dr slaa ni mwanasiasa mwenye msimamo alipinga ufisadi na wasio na akili wakamwona ni adui ,na walio aminisha watu ni hao unaowaita wanasiasa,upinzani wa kweli hauwezi tokea kwenye mkoa wa kilimanjaro,historia iko wazi walimpinga nyerere na kumkejeli akitafuta uhuru leo wanatafuta ukombozi upi,kwa wenzetu wa kilimanjaro hela kwanza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom