mcrounmj
JF-Expert Member
- Feb 26, 2016
- 380
- 885
Heshima yenu wakuu wa jukwaa hili, pia heri ya krismass na mwaka mpya.
Nchi zetu za kiafrica, zinazoongozwa na viongozi ambao kwa hiyari yao hawako tayari kuachia madaraka kwa amani. Ni nchi ambazo viongozi wake wamegeuka kuwa miungu watu, wana kibuli, wanatibu haja ya njaa zao kwa kujilimbikiza mali za umma, wala rushwa na mafisadi waliokubuhu.
Katika nchi hizi neno demokrasia imekuwa ni msamiati mgeni. Kupitia mwamvuli huu wa demokrasia wamekuwa wakirithishana madaraka kwa kujuana. Na uongozi umegeuka kuwa zawadi ama fadhira kwa jamaa zao huku wananchi wanyonge na masikini wakiishi kwenye lindi la umaskini na huduma za jamii zikisuasua au kusinzia kabisa.
Nchi yetu Tanzania tangu imepata uhuru mwaka 1961 imeongozwa na chama kimoja ndicho kimekuwa madarakani hadi leo, sanjali kwamba mwaka 1992 nchi iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi na mfumo huo ukaanza kutumika mwaka 1995, ambapo ilisemekana kuwa chama tawala kilishindwa kwenye uchaguzi huo ila kilitumia mabavu yake kukibakisha madarakani. Ni chaguzi kadhaa ambazo zimekuwa na dalili za wazi za kushindwa kwa chama tawala kushika dora, ikiwepo uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya kampeni tu ingetosha kuhukumu kuwa chama tawala kilikuwa ICU kikipumulia mipira, ila kilishinda kwa mazingaombwe na figisu za watawala walioweka mizizi ndani ya serikali.
Tunahitaji wapinzani wa kweli siyo waigizaji na wachumia tumbo watakaoendesha movement ya kukitoa hiki chama kikongwe kilichojichokea.
Wapinzani ambao watakabiliana na watawala iwe mahakamani, polisi, kwenye majukwaa ya kisiasa ama mbele ya watanzania. Godbless Lema ameonyesha siasa za upinzani wa kweli. Huyu ni mwanasiasa chipukizi mwenye ushawishi mkubwa na asiyekuwa na chembe ya uoga. Lema amekuwa mpambanaji, mwanamapinduzi na anayeitetea haki.....
Hajali madhara anayoyapata katika harakati za kuidai haki bali ameyatoa maisha yake na ya familia yake kupigania haki ya umma! Huyu ni mpinzani wa kweli anayefuata nyayo za kina Martin Luther King, Nelson Mandela na Marianne Angelle. Lema, waarusha wote na watanzania kwa ujumla wanakuunga mkono, haki ya kweli siku moja itapatikana.
Tundu lisu ni mwanasiasa nguli wa siasa za upinzani wa Tanzania. Harakati zake hazina woga, pia amekuwa mpambanaji na mwenye kupaza sauti. Hatishwi, ni mtaalamu, msomi na mahili wa vifungu vya sheria. Umahili huu wa sheria umempa umaarufu mkubwa wa kuweza kuikabili serikali mahakamani na mara kadhaa kuibuka mshindi.
Nawasihi wapinzani wenzangu, tuwape nafasi watu hawa watuvushe katika mapambano ya hizi serikali dhalimu.
Nawasilisha!!