Lema: Magembe ni Waziri Mzigo na Medeye ni bomu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,
Japo nilikuwa namuona Mhe. Godless Lema kama kichwa Nazi fulani kutokana na ule utumbo wake humu dhidi ya ZZK, naomba kukiri wazi Mhe. Godless Lema ni Kiboko!.

Sakata lenyewe lilianza hivi!,

Mhe. Ole Medeye ameomba muongozo wa spika kuwa Mhe. Godless Lema, amemtolea matamshi ya uongo kuwa yeye ni mbaguzi wa Wachagga kushika uongozi Arusha, hivyo matamshi hayo yamemdhalilisha na Kimvunjia heshima, yeye na familia yake, akaomba muongozo wa spika Mhe. Lema athibitishe kauli hizo za kibaguzi Ole Medeye alizitoa lini na wapi ?.




Naibu Spika, Mhe. Ndugai akasema kwa vile Mhe. Lema yupo analolote la kujibu!. Kiukweli hili lilikuwa kosa!, ni kama kichaa kapewa rungu na hapo hapo akatwanga!. Kama Waziri Magembe ni mzigo!, Ole Medeye ni bomu la hatari sana linalosubiri kulipuka!. Ni mbaguzi mkuu!, DVD zipo kwenye U-Tube (angalia video hapo juu).

Ukumbi kimya!.

Prof. Maghembe naye akaomba muongozo wa spika kwa nini Mhe. Lema amemtaja?!. Naibu Spika akampa tena Lema fursa ya kujibu!, hili ni kosa jingine, Mhe. Lema akapiga nyundo nyingine ya kichwa kwa Prof.Maghembe bila kupapasa wala kumungunya, kuwa Katibu Mkuu wa CCM na Mwenezi wa CCM ndio waliomtaja yeye Maghembe kuwa ni mzigo na CC ya CCM imeisha muita kumhoji!. Akasisitiza kama Maghembe ni mzigo, Ole Medeye ni bomu la hatari sana linalosubiri kulipuka!.

My Take.
Nimemkubali Mhe. Lema!, ni very bold, a dare devil, ambaye hamungunyi maneno he just call a spade a spade!.

Naomba kuwasilisha.
Pasco
 
Last edited by a moderator:
mbunge wetu Lema mida hii kazua balaa bungeni Baada ya Magembe na Medeye kuomba mwongozo wa spika Baada ya kusema kuwa Medeye ni bomu na Magembe ni mzigo
 
Bwana Pasco hukuwa na haja ya kuanzisha thread kama hiki ndio umeona ukiandike, au unaogopa utakosa bahasha kwa kuandika kitu positive about Lema?
Kama umeamua kuanzisha thread basi toa full maelezo sio unaandika kama unafukuzwa ilhali unajua sio wote wenye access ya kuangalia bunge.
 
Last edited by a moderator:
Shida ni nini kuwahi kupost? Ila amesema ni mzigo kwa mr maghembe na kuna siasa za arusha ukabila licha ya kuoa mchaga. Na ana dvd . Ila lema analipua shida yake ni nini hasa?


Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Wanabodi,
Japo nilikuwa namuona Mhe. Godless Lema kama kichwa Nazi fulani kutokana na ule utumbo wake humu dhidi ya ZZK, naomba kukiri wazi Mhe. Godless Lema ni Kiboko!.

Nipo Dilema!!!!!!!!
 
wanabodi,
japo nilikuwa namuona mhe. Godless lema kama kichwa nazi fulani kutokana na ule utumbo wake humu dhidi ya zzk, naomba kukiri wazi mhe. Godless lema ni kiboko!.

amefanya kipi kilichoondoa ukichwa nazi wake?
 
wanabodi,
japo nilikuwa namuona mhe. Godless lema kama kichwa nazi fulani kutokana na ule utumbo wake humu dhidi ya zzk, naomba kukiri wazi mhe. Godless lema ni kiboko!.

mkuu lema ni kiboko wa kufanya nini?labda kuropoka.
 
Amenikumbusha kipindi anamwambia wassira kwamba ni mwoga live ..

Kawaida tu, yeye kafanya kunukuu tu walichosema akina kinana na nape dhidi ya magembe na hiyo cd aliyorekodi kwenye mkutano...
mimi natamuona Kamanda pale atakapofukunyua ufisadi ndani ya wizara,idara au taasisi yoyote ya umma.si kunukuu.
aanzishe mada na apeleke hoja binafsi aonyeshe ukamanda wake.
 
Ha ha ha ha ama kweli Lema ni kiboko ya waongo wote BUNGENI, hadi watakapo punguka; juzi tu Pinda karudia kuongopa sijui MB LEMA hakumwona !! Hadi Prof. Maghembe kaomba Poo. Namhurumia Job Ndugai make timbwili zote zina angukia cku zake ila leo ka kwepa kukurupuka.
 
Wanabodi,
Japo nilikuwa namuona Mhe. Godless Lema kama kichwa Nazi fulani kutokana na ule utumbo wake humu dhidi ya ZZK, naomba kukiri wazi Mhe. Godless Lema ni Kiboko!.
mkuu Pasco , ni wewe au ID yako imeingiliwa?
 
Last edited by a moderator:
kawaida tu, yeye kafanya kunukuu tu walichosema akina kinana na nape dhidi ya magembe na hiyo cd aliyorekodi kwenye mkutano...
Mimi natamuona kamanda pale atakapofukunyua ufisadi ndani ya wizara,idara au taasisi yoyote ya umma.si kunukuu.
Aanzishe mada na apeleke hoja binafsi aonyeshe ukamanda wake.

Godbless J Lema ni mdandia hoja, hana uwezo wa kuandika hoja binafsi.

Kitu kinacho itwa hoja ni sumu kwa lema.
 
Last edited by a moderator:
Leo Mheshimiwa Lema kasema yuko na ushahidi wa Naibu waziri kuhubiri ukabila, amesema ushahidi anao, aambiwe tu wapi kwa kuupeleka, na akasema ushahidi wenyewe hata katika youtube upo.

sasa ushahidi wenyewe huu hapa.



mtaoweza kuwatafsiria wengine tutashukuru.
 
Last edited by a moderator:
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom