Lema, Lissu na Nassari washambulia Arusha leo

kila mtu ana wazimu ila wazimu wa wengine unatia mashaka kama hata akili za kibinadamu wanazo
 
Jana Lisu alikuwa Mwanza, leo yupo Arusha wakati jimboni kwake wanakufa njaa.

Sifa kijinga.
Kama kweli wanakufa njaa kwanini serikali isipeleke mahindi ya msaada kama walivyo fanya Igunga? Fikiria kabla ya kujibu hoja
 
Jamani JF naomba tujadili hoja inayoletwa jamvini kuliko post moja kujibiwa na watu wengi kiasi kwamba tunapoteza radha ya hoja husika kujadiliwa

Binafsi nawapa BRAVO CDM Ila sasa wakumbuke vijijini mjini wengi wameokoka
 
inauma acha kufikiri kwa kutumia makalio yako kijana, hiyo siyo kazi yake, ona sasa yanavyokuaibisha, acha uvivu wa kufikiri tumia bongo yako vizuri, 2005 kikwete aliongoza kusimama kwenye makanisa akisema yeye ni chaguo la Mungu, sasa kipi chama cha kanisa katii ya ..... na .....? lisu ni kamanda wa ukweli hajaanza harakati juzi wala jana so Tz inampata A 2 Z kwa kutetea wanyonge kazi yake ni kuwasilisha kero serikalini, serikali inalala usingizi we unasema watu wanakufa na njaa?
 
Kwa maneno mengine ndugu Mzee unatutangazia kuwa chini ya serikali ya CCM kuna watu wanaokufa njaa? Pengine utufafanulie, kwa nini watu wanakufa njaa? Nani mwenye jukumu la kuhakikisha wananchi wanakuwa na chakula cha kutosha? Professor Magembe na wizara yake wanalipwa mshahara kufanya nini?

Mh Lissu is a legislature (mtunga sheria) na sio waziri wa chakula. Na chama anachotoka Mheshimwa Lissu, hakikusanyi kodi. Kama serikali iliyopo imeshindwa kutimiza moja ya majukumu yake ya msingi (kulisha wananchi wake) kwa nini wanang'ang'ania kuendelea kukaa madarakani. Hivi Professor Magembe na CCM nzima wakiitwa waongo na waujaji itakoa kosa? Ni mara ngapi tumewasikia wanasema HAKUNA MTANZANIA ATAKAYEFUKA NJAA?
Mkubwa hapo unakosea (kwenye nyekundu). Our government is decentralised, kuna LGAs na mbunge ni mjumbe wa LGA iliyopo jimboni mwake. Badala ya ku- walk out na madiwani wake, labda wangekaa chini na kujadiliana jinsi ya kuwapatia chakula wananchi wenzao. Charity begins at home, at least be vocal about it!! let the world know about it. Nilipendezeshwa sana aliposimama kidedea kuhusu Barrick gold na Nyamongo killings. Huku marekanwafanyakazi wenzangu walikuwa wananiuliza kuhusu Nyamongo, Magazeti ya Canada, websites zote zilikuwa zikindirima na jina la Lissu lilikuwa everywhere.
Badala ya kwenda kwenye kampeni za udiwani na kuanza kuongelea mipasho, ni vyema asimamie kidedea wnajimbo wenzake angalau wapate chakula, angalau malori kadhaa ya mahindi, mwenye mbuzi, kuku, ng'ombe , mtama, ulezi... etc Tanzania hatutakiwi kufa kwa njaa.
 
kila siku arusha,mwanza,tegeta.kwa nini wasije huku kijijini kwetu kikonga?au wanasubiri uchaguzi mkuu wakati wa kampeni.

Huko kijijini kwenu si ccm tu? Hata muelimishe vipi ? Wakati wa kampeni pilau, kofia, kanga na buku mbili mbili. Huko ndipo mtaji wa chama cha m.... Ulipo mkuu. Ila usjali pole pole cdm watakuja.
 
Hongera viongozi wa chadema,ongozeni mapambano kupambana na hawa mafisadi na vibara wao ambao wanaleta post za kipuuzi kwa kukataa ukweli na kutaka kuficha ukweli ulio wazi.na kwa taarifa ya wewe unaeona wabunge wetu wanatembea sana huo ni mwanzo tu utayaona na kusikia mengi kazi ndo kwanza inaanza,hao ndo wawakilishi wa wananchi sio mibunge mifisadi ambayo ni mibunge ya mafisadi,kama nyie mna wabunge wa watu alikuwa wapi mbunge anaewakilisha wananchi waliovunjiwa nyumba zao kuhakikisha wanafanya mazungumzo ya amani nia kupata suluhu?
Endelezeni mapambano wana chadema.
 
Wanaweka mazingira ya kujiandikia posho.

Najua baadae wataenda Dodoma kujifanya kuwatetea wananchi waliovamia eneo.
 
Jamani JF naomba tujadili hoja inayoletwa jamvini kuliko post moja kujibiwa na watu wengi kiasi kwamba tunapoteza radha ya hoja husika kujadiliwa

Binafsi nawapa BRAVO CDM Ila sasa wakumbuke vijijini mjini wengi wameokoka

watampata nani kijijini!.

Vijijini wapo wazee wenye uwezo wa kufikiria, wanajua wametoka wapi na wanakwenda wapi. Hawawezi kuhamasishwa vurugu.
 
Siyo kazi ya Lissu kupeleka chakula jimboni mwake. Mathalani kashafikisha hilo swala la uhaba wa chakula serikalini, kilichobaki ni kazi ya serikali yako. Serikali inavizia sehemu zenye uchaguzi mdogo ndiko inapeleka chakula. Wote tumeshuhudia kilichotokea Igunga wakati wa kampeni wa uchaguzi mdogo, leo hii tunavyozungumza hapa ni kwamba serikali imeacha kusambaza chakula huko Igunga. Inasubiri uchaguzi mdogo mwingine..

kwahiyo jukumu la mbunge ni kuipelekea serikali taarifa serikali!. Mbunge lazma apate muda wa kukaa na madiwani na kuangalia jinsi gani ya kutatua matatizo yanayowakabili.
 
Hivi wewe hujui ni nani anayekusanya kodi? Tundu Lissu unataka awalishe wana Singida kwa mshahara wake?

uwezo huo hana. Lazma atulie jimboni kwake akae na madiwani wapange jinsi gani ya kutatua matatizo sio kuzunguka Tanzania nzima kutafuta sifa.
 
magwanda mmezoea matusi. Shika adabu yako.

Mzee juzi matusi yamerushwa hadharani kule Mwanza juu ya kuwashikisha watu ukuta leo unawatukana Chadema humu .Una ushahidi mwandishi aliyekupa dose ni mwana Chadema ? Maana hapa si ofisi ya Chadena ila kuna watanzania hawaipendi CCM na bado si wana Chadema .
 
Jana Lisu alikuwa Mwanza, leo yupo Arusha wakati jimboni kwake wanakufa njaa.

Sifa kijinga.


''Hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa'' Pinda na magamba walisisiza sana hili Igunga je watu wa Iramba jimboni kwa Lissu sio watz?
 
''Hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa'' Pinda na magamba walisisiza sana hili Igunga je watu wa Iramba jimboni kwa Lissu sio watz?

Mkuu Mzee ana fitina wewe au inaweza kuwa ni stress juu ya kasi ya Chadema mpe pole tu .
 
watampata nani kijijini!.

Vijijini wapo wazee wenye uwezo wa kufikiria, wanajua wametoka wapi na wanakwenda wapi. Hawawezi kuhamasishwa vurugu.

ujana kwenda uzee na baada uzee kwenda kifo..
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom