Lema: Kuna uwezakano wa Mayor/ wenzake kuwepo mahabusu mpaka wiki ijayo. Lakini kila mtu ajue

Kwa miaka 23 tumeshuhudia nchi ikiongozwa na utawala wa Visasi,Chuki na Ubaguzi. Wanachopanda ndicho watakachovuna.Hakuna chenye mwanzo kikakosa mwisho.Hata Yesu aliishi miaka 33 na alikuwa Mwana wa Mungu Sembuse CCM
Kwani ccm wote ni wakristo?
 
Maneno ya Lema si ya kupuuzwa hata kidogo, anajua anachokifanya na ndio maana anaongea kwa kujiamini, hata mimi nakiri wazi kabisa..time alone..time will tell..huwezi ukapeleka mambo kiubabe bila kufuata maridhiano aisee! Mayor na viongozi wa dini waliokamatwa wana makosa gani? dah
Wamefanya mkutano bila kufuata taratibu stahiki
 
Wise man learns from his own mistakes but a wiser man learns from other people's mistakes Kama gambo kujifunza kutokana na makosa ya wengine, akumbuke akina magesa mulongo
 
Mzee wa Visasi na Chuki aka Mrisho Gambo anatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Maana Ilani ya CCM ni Visasi na Chuki,Ika simshangai dini yake inamruhusu.

Ika kuweka ndani Mapadre wetu atalupua hilo.
Kwani padre hawezi kufanya kosa?
 
Salary Slip Ar achunga kumekuwaje siku hizi? Au ndio siasa za upole za Edo hizo? Mbona zamani ujinga kama huu taifa zima lingekuwa kwenye taharuki?
Acha sie tuu, hata hapo Kenya kiongozi wa upinzani hafanyiwi uhuni namna hiyo na vijana wakanywea namna hiyo!
Hata kidogo kuna jambo, sii pendi ccm ila naanza kuchukia jinsi Chadema nayo inavyo anza kuwa mdebwedo
Ndio maana niliwahi leta mada nikashauri CHADEMA iongozwe na watu aina ya Tundu Lissu au Lema ila nakumbuka sikueleweka na nilishambuliwa na baadhi ya watu humu ambao ni pro-CHADEMA.
 
Mmekula rambirambi mmeona haitoshi mmewakamata na watoa rambirambi na kuzuia dhamana zao ni haki yao kisheria.
Mna laana nyie
Haki yao kisheria lkn mkuu wa polisi anaruhusiwa kukaa na mtuhumiwa mpk mwezi mmoja akiona inafaa.
 
Visasi vinavyo pelekea kuuwawa kwa Watu vilianzishwa na mambo yanayo nyima /yanayo vunja 'Haki' za wengine ,wanaofanyiwa haya yasioendana na utaratibu/kanuni na Sheria ni Watu wenye mioyo wenye hisia wenye kuumia na mbali ya hayo wapo wasio pendezwa na yanayo endelea dhidi ya wapendwa wao...

Binadamu anapokosa mmbadala wa wapi apumulie atakata tamaa , na alie kata tamaa ni zaidi ya silaha ya moto.

Tuendelee kwa sababu Wakubwa ndio mmeamua.
 
Wameanza kuligusa KANISA KATOLIKI subiri wauone moto wake
 
Wamefanya mkutano bila kufuata taratibu stahiki
Wamefanya mkutano? Hii ndio kwanza naisikia kutoka kwako mkuu..anyway kwa nini wasipelekwe mahakamani basi..kwani sheria inasemaje juu ya mtuhumiwa kukaa mahabusu zaidi ya saa 24? Tusaidiane katika hilo mkuu!
 
Mnafurahia leo mnaahindwa kuelewa kuna kesho pia.Hata Adam Malima alikuwa kama wewe juzi akalala Mahabusu.

Yona na Mramba walikuwa kama wewe wakalala Keko.

Chenye mwanzo kina mwisho,hata Yesu pamoja na kwamba alikuwa Mwana wa Mungu bado aliishi miaka 33 tu.

Kesho yako hujui,tathmin maneno yako.Chuki,visasi na Ubaguzi havikuongezei hata urefu wa kucha yako.

Chuki,visasi na Ubaguzi haujengi Taifa Bali hulibomoa Taifa vipande vipande.

Nenda kamsikilize JKN alivyoasa kuhusu Chuki,visasi na Ubaguzi. Labda utamuelewa.

Kikubwa CCM ilikuwa n JKN iliyobaki ni Chama Cha Mauaji.
Wafungwa wote magerezani wamefungwa sab ya chuki au uhalifu wao?
 
Aibu hii hata haiwapendezi wana ccm, ilawale wenye kukosa utu kama Gambo na baba ake, yaani ingekuwa ni familia yake imepata msiba angeweka masharti ya kutoa rambirambi?
 
Mayor alikuwa anasimuliwa habari za mahabusu na lema sasa atayaona mwenyewe....
Lema naye alisema natoka Next Week alikata miezi mahabusu haya tumekusikia lema
Nyie endeleeni kufurahia na kuchochea unyanyasaji,

Jiulizeni kwanini wanaodunguliwa Kibiti ni viongozi wa CCM na polisi tu, mnafikiri yanayotokea Kibiti yanasababishwa na nini kama sio chuki, dhuluma, maonevu mnayoshangilia leo,

hivi watu wakianza kufurahia wanaCCM wanavyouawa Kibiti mtafurahi??????.

Wapambe wa CCM taifa mnalisambaratisha kwa kushabikia ulevi wa madaraka wa baadhi ya viongozi wajinga kwa hawa.
 
Aibu hii hata haiwapendezi wana ccm, ilawale wenye kukosa utu kama Gambo na baba ake, yaani ingekuwa ni familia yake imepata msiba angeweka masharti ya kutoa rambirambi?
Wenye busara wengi ndani ya ccm hawapendezwi na mambo haya!Hawawezi kusema kwani mambo yanayomfurahisha mkulu
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom