Lema: Kikombe kikijaa lazima maji yamwagike

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,836
Nimesikia clips yenye sauti inayofanana na Godbless Lema.Akisisitiza dikteta uchwara na kusema kama rais alisisitiza polisi wanyanganye bunduki harakaharaka vipi raia mwema akiingia benki na slaha yake"Na ikaonekana bahati mbaya"Polisi anayelinda Si ataichukua harakaharaka kwa kumua?

Ameendelea kusisitiza hii nchi si ya mtu mmoja ni ya watanzania,Amesema kikombe kikijaa maji yatamwagika.Maana Tanzania hawana jeshi imara kama ilivyokuwa Libya au Misri lakini viongozi wao walidondoshwa.

Nimeshindwa kuiweka clips yenyewe ila kwa speed inayo sambaa itakuwa hapa JF muda si mrefu.Namwona lema naye akienda kuhojiwa polisi kesho.Kazi ipo.

Unaingia benk na Sime kwa sababu zipi hasa??hata masai wanaacha sime nyumbani au kwenye gari wanapoingia benki....Tuwapeleke frontline mkatusaidie kutambua wabeba silaha wasio na madhara

Tuache siasa hadi 2020...hizi ndizo siasa inazotakiwa tuziache.
 
Huyu Mbunge wetu ni Bingwa wa kununua kesi. Arusha tunajuta kumchagua kwakweli ila sio mbaya 2020 sio mbali sana. Wana Arusha tutafanya kama walivyofanya wana Ilemela na Nyamagana.
 
Mnamlisha Lema maneno. Katika harakati za Lema hata kama si mtu ninayempenda sana hajawahi kutukana zaidi ya kuhamasisha watu watafute haki.

Hata majuzi ameandika mwenyewe humu "siungi matusi kwa Rais".

Na ndo siasa. Haki huwezi tafuta kwa kukejeli harafu ukaona watu watakuunga tu. Una nini cha maana sana?

Tujifunze siasa.
 
Huyu Mbunge wetu ni Bingwa wa kununua kesi. Arusha tunajuta kumchagua kwakweli ila sio mbaya 2020 sio mbali sana. Wana Arusha tutafanya kama walivyofanya wana Ilemela na Nyamagana.
Unaumwa ugonjwa gani? Si mlisema 2015 harudi bungeni kwa sababu amegeuza Arusha mji wa vurugu? Mkaambulia kiti kimoja cha diwani mji mzima! Mnamjua Lema mnamsikia?
 
Mnamlisha Lema maneno. Katika harakati za Lema hata kama si mtu ninayempenda sana hajawahi kutukana zaidi ya kuhamasisha watu watafute haki.

Hata majuzi ameandika mwenyewe humu "siungi matusi kwa Rais".

Na ndo siasa. Haki huwezi tafuta kwa kukejeli harafu ukaona watu watakuunga tu. Una nini cha maana sana?

Tujifunze siasa.
Unaweza kutwambia nani ambaye hutukana na tusi lipi alitumia dhidi ya nani?? Ukishindwa basi nawe in mfuasi wa mropokaji dikteta uchwara
 
Nimesikia clips yenye sauti inayofanana na Godbless Lema.Akisisitiza dikteta uchwara na kusema kama rais alisisitiza polisi wanyanganye bunduki harakaharaka vipi raia mwema akiingia benki na slaha yake polisi anayelinda akaiona?Si ataichukua harakaharaka kwa kumua?

Ameendelea kusisitiza hii nchi si ya mtu mmoja ni ya watanzania,Amesema kikombe kikijaa maji yatamwagika.Maana Tanzania hawana jeshi imara kama ilivyokuwa Libya au Misri lakini viongozi wao walidondoshwa.

Nimeshindwa kuiweka clips yenyewe ila kwa speed inayo sambaa itakuwa hapa JF muda si mrefu.Namwona lema naye akienda kuhojiwa polisi kesho.Kazi ipo.
Acha kumlisha maneno Lema ni kijana safi hawezi kumtukana Rais! Hivi unaingia bank na bunduki kufanya nini?
 
Mnamlisha Lema maneno. Katika harakati za Lema hata kama si mtu ninayempenda sana hajawahi kutukana zaidi ya kuhamasisha watu watafute haki.

Hata majuzi ameandika mwenyewe humu "siungi matusi kwa Rais".

Na ndo siasa. Haki huwezi tafuta kwa kukejeli harafu ukaona watu watakuunga tu. Una nini cha maana sana?

Tujifunze siasa.

Kwa hiyo "uki kejiliwa" tu utamaindi sana siyo na kuanzisha "vagi" kwa sbb ya "kejeli" toka kwa "mkejeli?"

Hujui kuwa wewe unaye maindi ndiye utakuwa na shida ktk judgement yako kuliko aliye kukejeli?

Kama wewe ni muumini wa dini ya kikristo i.e mkristo nishushauri uende ukasome kitabu kitakatifu cha Biblia (New Testament) kuhusu kiongozi shujaa na mfalme wa wafalme Yesu Kristo kuanzia kitabu cha Mathayo Mtakatifu hadi Ufunuo, utajifunza mengi sana juu ya kuzishinda kejeli.

Hakuna kiongozi yeyote mkubwa aliyewahi kuishi ktk dunia hii na kupokea kejeli za hali ya juu kama YESU KRISTO na kamwe hakuwahi kugombana wala kulipiza kisasi dhidi wakejeli wake ambao walifikia hatua mpaka ya kumtemea mate na yeye kamwe hakuwahi hujali zaidi ya kusema "baba wasamehe kwa kuwa hawajui walitendalo!"

Hawakuona hilo linatosha kwani huyu ndugu pamoja na kukejeliwa saaana, hakuwahi kuanzisha vurugu japo alikuwa na nguvu na mamlaka ya kuwaangamiza wote kufumba na kufumbua tu!!

Mwisho waliona huyu mtu dawa yake ni kumuua tu tena kwa kifo cha fadhaa na kutisha. Yet he went on loving all na leo hii bila yeye mimi na wewe si kitu!!

Ukimuona mtu "ana maindi" hata kejeli za mwendawazimu wakati yeye anajijua ni "timamu" jiulize mara mbili mbili kuhusu utimamu wake na pengine tambua mara moja kuwa yeye ndiye hasa mwendawazimu!!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom