Lema: Ikulu imenivua ubunge ; Ikulu yamjibu vikali

Lengo lao kuu la kwanza litakuwa limegonga mwamba,ikiwa mh lema hatakata rufaa,vinginevyo walitegemea kuwa lema angekurupuka na kukata rufaa,na hakika ccm wangeshangilia kwani wangetumia mkono wao ndani ya mahakama kuivuta kesi hii hadi baada ya uchaguzi mkuu,kisha wangurudi kujinadi kwa wananchi kuwa chadema haikufanya lolote la maendeleo jimboni humu!!tumeshtuka! Tunachotaka kwa sasa ni mabadiliko kwanza mengine baadaye.
 
Siku zote tunakumbushana kuhusu source! inawezekana Director akawa ana kitu kizuri cha kutujuza lakini namna anavyowasilisha haeleweki!
 
Nimeiskia hiyo taarifa,kweli ikulu imegeuka sehemu ya mipasho na uswahili,ikulu imekaliwa na mswahili pure!inaonyesha Lema walikua wanamchukia sana,ila m****e asipokua makini atatoka ikilu kwa aibu na kwa bakora,hii nchi watu wamechoka,wana hasira na ugumu wa maisha na mbaya zaidi wamejikatia tamaha kutokana na ugumu wa maisha,ni kama wanasubiri tu wapi au nani aanzishe wengine watu waingie!kwa jinsi ikulu ilivyojibu kauli ya Lema,imenipa ushawishi kabisa kua hii kesi ilikua coocked na mbaya zaidi,waliyoipika walikua na uwezo mdogo sana kichwani!
 
Unatuondolea mbunge wetu halafu unawaelekeza waseme nini kwetu!! kwamba dowans si yako! ha ha ha! hasira unazoendelea kuzijaza miyoni mwa watu! si muda mrefu tutageuka wapelestina! si juzi ulikuwa Mount meru wewe! sawa we shall see!
 
Dikteta asiyejiamini ha ha ha ha! wa kina Idd Dada walikuwa wanauwa tuu! wewe waenda kama warudi nyuma! ha ha ha!
 
Hata kama Ikulu ingetaka kujibu tuhuma za Lema, haina watu wenye uwezo wa kuandika vizuri kulingana na hadhi ya ofisi ya Rais? Hiyo habari kama vile imeandikwa mtaani. Hivi hakuna wahakiki wa habari za ofisi zetu nyeti?
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


clip_image002.png

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yake ya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumu ya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.
Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala Ikulu imeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu ama kuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.
Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumu ama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.
Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa Mahakama ambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katika maamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazima atambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.
Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba Bwana Lema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni la kisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.
Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wa kumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hana mtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012
Siamini kama hii barua ni ya Ikulu mbona imeandikwa kimipasho sana? wapi heshima ya Ikulu.
 
JK amefanya hivyo akitegemea CDM atakata rufaa bahati mbaya kwake CDM ni makini zaidi ya serikali yake;
pili alipenda kutumia trick hii ili kuwafanya wahandishi wa habari na wananchi kuconcetrate kwenye issue Lema Arusha na sio kushindwa kwa uchaguzi wao wa Arumeru.
ndugu wapenda haki naomba kuwashauri kukingana na lengo la JK kama walivyofanya CDM kwa kutokata rufaa na sisi tuendelee kuongelea kushindwa kwao Arumeru
 
Ok clip za lusinde na maneno yake zipo hapa embu naomba nipewe evidence ya Lema kuituhumu ikulu,maana ciwezi comment pasipo kuisikia,ila kwa kweli chadema we need to calm down,lets not give ccm any chance to play in their favour
 
Imekuaje jk kupitia salva kujibu tuhuma za kupanga hukumu ya lema haraka haraka?suala la madai ya madaktari alikaa kimya
 
Ni za kweli ndo maana wamekurupuka kujibu

mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala aliamriwa na Ikulu kumtangaza Dr.Mahanga mshindi wa Jimbo la Segerea

ni hii hii Ikulu inayosababisha kesi hiyo kupigwa danadana baada ya N/Waziri Dr.Mahanga kuelemewa
 
hii nchi inakera sana kama mahakama itatumia kisiasa tutakuwa hatuna pa kwenda zaidi ya kutumia njia moja tu "people's power. Mh Lema ucjali ingia tena kwa wananchi na watakurudisha bungeni.
 
Baada ya mahakama kutoa hukumu, Lema ametoa maoni akishutumu ikulu kushinikiza Mrema avuliwe Ubunge. Masaa machache sana baadaye ikulu ikatoa tamko/taarifa kwa vyombo vya habari.
Kuna matukio mengi sana yaliyoliweka taifa katika hali tete na hayakuwa kujibiwa ndani ya muda mfupi kiasi hicho!! mfano wa matukio ya aina hiyo ni:-
1. Ushiriki wa JK kwenye kashfa ya richmond
2. Ushiriki wa JK kwenye kifungo cha Babu Seya
3. Usiriki wa JK kwenye Wizi wa Twiga kwenda Uarabuni
4.
5.
.
.
.
Orodha ni ndefu!! na hoja zote hizo ama hazijawahi kujibiwa na Ikulu katika muda mfupi kiasi hicho au kutolewa ufafanuzi.
Kutokana na mizani hiyo,
Je, Tuamini kuwa Lema kasema kweli au hoja ya Lema ni hatari kwa usalama wa nchi hii?
TOA MAONI YAKO!
 
Back
Top Bottom