Lema: Ikulu imenivua ubunge ; Ikulu yamjibu vikali

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Hukumu ya leo imeibua mambo mazito ambapo Lema amesema kuwa anajua amevuliwa ubunge kwa shinikizo kutoka Ikulu hasa baada ya kuwa amekataa ombi la mmoja wa viongozi wakuu wa serikali wakati huo la kutaka agombee nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi kwa ahadi ya kumpa cheo kikubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada kutolewa kwa hukumu hiyo, Lema mwaka 2007 aliitwa na kiongozi huyo ili akubali ombi hilo na alimpa watu watakaomsaidia kwenye kampeni zake lakini hakukubaliana naye.
Alisema kuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 aliitwa tena na kuombwa amuunge mkono mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, ambapo wangemtafutia Lema nafasi ndani serikali, lakini alikataa tena hatua ambayo anaamini ilisababisha chuki.

Aliongeza kuwa sababu nyingine iliyoongeza chuki dhidi yake na serikali, ni hatua yake ya kukataa kushiriki katika mapokezi ya viongozi wa kitaifa waliotembelea Arusha akiwemo Rais Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, na kubwa zaidi kutomtambua meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo.
Katika kuthibitisha madai yake hayo, Lema alisema kuwa alianza kupata taarifa za kushindwa kwake katika kesi hiyo kutoka kwa watu mbalimbali kabla ya hukumu ya jana.

Aliwataja waliowahi kumjulisha kushindwa kwake kuwa ni pamoja na baadhi ya wabunge wa CCM, maafisa usalama wa taifa na marafiki zake muhimu walioko serikalini.
Aliwataja waliomtaarifu kuanguka kwake kuwa ni pamoja na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Mweka Hazina wa chama hicho tawala Mwigulu Mchemba na ofisa usalama mmoja wa ngazi ya juu (jina linahifadhiwa).Alisema kuwa hata walipokuwa kwenye harakati za kampeni jimbo la Arumeru Mashariki Mwigulu Nchemba alisikika akimwambia kijana mmoja aliyeshiriki kura za maoni ndani ya CCM kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kuwa ajiandae kwa uchaguzi wa Arusha Mjini kwani mahakama itatengua ubunge wake (Lema).“Nilipokuwa najiandaa asubuhi kwenda mahakamani nilipigiwa simu na mbunge wa Kawe Halima (Mdee) ambaye aliniambia amepata taarifa kuwa navuliwa ubunge na katibu wetu mkuu (Dk. Willbrod Slaa) alinipigia kunieleza hivyo hivyo na walinitaka nijipe moyo,” alisema Lema.

Lema alisema hata alipopita kwenye ofisi yake ya ubunge iliyoko jengo la mkuu wa wilaya alikuta magari ya polisi karibu 10 yaliyokuwa na polisi wengi wenye silaha.
Alisema ulinzi mkali na kuzuiwa kwa watu mahakamani kwa kuweka mkanda wa njano kuzunguka majengo ya mahakama, kulithibitisha kuwa tayari watendaji wa serikali na vyombo vya dola walijua kitakachoamriwa.“Kitu walichofanya leo ni cha kusikitisha, maana haiwezekani kesi iliyosikilizwa kwa miezi karibu mitatu jaji akatoa hukumu kwa muda mfupi kiasi kile.

Wao wana dola sisi tuna Mungu,” alisema.
Mbunge huyo aliwaambia mamia ya watu waliomsindikiza kwa maandamano kutoka mahakamani hadi zilipo ofisi za CHADEMA mkoa kuwa hukumu hiyo imeendeleza ari yake ya kupigania haki kwa vile ubunge kwake ulikuwa ni utumishi na si vinginevyo hivyo kwa sasa ataendeleza harakati za kudai haki mpaka kieleweke.“Safari ya ukombozi ilianza zamani wengine walikufa wengine walipoteza viungo vyao lakini safari inaendelea, msiogope ninyi mlio wengi, maana mkiogopa mimi nitaogopa zaidi lakini nawatia moyo msiogope kuweni jasiri haki haiwezi kudhalilishwa,” alisema Lema.“Tafsiri niliyoipata mahakamani ni kuwa wametengua matokeo yangu ya ubunge; mtu leo asiumizwe yeyote unayekutana naye leo ni kura yetu, kila mtu ameumia kwa sababu mlipiga kura mkachunga na tukashinda, wao wana jaji wa mahakamani sisi tuna jaji wa mbinguni.”

soma zaidi tanzania daima

JE SHERIA YA UCHAGUZI INASEMAJE?
Hapa chini ni baadhi ya vifungu kutoka sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985

108 (3) The election of a candidate as a member shall be declared void on
any of the following grounds which are proved to the satisfaction of the
court, namely-
(a) that by reason of corrupt or illegal practices committed in circumstances whether similar to those before enumerated or not the majority of voters were, or may have been, prevented from election the candidate whom they preferred;
(b) that, during the election campaign, statements were made by the
candidate, or on his behalf and with his knowledge and consent
or approval with intent to exploit tribal, racial or religious issues
or differences pertinent to the election or relating to any of the
candidates or, where the candidates are not of the same sex, with
intent to exploit such difference
c) non-compliance with the provisions of this Act relating to election,
if it appears that the election was not conducted in accordance
with the principles laid down in such provisions and that such
non-compliance affected the result of the election;
(d) that a corrupt or illegal practice was committed in connection with
the election by or with the knowledge and consent or approval of
the candidate or by or with the knowledge and consent or approval
of any of his agents; or
(e) that the candidate was at the time of his election a person not
qualified for election as a member.

***********Maamuzi ya kumvua ubunge Lema yamejikita zaidi katika kipengere 3 (a) baada ya mashitaka mengine yaliyohusiana na kipengere (b) kutupiliwa mbali***************




ADHABU YA ZIADA KWA KOSA LA "CORRUPTION AND ILLEGAL PRACTICES" KWA LEMA

Kulingana na kifungu cha 96 (1) na (2) jina lake litaondolewa katika orodha ya wapiga kura (kifungu hiki kitamzuia Lema kujiandisha na kupiga kura ila kugombea ubunge ruksa):

(a) miaka 10 kama amepatikana na rushwa
(b) miaka 5 kama amepatikana na "illegal practices"


Majibu ya Serikali:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yakeya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumuya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.

Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala Ikuluimeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu amakuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.

Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumuama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.

Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa Mahakamaambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katikamaamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazimaatambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.

Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba BwanaLema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni lakisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.

Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wakumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hanamtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012



 
wakuu ikulu imetoa taarifa kwa uma haipo kwenye hukumu ya lema kama baadhi ya watu wanavyodai ni shinikizo la kikwete'wamemalizia kwa kusema Lema hana adabu'nimeshindwa kuelewa maana ya hiyo taarifa
 
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imekanusha kauli ya Mh. Lema kuwa inahusika maamuzi ya kumvua Ubunge. Imemshauri akate rufaa Kama ajaridhika na hukumu. Source clouds fm
 
wakuu ikulu imetoa taarifa kwa uma haipo kwenye hukumu ya lema kama baadhi ya watu wanavyodai ni shinikizo la kikwete'wamemalizia kwa kusema Lema hana adabu'nimeshindwa kuelewa maana ya hiyo taarifa

hiyo taarifa imetolewa kwa maandishi au msemaji wa ikulu
 
wakuu ikulu imetoa taarifa kwa uma haipo kwenye hukumu ya lema kama baadhi ya watu wanavyodai ni shinikizo la kikwete'wamemalizia kwa kusema Lema hana adabu'nimeshindwa kuelewa maana ya hiyo taarifa

Yaani sentensi ndefu huvi sijawahi ona maana haina nukta wala koma! Unakimbilia wapi director? Tulia ulete habari inayoeleweka!
 
kama ikulu yupo *,tutegemee nini,mtaweweseka sana mwaka huu,this country is rotten at heart
 
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imekanusha kauli ya Mh. Lema kuwa inahusika maamuzi ya kumvua Ubunge. Imemshauri akate rufaa Kama ajaridhika na hukumu. Source clouds fm

Waambie hakuna kupeleka Kesi ya Nyani kwa Ngedere. Biashara hiyo tumefanya miaka 50 iliyopita hatutaki kuendelea nayo...

Mwambieni JK nani alisema hivyo... Mbona sijasikia CDM au Mbowe aua Lema akisema hivyo..

Au ndicho kilochofanyika sasa mnahofu watu watajua?...
 
kurugenzi ya mawasiliano ikulu imekanusha kauli ya mh. Lema kuwa inahusika maamuzi ya kumvua ubunge. Imemshauri akate rufaa kama ajaridhika na hukumu. Source clouds fm

Sijawahi ona presidential press service ya kipuuzi kama ya tanzania inayoongozwa na Salva Rweyemamu wanashindwa hata kujifunza kwa wenzetu wa Kenya!real sijapata waelewa hawa jamaa wanatumia kodi zetu bure very incompetent department at the state house.kuna mengi mazito ambayo walipaswa kutoa respose hata hili la Mheshimiwa Lema lilihitaji response ya haraka kiasi hichi shame upon you Id**ts of magogoni!
 
Back
Top Bottom