Lema: Bonde la uvuli wa mauti - Mkakati umepangwa nikamatwe na Jeshi la Polisi leo, maelekezo yameshatolewa

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,204
Nimepata taarifa kwamba ninatafutwa na Jeshi la Polisi Arusha kwa maelekezo kutoka juu.

Ninaelezwa kuwa mipango mingi inapangwa juu ya uchaguzi wa marudio hapa Arusha , tunatarajia kuwa na wakati mgumu sana ktk kampeni hizi, na hivi sasa tunaanza kushuudia mateso ya aina mbali mbali.

Watesi wetu wanapata sifa na vyeo kwa namna ya ukatili wanaonyesha dhidi yetu , kila wakati tulipolalamika dhidi ya matendo mabaya na nia ovu , tulifikiri tunafanya jambo jema na muhimu , lakini badala yake uovu wao umekuwa msaada ktk kazi zao . Wengine wamepanda vyeo kwa sababu ya ukatili , kukandamiza haki na demokrasia , tunarudi kwenye uchaguzi leo kwa sababu pia ya rushwa , hata walitoa rushwa hadharani walipandishwa cheo badala ya kukutana na mkono wa sheria.

Ni dhahiri sasa Dc anayetaka kuwa RC ni lazima awe na tabia na matendo ya aina hii , hali kadhalika kwa nafasi nyingine mbali mbali. Hili ni tishio kubwa la usalama wa Nchi yetu.

Hakuna majadiliano ya kikazi kati ya Viongozi wa upinzani na Serikali , kwani hali yoyote yakuonyesha mahusiano mema kati yetu na Viongozi wa Serikali ni risk kwa kazi zao. Kwa hiyo namna pekee ya wao kuonyesha nidhamu na utendaji uliotukuka kwa Mamlaka zao za uteuzi ni kuonyesha na kutenda mahusiano na matendo mabaya dhidi yetu.

Ubaguzi huu unakua kwa kasi sana , hii ni saratani , wako wengi wanaotuonea huruma na wachache hawataelewa msingi huu wa malalamiko yetu , wanafikiri msalaba huu unatustahili sisi peke yetu kumbe ni msalaba wetu sote kama Taifa.

Wachache hao walioko mahabusu kifikra wanahitaji msamaha wetu .
Martin Luthet Jr alipata kusema " Injustice anywhere is threat to justice everywhere " akaendelea kusema " Whatever affects one directly , affects all indirectly .

Tusikate tamaa , baada ya giza nene asubuhi utokea .

Godbless J Lema (MB)
 
Ni Kweli kamanda wamegundua ukitaka kupanda cheo haraka nyanyasa wapinzani, huu ni utawala uliolaaniwa mbele ya Mungu
hizi kauli zimeanzwa kusemwa toka enzi za kina mrema wakiwa wapinzani wakuu katika nchi hii mpaka leo bado story ni zilezile tuu,ni wakati wa kureact bahati mbaya waliokuwa mstari wa mbele kureact leo ndo wanaitwa wasaliti...

Kalaghabao endeleeni kulalamika tuu,CCM haitatoki madarakani kwa kulalamika kwenu itatoka kwa nguvu. Na wenye nguvu ndio wataiteka na kuitawala hii nchi.
 
Ipo siku wananchi wengi wataichoka ccm na hapo ndipo itatolewa kwa nguvu
 
Staying silent in times of oppression, puts you in the side of the oppressers.
Long walk to freedom.

Tell my people that I love them, and they must continue the struggle, my blood shall nourish the tree that will bear the fruits of freedom.
Aluta continua

Solomon Mahlangu
 
Ipo siku wananchi wengi wataichoka ccm na hapo ndipo itatolewa kwa nguvu
hiyo siku haifiki kwa style yenu ya nyinyi kwa nyinyi kutoaminiana, upinzani huu umekosa nguvu haijawahi tokea tangu kuanza kwa vyama vya upinzani hii yote ni kuingiliwa na kukosa kuaminiana wenyewe kwa wenyewe.

leo replacement ya Dr.Slaa ni Dr.Mashinji are you serious???na mnaexpect kiongozi kama huyu ndo aitoe ccm kwa nguvu?? Nani aliyewaloga??utawala huu ni wa kutumia nguvu sio wa watu waliopooza kama viongozi wenu hawa wasasa.
 
Nimepata taarifa kwamba ninatafutwa na Jeshi la Polisi Arusha kwa maelekezo kutoka juu.

Ninaelezwa kuwa mipango mingi inapangwa juu ya uchaguzi wa marudio hapa Arusha , tunatarajia kuwa na wakati mgumu sana ktk kampeni hizi, na hivi sasa tunaanza kushuudia mateso ya aina mbali mbali.

Watesi wetu wanapata sifa na vyeo kwa namna ya ukatili wanaonyesha dhidi yetu , kila wakati tulipolalamika dhidi ya matendo mabaya na nia ovu , tulifikiri tunafanya jambo jema na muhimu , lakini badala yake uovu wao umekuwa msaada ktk kazi zao . Wengine wamepanda vyeo kwa sababu ya ukatili , kukandamiza haki na demokrasia , tunarudi kwenye uchaguzi leo kwa sababu pia ya rushwa , hata walitoa rushwa hadharani walipandishwa cheo badala ya kukutana na mkono wa sheria.

Ni dhahiri sasa Dc anayetaka kuwa RC ni lazima awe na tabia na matendo ya aina hii , hali kadhalika kwa nafasi nyingine mbali mbali. Hili ni tishio kubwa la usalama wa Nchi yetu.

Hakuna majadiliano ya kikazi kati ya Viongozi wa upinzani na Serikali , kwani hali yoyote yakuonyesha mahusiano mema kati yetu na Viongozi wa Serikali ni risk kwa kazi zao. Kwa hiyo namna pekee ya wao kuonyesha nidhamu na utendaji uliotukuka kwa Mamlaka zao za uteuzi ni kuonyesha na kutenda mahusiano na matendo mabaya dhidi yetu.

Ubaguzi huu unakua kwa kasi sana , hii ni saratani , wako wengi wanaotuonea huruma na wachache hawataelewa msingi huu wa malalamiko yetu , wanafikiri msalaba huu unatustahili sisi peke yetu kumbe ni msalaba wetu sote kama Taifa.

Wachache hao walioko mahabusu kifikra wanahitaji msamaha wetu .
Martin Luthet Jr alipata kusema " Injustice anywhere is threat to justice everywhere " akaendelea kusema " Whatever affects one directly , affects all indirectly .

Tusikate tamaa , baada ya giza nene asubuhi utokea .

Godbless J Lema (MB)
..mbona sijaona Bonde la Mauti hapo? ,..naona bonde la kuomba huruma tu hapo,..
 
92 Reactions
Reply
Back
Top Bottom