Lema: Bonde la uvuli wa mauti - Mkakati umepangwa nikamatwe na Jeshi la Polisi leo, maelekezo yameshatolewa

Ningelikuwa ni mimi wewe Lema ningelienda mwenyewe kule kule kwao. Kwa sababu, waweza kukujia ghafla na kuanza kurusha vya moto kuwa ulikuwa unajibizana nao. The dead stay dumb yu know.
 
Polisi wanakula kwa kutumwa, kulinda
Mwalimu anakula kwa kilufundisha
Dactor anakula kwa kutibu

MWANASIASA wanakula kwa kutudanganya, kutukanana

[HASHTAG]#kama[/HASHTAG] anahofia bora aache siasa alafu akatumie chet cha form4 kupata ajira mpy
Hapana, polisi wanakula kwa kutumwa kutukamata.
 
Upinzani Tz ulishapoteza dira 2015 baada ya kumsaliti Dr. Slaa, tuliwaeleza mkatuita Lumumba buku 7. Kwasasa wengine tunawaamgalia tu na kuwapuuza, asilimia kubwa wanaolalama mitandaoni ni wapiga domo na maslahi binafsi tu. Kwa sasa TZ hakuna upinzani wenye uwezo wa kuhoji maana wao kwa wao hawaaminiani.
 
..utawala wa kishetani...matendo yao ya kishetani.... Mtu unajiuliza wanapata nini kwa kufanya hivi???....mbegu ya kishetani hii inapandwa toka juu....Na kila wa chini lazima atii na kutekeleza....hii dhambi mbaya sana....lazima ifike mahali watu wadai haki zao pale wanapozikosa....msiogopwe kukamatwa...hamwezi kufungwa kwa kudai haki zenu....
 
Kaandae press release KTN kulalamika haya. Mbona Hemed yupo KTN mda huu. Mlimchezea sana JK.Hiki chuma kinawabatiza kwa moto.
 
Nimepata taarifa kwamba ninatafutwa na Jeshi la Polisi Arusha kwa maelekezo kutoka juu.

Ninaelezwa kuwa mipango mingi inapangwa juu ya uchaguzi wa marudio hapa Arusha , tunatarajia kuwa na wakati mgumu sana ktk kampeni hizi, na hivi sasa tunaanza kushuudia mateso ya aina mbali mbali.

Watesi wetu wanapata sifa na vyeo kwa namna ya ukatili wanaonyesha dhidi yetu , kila wakati tulipolalamika dhidi ya matendo mabaya na nia ovu , tulifikiri tunafanya jambo jema na muhimu , lakini badala yake uovu wao umekuwa msaada ktk kazi zao . Wengine wamepanda vyeo kwa sababu ya ukatili , kukandamiza haki na demokrasia , tunarudi kwenye uchaguzi leo kwa sababu pia ya rushwa , hata walitoa rushwa hadharani walipandishwa cheo badala ya kukutana na mkono wa sheria.

Ni dhahiri sasa Dc anayetaka kuwa RC ni lazima awe na tabia na matendo ya aina hii , hali kadhalika kwa nafasi nyingine mbali mbali. Hili ni tishio kubwa la usalama wa Nchi yetu.

Hakuna majadiliano ya kikazi kati ya Viongozi wa upinzani na Serikali , kwani hali yoyote yakuonyesha mahusiano mema kati yetu na Viongozi wa Serikali ni risk kwa kazi zao. Kwa hiyo namna pekee ya wao kuonyesha nidhamu na utendaji uliotukuka kwa Mamlaka zao za uteuzi ni kuonyesha na kutenda mahusiano na matendo mabaya dhidi yetu.

Ubaguzi huu unakua kwa kasi sana , hii ni saratani , wako wengi wanaotuonea huruma na wachache hawataelewa msingi huu wa malalamiko yetu , wanafikiri msalaba huu unatustahili sisi peke yetu kumbe ni msalaba wetu sote kama Taifa.

Wachache hao walioko mahabusu kifikra wanahitaji msamaha wetu .
Martin Luthet Jr alipata kusema " Injustice anywhere is threat to justice everywhere " akaendelea kusema " Whatever affects one directly , affects all indirectly .

Tusikate tamaa , baada ya giza nene asubuhi utokea .

Godbless J Lema (MB)
CDM imeshakufa baada ya kumkaribisha uliyeapia kwa Mungu kuwa ni sifa kwa Mungu kumzomea Lowassa na kwa sasa ni kiongozi wako hapo CDM. Ulimzihaki Mungu itakucost sana Mh. MB!! Hata kuota huoti tena siku hizi.
 
Ni heshima kubwa kwa Mungu kumzomea fisadi lowassa. Mwisho kunukuu.
Lema nipe mrejesho wa hii quote yako mujarabuu kabisa. Na log out mheshimiwa
 
Back
Top Bottom