Lema: Bonde la uvuli wa mauti - Mkakati umepangwa nikamatwe na Jeshi la Polisi leo, maelekezo yameshatolewa

Nimepata taarifa kwamba ninatafutwa na Jeshi la Polisi Arusha kwa maelekezo kutoka juu.
Tusikate tamaa , baada ya giza nene asubuhi utokea .

Godbless J Lema (MB)
Poleni sana Chadema kwa yote, japo suing mkono any persecutions you suffer, pia sifurahishwi na zile persecutions mnazowafanyia, wale msiokubaliana nao ndani ya nyumba yenu, ila msijali kwa sababu hapa duniani ni mapito tuu, wote tuko safarini, hivyo ukiwaondoa wale tuu watakaookolewa kwa neema, wengine wote na kila mmoja wetu, atahukumiwa kwa matendo yake, kupitia kitu kinachoitwa karma, and its for real!, hao wote wayatendao maovu, wote watalipwa malipo sawia kwa uovu wao, ila nanyi pia, msikute hayo ni sehemu tuu ya malipo yenu!.

Poleni!.

Paskali
Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!" | Page 6 ...
Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau ...
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...
 
Wee mura kila siku unakimbizana na polisi/uvccm maendeleo utaleta lini?? wakati sio rafiki tena,ingekua vema muda unaotumia kukijenga chama ukautumia kutengeneza fursa za maendeleo mfn ile project y kituo cha afya n.k
 
Mpaka habari imekufikia muhusika kuna dalili kubwa ya kulichokoza jeshi la polisi ili maneno yako yatimie!
 
Kamanda Lema, nakupongeza sana tena sana. Ujasiri wako , uwezo wako wa kuamsha na kuhamasisha wanaArusha ndiyo chanzo cha mkoa huo kuwa chini ya chadema. CCM wanalijua hilo na ndiyo maana wanakuogopa mno.

Mwito wangu kwako kamanda shikilia hapo hapo. Ipo siku ccm wataomba poo na siku hiyo haiko mbali.

Ni mimi Sexless, Bongo bahati mbaya.
 
hizi kauli zimeanzwa kusemwa toka enzi za kina mrema wakiwa wapinzani wakuu katika nchi hii mpaka leo bado story ni zilezile tuu,ni wakati wa kureact bahati mbaya waliokuwa mstari wa mbele kureact leo ndo wanaitwa wasaliti...

Kalaghabao endeleeni kulalamika tuu,CCM haitatoki madarakani kwa kulalamika kwenu itatoka kwa nguvu. Na wenye nguvu ndio wataiteka na kuitawala hii nchi.
Kwa hiyo unashauri tuingie msituni?
 
Nimepata taarifa kwamba ninatafutwa na Jeshi la Polisi Arusha kwa maelekezo kutoka juu.

Ninaelezwa kuwa mipango mingi inapangwa juu ya uchaguzi wa marudio hapa Arusha , tunatarajia kuwa na wakati mgumu sana ktk kampeni hizi, na hivi sasa tunaanza kushuudia mateso ya aina mbali mbali.

Watesi wetu wanapata sifa na vyeo kwa namna ya ukatili wanaonyesha dhidi yetu , kila wakati tulipolalamika dhidi ya matendo mabaya na nia ovu , tulifikiri tunafanya jambo jema na muhimu , lakini badala yake uovu wao umekuwa msaada ktk kazi zao . Wengine wamepanda vyeo kwa sababu ya ukatili , kukandamiza haki na demokrasia , tunarudi kwenye uchaguzi leo kwa sababu pia ya rushwa , hata walitoa rushwa hadharani walipandishwa cheo badala ya kukutana na mkono wa sheria.

Ni dhahiri sasa Dc anayetaka kuwa RC ni lazima awe na tabia na matendo ya aina hii , hali kadhalika kwa nafasi nyingine mbali mbali. Hili ni tishio kubwa la usalama wa Nchi yetu.

Hakuna majadiliano ya kikazi kati ya Viongozi wa upinzani na Serikali , kwani hali yoyote yakuonyesha mahusiano mema kati yetu na Viongozi wa Serikali ni risk kwa kazi zao. Kwa hiyo namna pekee ya wao kuonyesha nidhamu na utendaji uliotukuka kwa Mamlaka zao za uteuzi ni kuonyesha na kutenda mahusiano na matendo mabaya dhidi yetu.

Ubaguzi huu unakua kwa kasi sana , hii ni saratani , wako wengi wanaotuonea huruma na wachache hawataelewa msingi huu wa malalamiko yetu , wanafikiri msalaba huu unatustahili sisi peke yetu kumbe ni msalaba wetu sote kama Taifa.

Wachache hao walioko mahabusu kifikra wanahitaji msamaha wetu .
Martin Luthet Jr alipata kusema " Injustice anywhere is threat to justice everywhere " akaendelea kusema " Whatever affects one directly , affects all indirectly .

Tusikate tamaa , baada ya giza nene asubuhi utokea .

Godbless J Lema (MB)
Unabii huu utatimia tu na hawatakuwa na pa kutokea
 
Unajua huwa nawashangaa sana viongozi wa upinzani na kulalamika kila siku. Siasa haziwezi kufanana na wakati uongozi wa sasa ni mwingine, na kama mtaendelea kufanya siasa kama mlivyokuwa mnafanya kipindi kilipita, siasa za kulialia basi mtapotea zaidi. Badilisheni siasa zenu hizo za kulialia kwani hizi ni zama zingine hivyo ni lazima mje na siasa za kujipanga zaidi na sio kukurupuka na kulialia kwenye media hiyo haitawasaidia sana sana mtapotea tu na kuacha wenye nguvu za kufanya siasa wafanye siasa.
 
Sio siku za mbali kutachimbika tu kwani kawaida uvumilivu una mwisho.
Hakuna cha kuchimbika wala kuchimbuka. Polisi mkamateni huyo Lema ajieleze vizuri. Hawezi kukurupuka tu na kuanza kulishutumu jeshi la polisi. Haiwezekani na haivumiliki kamwe.
 
Back
Top Bottom