Lema apokea wajumbe wa nyumba kumi 3 (CCM) Kata ya Daraja Mbili waliohamia Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema apokea wajumbe wa nyumba kumi 3 (CCM) Kata ya Daraja Mbili waliohamia Chadema

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Kitu Kizito, Oct 22, 2012.

 1. Kitu Kizito

  Kitu Kizito JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  SAM_5783.JPG Mh Godbles Lema ambae anasubiria "ruling" ya rufaa yake kupinga kuvuliwa ubunge katika maamuzi tata ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha akiwasindikiza kwa macho wakishuka jukwaani kinamama watatu waliokuwa wajumbe wa nyumba kumi CCM katika mitaa ya Jamhuri na Ndarvoi iliyopo Kata ya Daraja Mbili ambapo kamapeni za kuwania udiwani zinaendelea! Tukio hili lilitokea juzi katika mkutano uliofanyika eneo jirani na kiwanda cha bia.
  SAM_5781.JPG Picha hii inamuonesha mgombea wa Chadema katika Kata ya Daraja Mbili, Proper Msofe (kushoto) anaefuatiwa na Kalist Bush (huyu alikuwa Mwenyekiti wa TLP Wilaya ya Arusha kabla ya kujiunga na Chadema) na Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Arusha, Noel Olevaroya mwenye kadi za CCM zilizokabdihdiwa siku hiyo.

  Kina mama hao ambao pia walikabidhi kadi zao za uanachama wa Umoja wa Wananwake mkoani Arusha, ni pamoja na Amida Waziri anaetokea Mtaa wa Jamhuri.

  Wengine ni Lusia Joseph na Rispa Gilbert ambao wote wanatokea Mtaa wa Ndarvoi katika Kata hiyo. Kujitoa kwa wajumbe hao ni pigo sana kwa CCM ambao mara nyingi wamekuwa wakitegemea wajumbe hao kutengeneza matandao wa ushindi kwa njia zilizo halali au haramu!.

  Sambamba na hayo, vijana wawili walioelezwa kutumiwa na CCM kupita maeneo tofauti kumchafua Lema walikamatwa katika kkutano huo na nusura wapate kichapo kitakatifu kutoka kwa watu waliokuwa tayari wana hasira. Ni busara za lema kuamua kuondoka nao na gari yake na kwenda kuwaachambele baaya ya kuwapandisha jukwaani na kutangaza madhambi yao!!

  Tukio lingine la kufurahisha ni ala kijana Stanley Musa aliyerudisha kadi ya TLP ambayo inaonekana ilitolewa tar 13/10/2012 kwa kurudisha kadi ya CCM. Chadema hawakumpa kadi na badala yake akavalishwa tu skafu!! WebRep


  currentVote


  noRating
  noWeight
   
 2. n

  namkweche Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tunasonga mbele na kwa uwezo wa MUNGU tutafika tu. CDM 4ever
   
 3. C

  CNN Senior Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2012
  Messages: 112
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kikwete nae anajianda kuresha kadi.
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naona jamaa anasubiri kesho kuapishwa tu,
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Peoples Power, Arusha stand up!!!!
   
Loading...