Lema amvaa Ridhiwani Kikwete, Ni kuhusu umiliki kampuni ya Tanzanite One

Status
Not open for further replies.

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Hii nime'copy na ku'paste toka kwenye facebook page ya kamanda Lema...........

Naomba hili liwe wazi kwa Watanzania, Ridhiwan Jakaya Kikwete, chini ya kampuni ambayo wanaharakati tutaleta ushahidi wake kwa wananchi wanaotaka ukombozi, wiki hii alikuwepo Jijini Arusha na tayari ana mkataba wa umiliki wa zaidi ya hisa asilimia 45 za kampuni ya Tanzanite One. Hii ni biashara ya Rais wa nchi. Ametumia madaraka yake kwa siri kupisha umiliki huu kupitia mtoto wake.

Linaweza kukanushwa na kupingwa lakini muda unafika ambapo umma wa Watanzania utaamua. Hata wakishinda kesi za mahakamani, hawataushinda uamuzi wa umma.

CCM inakufa, iko hatua za mwisho kabisa.
 
Huyu chalii anakulaga deal zote za kupokea wageni wakubwa wakubwa kwa mikutano Arusha kwa Mgongo wa Angoni. Hata Juzi palikuwa na mkutano kama wiki na zaidi jamaa Mark II Grande GX110 zake ndio zilikuwa mzigoni.

Siku si nyingi atarudisha tu mali zetu.
 
Hii nchi inapaswa wananchi kuamua na si hawa tuliowaweka wakituona sisi wajinga na wapuuzi. Hatima ya tanzania ipo mikononi mwetu. Hawa akina riziwani tunawachekea wenyewe
Utamfanya nini wewe? Utabaki kulalama kama kina Lema tu, kama ushahidi upo basi kwanini msiende mahakamani?
 
Huyu chalii anakulaga deal zote za kupokea wageni wakubwa wakubwa kwa mikutano Arusha kwa Mgongo wa Angoni. Hata Juzi palikuwa na mkutano kama wiki na zaidi jamaa Mark II Grande GX110 zake ndio zilikuwa mzigoni.

Siku si nyingi atarudisha tu mali zetu.
Hadhith za kwenye mbege hizi
 
Haka katoto mbona ni mali yetu siku nyingi. Kila mtanzania ana hisa kwenye haka kamgodi kanaitwa Ridhwani lazima watanzania wote tugawane haka katoto coz baba yake hafai ameshakuwa scraper. Imeshakuwa mbaya na iwe mbaya
 
Kujipanga tu tena sana sana ,fukuzeni mamluki wote waliopo kwenye chama makini,jiandaeni na 2015 maana si mbali,hata mkishindwa "urahis"mpate wabunge zaidi ya theluthi mbili...muweze kuendesha serikali kupitia bunge!!bila hivyo itabakia kulalamika milele amina
 
wewe ndio umekosa mwelekeo dhaifu wee,hata waliofichua pesa zilizo uswiss wamekosa mwelekeo?ole wako na hao magamba wenzio siku zenu zinakaribia mtalia na kusaga meno
Mtabaki hivyo hivyo tu. wewe umeshaambia CCM itatawala milele, sasa bado hujui tu maana ya MILELE? Nyie endeleeni kuchagamsha genge humu JF.
 
Tatizo si kukosa mwelekeo kwa Bwana Lema, hii ni Jamii forums, na kwamba mchanganyko wa mawazo ndo suluhisho na uhamsho wa kutatua Matatizo yetu. Lema ametoa taarifa kwa wanajamii kufuatilia. Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri, change za Rada ambazo sasa mjadara mzito Mjengoni, ilianza hivi hivi
 
Status
Not open for further replies.
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom