Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Jun 3, 2012.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.

  "Ndugu Wananchi;


  Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

  "Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge".

  Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .

  Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

  Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni "Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu" umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako. Hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa, Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar, mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

  Mh Rais, Mama Theresa, Nelson Mandela, Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao. Sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu, nahitaji dhamira safi, nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini, nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya. Ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta, magorofa, magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki, Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo. Pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi, Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe, hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho, nitakufa siku moja ambayo siijui, napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana, lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki. Kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana, unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako, niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

  Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

  Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

  Mh Rais "Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri" Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

  "ONLY TIME WILL TELL".


  GODBLESS .J. LEMA.

   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Jamani CDM msaidieni huyu mtu wenu. Naona kama hayuko sawa!
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Lema napenda unavyojiamini
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Dah,,,,hahahahahha..........nabaki naasama mdomo tu hapa....wanasiasa bhana,,,,,,leo yote yapo wazi,,,kumbe mlikaa Oysterbay?????shabassssh........
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Uko wapi Rweyemamu????njoo ujibu hapa.......hatutaki ubishi
   
 6. only83

  only83 JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kauli za kamanda Godbless Lema zinachochea kupigania haki, hakika huyu jamaa ni chachu ya mabadiliko kwa kizazi hiki...Endelea kamanda, bora kufa ukiwa unapigania haki na utu wa mwanadamu kuliko kuishi miaka 100 ya udhalimu na ujambazi. Godbless Lema ni mwanamapinduzi wa kweli hakika kauli zake zinachochea kupigania haki.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA, Mungu mbariki Godbless Lema.
  Tulianza na MUNGU, tunaendelea na MUNGU, tutamaliza na MUNGU.
   
 7. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa maneno ya Lema, haki daima hushinda dhuluma!
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Aisee... Kumbe hotuba ya JK ilitaja mtu... kweli simple people real have problems....
   
 9. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Pamoja sana mkuu
   
 10. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Duuh maneno mazito sana haya!...yaani yamejaa hekima,busara na hoja ya nguvu. Hongera sana Lema.
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Something is Wrong with Lema... time will tell.
   
 12. s

  silie Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu yu nawe,na haki ya kila mwananchi inaweza kucheleweshwa,lakini itakuja tu!!!
   
 13. magosha

  magosha JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mh Rais "Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri" Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Duuuuh hapa lazima tifu lizuke tena baina ya Ikulu na Lema, JK kalianzisha tena.
   
 15. a

  andrews JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  SALVA RWEYEMAMU UKAE DAR HUKOHUKO BAADA 2015 MAANA UKIJA BUKOBA UTATUELEZA KWANINI UMETUUZA KWA JAKAYA,NAPE NAE MWISHO NI 2015:israel:
   
 16. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Duh, katika kauli hii kuna mengi sana yaliyojificha
   
 17. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,200
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Sisi ni wafungwa wa kweli haki na usawa. Na hatutalala hadi vitu hivi vimetamalaki katika jamii yetu sasa na kwa vizazi vijavyo. Mwenye kuthulumu atafurikishwa na kimbunga cha ghadhabu ya Mungu na mwenye haki hata mafuriko yajapofurika kwa kiwango cha kusukwasukwa, bwana atainua kiwango dhidi yake. Bendera ya mwenye haki itapepea juu ya maji ya mafuriko daima, wala kamwe haitakaa izame ndani ya hayo maji yaliyofurika.
  .
   
 18. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Mh!! Nahisi baridi ghafla!
  Haya, ndio siasa hiyo.
   
 19. M

  Mohamed Ngwasu JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 304
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  du mie hoi.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  uchaguzi arusha ufanyike ili lema akatwe kilimi limi rasmi
   
Loading...