PRODA LTD
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,005
- 1,333
Lema aliza waumini wakati akitoa sadaka ya shukrani.
Mbunge wa Arusha na mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Godbless Lema leo akiongozana na mkewe na wanae ametoa sadaka ya shukrani kwa Mungu ndani ya kanisa la Winners Arusha.
Lema ametoa sadaka hiyo ya shukrani ikiwa ni siku mbili tu tangu aachiwe kwa dhamana baada ya kuzuiliwa gerezani kwa miezi minne.
Akizungumza mbele ya umati wa waumini mbunge huyo amesema hana kinyongo na yeyote aliyekusudia mabaya dhidi yake.Amesema wakati maadui zake wakikusudia mabaya dhidi yake kwa upande mwingine Mungu alikusudia mema kwake.
Mbunge huyo ambaye alilakiwa kama mfalme na wananchi alipotoka gerezani kwa kutandikiwa kanga ili apite juu yake amesema akiwa gerezani kila siku alikuwa anasali masaa manne mfululizo bila kuchoka.
Amesema katika maombi yake alikuwa anaombea Taifa,wabunge,viongozi na Rais John Pombe Magufuli.Lema amesema alichofundishwa na Mungu akiwa gerezani ni kuwapenda maadui na kuwaombea mema wale wanaomtakia mabaya.
Amesema anamshukuru sana Mungu kwani amembadilisha mno akiwa gerezani na yeye siyo yule Lema wa zamani.
Mbunge huyo maarufu kama Mandela wa Tanzania alikuwa akishangiliwa sana na waamini huku wengine wakibubujikwa na machozi ya furaha huku wakimtukuza Mungu.
Mbunge huyo mara baada ya Ibada amerejea nyumbani huku akitarajiwa kukutana na kada mpya na maarufu wa chama hicho Wema Sepetu kwa majadiliano maalum