Lema alishawaandaa watoto wake kisaikolojia - Mkewe

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Neema Lema, mke wa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, amesema yeye na watoto wake hawajutii kutokuwa na mwanasiasa huyo ambaye yuko mahabusu kwa kuwa anapigania haki ya kidemokrasia.

Lema, ambaye alikamatwa Novemba 2 mjini Dodoma, hatakuwa pamoja na familia yake msimu huu wa sikukuu baada ya Mahakama Kuu kutupa hoja zake za kupinga kunyimwa dhamana katika kesi inayomkabili ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. Mbunge huyo atakaa mahabusu hadi Januari.

“Mimi na hata watoto wangu, hatusikitiki kumkosa Lema ambaye yupo mahabusu. Tungejisikia vibaya sana kama Lema angekuwa mahabusu kwa kesi kama ya wizi au makosa mengine ya jinai,” alisema Neema

Chanzo: Mwananchi
 
Kosa la Lema lina dhamana kisheria...

Mhimili wa Mahakama sasa ni rasmi unaingiliwa na watawala.

Kwenye hili nasema watawala mnaona mnamkomoa Lema na CDM, lakini it's just a matter of time... u will prove urself that u were absolutely wrong.

Mungu endelea kumpigania Godbless Lema huko alipo.
 
Bunge,mahakama vyote kwa sasa vipo chini ya serikali. Serikali inatumia nguvu kubwa sana kubana hii mihimili mpaka inashindwa kufanya kazi yake. Kesi ya Lema ina dhamana lakini kwa kuwa RC wa arusha ana bifu nae basi vyombo vya dola vinaingilia uhuru wa mahakama na pili inaonekana ni order kutoka juu kwa lengo la kumkomoa Lema. Nway sisi sote tunapita hapa dunian na hatujui kesho kitatokea nini, lakini malipo ni hapa hapa duniani. Hawa viongozi wanaijiona miungu watu sasa hivi baadae watajiona mashetani.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ni aibu kubwa kutafuta kiki kwa kutoa maneno ya dharau kwa viongozi...mbona kwa nasari hakuna huu upuuzi??we mwanamke tulia ulee watoto..usije ukajazwa upepo kama mumeo kisha ukaishia ndani..mkitoka mtakuta kijana wako watu washafanya yao anabinua kiuno tu..kaa na Joyce kiria akufunde
Ushabiki kwny masuala ya kisheria au mahakama sio issue

Hapa issue kubwa ni dhamana na kosa analoshtakiwa lema lina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Kumbuka dhamana ilishatolewa, upande wa jamhuri wakapinga wkt bail was granted sasa hapa ndo tunawasiwasi kwnz sio taratibu za kimahakama iko hv mahakama ikishatoa maamuzi yoyote upande ambao upo aggrieved unashauriwa ukate rufaa sasa kwny hili yametoka maamuzi mawili kuruhusu dhamana alafu kukataa bila upande wowote kukata rufaa hapa kuna maana kwamba kama kulikuwa kuna pingamizi la dpp la kupinga dhamana lingetoka kabla ya maamuzi ya mahakama

Hakuna njia yoyote ya kupinga maamuzi ya mahakama zaidi ya kukata rufaa dpp hakufanya hivyo

Lakini ni mahakama hiyohiyo ndio ilishauri ikatwe rufaa alafu imeikataa

Kwa hiyo hapa tunaongelea kesi ya lema ina dhamana hayo mambo mengine ni ya kifamilia zaidi hatuwezi kuingilia
 
Mbowe huu upuuzi hataki hata kuusikia huwezi kumuona hata siku moja na familia yake kwenye siasa wao wanakula ruzuku tu.
 
Bunge,mahakama vyote kwa sasa vipo chini ya serikali. Serikali inatumia nguvu kubwa sana kubana hii mihimili mpaka inashindwa kufanya kazi yake. Kesi ya Lema ina dhamana lakini kwa kuwa RC wa arusha ana bifu nae basi vyombo vya dola vinaingilia uhuru wa mahakama na pili inaonekana ni order kutoka juu kwa lengo la kumkomoa Lema. Nway sisi sote tunapita hapa dunian na hatujui kesho kitatokea nini, lakini malipo ni hapa hapa duniani. Hawa viongozi wanaijiona miungu watu sasa hivi baadae watajiona mashetani.
Kweli kabisa malipo ni hapa hapa duniani, Lema alijigamba sana kuwa yeye ndiye aliyemundoa mkuu wetu Felix Ntibenda na angemundoa Gambo muda mfupi kama alivyong'oka Felix, sasa yeye mwenyewe ndo anaongelea nyuma ya nondo.
 
Ushabiki kwny masuala ya kisheria au mahakama sio issue

Hapa issue kubwa ni dhamana na kosa analoshtakiwa lema lina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Kumbuka dhamana ilishatolewa, upande wa jamhuri wakapinga wkt bail was granted sasa hapa ndo tunawasiwasi kwnz sio taratibu za kimahakama iko hv mahakama ikishatoa maamuzi yoyote upande ambao upo aggrieved unashauriwa ukate rufaa sasa kwny hili yametoka maamuzi mawili kuruhusu dhamana alafu kukataa bila upande wowote kukata rufaa hapa kuna maana kwamba kama kulikuwa kuna pingamizi la dpp la kupinga dhamana lingetoka kabla ya maamuzi ya mahakama

Hakuna njia yoyote ya kupinga maamuzi ya mahakama zaidi ya kukata rufaa dpp hakufanya hivyo

Lakini ni mahakama hiyohiyo ndio ilishauri ikatwe rufaa alafu imeikataa

Kwa hiyo hapa tunaongelea kesi ya lema ina dhamana hayo mambo mengine ni ya kifamilia zaidi hatuwezi kuingilia
Unawafundisha kazi yao wakina Kibatala?
 
Neema Lema, mke wa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, amesema yeye na watoto wake hawajutii kutokuwa na mwanasiasa huyo ambaye yuko mahabusu kwa kuwa anapigania haki ya kidemokrasia.

Lema, ambaye alikamatwa Novemba 2 mjini Dodoma, hatakuwa pamoja na familia yake msimu huu wa sikukuu baada ya Mahakama Kuu kutupa hoja zake za kupinga kunyimwa dhamana katika kesi inayomkabili ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. Mbunge huyo atakaa mahabusu hadi Januari.

“Mimi na hata watoto wangu, hatusikitiki kumkosa Lema ambaye yupo mahabusu. Tungejisikia vibaya sana kama Lema angekuwa mahabusu kwa kesi kama ya wizi au makosa mengine ya jinai,” alisema Neema

Chanzo: Mwananchi
Hata masheikh wamekaa ndani mwezi wa Ramadhani na sikukuu ya IDD

Wacha tu akae ndani, masheikh na wao ni binadamu kama yeye...
 
Back
Top Bottom