Lema akwepwa; Atakiwa kuleta ushahidi kwa maandishi siyo kuhutubia!

Mbunge wa Arusha Mheshimiwa Godbless Lema amesikitishwa na kitendo cha Spika wa Bunge Anna Makinda Samamba kutomruhusu kuwasilisha ushahidi wa Waziri Mkuu Pinda kulidanganya bunge.

Source:

 
Last edited by a moderator:
Kila kina mwisho hata misri rais aliyetumua hakufikili kuwa hipo siku ataachia madaraka.
mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni ,:clap2:
 
Apola Katutu, yiposile yonsi., Endita mkwai
Jamani mtoto wa mkulima niombe ushauri mie mdogo wako na uchungu maana unavyotumiwa kuwakingia kifua wafilisi nchi dhamiri yako inakusuta na hata heshima ya mtoto wa mkulima wa Wilaya yako ya uchaguzi ya Lyamba Lya ...... kule katavi utapoteza umaarufu wako.
Kuwa mkweli tu kuliko mtindo wa kujibu hoja kisiasa wakati bungeni ni hoja za kisheria.
 
Pinda naona siku hizi anaimba sana ule wimbo wa "CCM Pambalama, pokeleli CCM ehh, pokeleli CCM pambalamba......"

Watani zangu Wafipa bana, mababe walikuwa ni Nswima na Mzindakaya.

Ila Mzindakaya alikuja akalishwa KEKI za Mafisadi, akanogewa.
 
hilo mbona tulishajua toka zamani tu kuwa hawatamruhusu kuhutubia bunge.
Bado wanaficha uchafu wao.
Hata kama wangemruhusu basi jua jana siku nzima kusingekuwa na umeme ili msimwone kwenye TV
 
Nampongeza mh spika kwa kukwepa aibu ambayo serikali ingepata. Binafsi nilijua pmalipewa wroong info na akapresent hivyo hivyo kama CCM walivyozoea. Nadhani wazee kama Sitta , EL na wengine wamemshtua kuwa alichemsha so amefundishwa busara za kispika. Ukweli alikurupuka anatumia zaidi hisia sio busara.unadhani kama Lema akitoa ushahidi na ukawa na uzito zaidi what next. Busara zitumike Bungeni.
 
Huyu spika wa sasa na Waziri wake mkuu wasipuzinduka na kuacha propaganda na ushabiki wa kiCCM ndani ya Bunge, wanaaibisha sana. Wabunge wengi wa upinzani ni vijana makini na jasiri sana, zile enzi za ndio mzee na nidhamu za woga na kinafiki zimepitwa na wakati. Hizi ni zama za ukweli na uwazi, na wananchi tumezinduka sana, tuna uwezo wa kuchambua kati ya mbivu na mbovu. Kazi kwako Makinda na Pinda, ukweli na uwazi ndio utakaowarudishie heshima ambayo imeshapotea!
 
Wanajamii members nadhani tumpe pongezi speaker kwa kutomruhusu LEMA kuhutubia.Nchi ingechafuka maana kila mmoja angepata habari za mjengoni kuwa ni za ukweli halafu unadhani lile lichama letu la zamani hapangetosha.Mi naamin peoples power inanguvu zaidi bwana. Wee twendeni polepole tutawabamba tu na ukichukulia muheshimiwa AKAEL mwana wa MBOWE kashatangaza baraza lake makini tusiwe na haraka kwani hoja zimeishaa narudia kusema tutawabamba tu.
 
Wanajamii members nadhani tumpe pongezi speaker kwa kutomruhusu LEMA kuhutubia.Nchi ingechafuka maana kila mmoja angepata habari za mjengoni kuwa ni za ukweli halafu unadhani lile lichama letu la zamani hapangetosha.Mi naamin peoples power inanguvu zaidi bwana. Wee twendeni polepole tutawabamba tu na ukichukulia muheshimiwa AKAEL mwana wa MBOWE kashatangaza baraza lake makini tusiwe na haraka kwani hoja zimeishaa narudia kusema tutawabamba tu.
 
sasa spika akinyamaza tutajuaje aliyemwongo ni nani kati ya lema na pinda. hebu spika atupe mwongozo ili tuweze kutoka hapo
 
Wanajamii members nadhani tumpe pongezi speaker kwa kutomruhusu LEMA kuhutubia.Nchi ingechafuka maana kila mmoja angepata habari za mjengoni kuwa ni za ukweli halafu unadhani lile lichama letu la zamani hapangetosha.Mi naamin peoples power inanguvu zaidi bwana. Wee twendeni polepole tutawabamba tu na ukichukulia muheshimiwa AKAEL mwana wa MBOWE kashatangaza baraza lake makini tusiwe na haraka kwani hoja zimeishaa narudia kusema tutawabamba tu.
 
Now Whats Next...?
Lema Kuandika Barua...., Speaker Kukaa Nayo Ofisini...., Nothing Happens Till 2015
Same Old Same Old Story...

Nilimsikia Spika na kusoma maneno yake akimtaka Lema afikishe utetezi wake. Nilikuwa nasubiri kusikia upande wa pili kama alivyoshauri Makinda ili niweze kujiridhisha ukweli au uzushi wa Lema. Kama Makinda akikalia taarifa ofisini kwake, mimi sioni tatizo kwasababu nitabaki na kauli iliyowekwa hadharani na Lema kuwa Pinda kalidanganya Bunge.
 
Bora nipigwe risasi kuliko kufuta kauli-Lema


Na Pendo Mtibuche, Dodoma

MBUNGE wa Arusha mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Bw. Godbles Lema amesema kuwa yupo radhi achague
kupigwa risasi kuliko kufuta kauli yake aliyotoa bungeni wiki iliyopita kuwa Waziri Mkuu amesema uongo kwa kuwa ana ushahidi kwa asilimia mia moja na ana uhakika nao.

Kauli ya mbunge huyo ambayo ilisababisha Spika Anne Makinda kumtaka athibitishe kauli hiyo kwa maandishi kufikia jana, aliitoa Februari 10, mwaka huu bungeni akidai kuwa Waziri Mkuu amelidanganya bunge kuhusiana na mauaji ya Arusha.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bw. Lema alibainisha kuwa alikuwa tayari kusoma uthibitisho wake bungeni jana lakini cha kushangaza ni kwamba spika amemtaka awasilishe katika ofisi yake kwa maandishi.

“Mimi nilikuwa tayari na ushahidi wangu na bado nipo vizuri, nilikuwa niwasilishe ushahidi wangu bungeni, sasa naambiwa niwasilishe ushahidi wangu ofisini kwa spika, nipo radhi nichague kupigwa risasi kuliko kufuta kauli yangu ambayo niliitoa hivi karibuni bungeni, kwa kuwa nina ushahidi wa
uhakika,� alisema Bw. Lema.

Hata hivyo, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, mbunge huyo alikataa kuulizwa maswali kuhusu kilichomo kwenye ushahidi wake.




1 Maoni:

blank.gif

ngereja said... wabunge chadema simamieni maslahi ya wanyonge tuko nyuma yenu
February 14, 2011 8:25 PM
 
Lema: Bora kupigwa risasi sifuti kauli

Tuesday, 15 February 2011
Exuper Kachenje, Dodoma

MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbelss Lema, amesema ni heri kuchagua kupigwa risasi kuliko kufuta kauli yake kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amedanganya jamii.

Lema alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma kwenye mkutano na wanahabari muda mfupi baada ya kushindwa kuwasilisha
uthibitisho wake bungeni kwa kusoma, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuelekeza kupelekewa ushahidi huo kwa maandishi.

"Nina ushahidi, nyie jueni hivyo. hata nikiambiwa nichague kati ya kupigwa risari na kufuta kauli yangu, nitachagua kupigwa risasi," alisema Lema na kuongeza:"Nilipangiwa ifikapo leo niwe nimewasilisha ushahidi wangu, nilikuwa tayari leo kwa mujibu wa maelekezo ya spika na Kanuni za Bunge, nimekuwa discouraged (Nimekatishwa tamaa) kwa nini hakunipa nafasi?"

Hata hivyo, Lema alisema yupo kwenye hatua za kuwasilisha ushahidi wake huo bungeni, huku akijinasibu kuwa alijiweka vizuri.

Hata hivyo, Lema hakuwa tayari kuwasilisha aina ya ushahidi au kutaja maeneo ambayo ameona Pinda amedanganya jamii.

"Sitaki kuvunja Kanuni za Bunge, lakini nilikuwa nimekuja kuwasilisha ushahidi, sijui kwa nini leo naambiwa ni kwa maandishi sio bungeni kama awali Spika alivyotaka?" alihoji Lema.

Awali, kabla ya Lema kuzungumza na wanahabari Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, alisimama bungeni na kuomba mwongozo wa Spika akikariri kifungu cha 63 cha kanuni za Bunge, kumkumbusha kuhusu Lema kutoa ushahidi wake bungeni.

Hata hivyo, Makinda licha ya kukiri kuwa jana ndio siku aliyomtaka Lema kuwasilisha uthibitisho wa madai yake, alimtaka kufanya hivyo kwa maandishi.

"Leo, ndivyo nilivyosema leo ataleta, lakini kwa mujibu wa Kanuni, leo ataleta kwa maandishi naye Spika ataendesha kwa namna anavyoona. Kwa hiyo ataleta kwa maandishi,"alisema Makinda.

Wakiwa katika mkutano wa hadhara Jumamosi iliyopita, wabunge wa Chadema walisema chama kimejipanga kuhakikisha Lema anatoa ushahidi kuhusu madai kuwa, Pinda alidanganya umma.

"Waziri Mkuu alitaka kugeuza Bunge kama jukwaa la Propaganda, akalitumia kuwadanganya wananchi, lakini Jumatatu (jana) atajibiwa na wote mtaona, labda wakate umeme. Hakikisheni 'majenereta' yenu yana mafuta mpate kujua yaliyowapata wenzenu Arusha," alisema Halima Mdee, Mbunge wa Kawe.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Lema, aliyesema tayari alikuwa amepata mambo 23 aliyodai Pinda alidanganya Bunge kuhusu mauaji ya Arusha.

"..Mnyika na Lisu walipitia majibu ya Pinda na kugundua maeneo 13 ambayo ni uongo 23 hadi sasa kulingana na tukio halisi lilivyokuwa na bado wanaendelea kupitia na kuchambua mkanda wa video," alisema Lema.

http://mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/9301-lema-bora-kupigwa-risasi-sifuti-kauli#
 
Mimi ninashindwa kuelewa hii hoja ya kulinganishwa mwenendo wa shughuli za Kibunge na kupigwa risasi sijui uhusiano wake unatoka wapi..............................tangia tupate uhuru maeneo ya Bunge kamwe hayajawahi kusikika mirindimo ya risasi .............sasa sijui haya malinganishi haya yanatoka wapi?
 
Back
Top Bottom