Lema akutana na Meya wa jiji la London nchini Uingereza

Kiingereza kama zilivyo lugha zingine, ni chombo cha mawasiliano lakini siyo utaalam wala siyo kipimo cha elimu au ujuzi. Wakuu wa China, Ujerumani, Urusi, Italy, n.k. wakienda mataifa mengine wanaongea lugha zao, siyo kiingereza, na hilo haliwapunguzii chochote. Kama Lema kiingereza kama hakijui, anaweza kuongea kiswahili, na hilo halitampunguzia chochote.
Humu JF, wengi wa wasiokijua kiingereza ndiyo wanaonekana kuhusudu sana mjadala wa lugha, kwa vile ni kitu kinachowasumbua, wanadhani ni kitu muhimu sana. Nenda kule Brazil, Chile, Argentina, Peru, Mexico na hicho kiingereza chako cha kubabaisha ungejiona kutokuwa tofauti na yeyote asiyejua hata neno moja la kiingereza. Bila hata ya kiingereza, leo uchumi wa Brazil ni wa tano kwa ukubwa Duniani.

Mkuu umeongea mengi bila sababu tatizo hapa sio masuala ya uchumi watu wanahoji Lema kaongea nini na huyo Meya wa London wakati hajui kingereza bahati mbaya Meya wa London naye hajui kiswahili...unatakiwa kujibu hili.
 
CDM na wao wanafungua matawi nje ya nchi sasa ...

CCM london fanyeni kazi ya kutosha wasipate wanachama huko
 
Mbona hujataja jina la mkalimani wake au yeye siyo muhimu?

Lema anaongea grammer english ambacho hakuna mwanasiasa nchi hii anayeweza pambana nae mdomoni..mind u pia lema anaongea kwa ufasaha ki portugal,na pia kihispaniola.PERIOD
 
Kauli mbiu ya cdm nadhani ni twanga kote kote. Kwa hivyo usiseme iweje waanzishe matawi ughaibuni wakati vijiji vingine hawajafika.

Kazi iliyopo ni kubwa na inashirikisha wote; wa vijijini twende, wa kwa Boris twende. Boris kama ana tatizo la lugha basi atafute yeye mkalimani. Akiongea lugha ya taifa lake Lema atamsikia; na Lema akiongea lugha ya tafa lake Boris aidha amsikie au atafute yeye mkalimani.
 
Aliyeuliza english kwa lema NIMEAMINI HAMJUI GODIII...SUBIRI WANAOMJUA PERSONAL WATAKAVYOKUTUSI.katika vitu lema anavyoringia ni HILO YAI MDOMONI.
 
Lema anaongea drammer english ambacho hakuna mwanasiasa nchi hii anayeweza pambana nae mdomoni..mind u pia lema anaongea kwa ufasaha ki portugal,na pia kihispaniola.PERIOD

Mkuu Drammer english ikoje? Inatofauti na Grammar english? Kweli Lema kiboko.
 
CDM na wao wanafungua matawi nje ya nchi sasa ...

CCM london fanyeni kazi ya kutosha wasipate wanachama huko

Watafanya nini? wanachama wote wa ccm london ni njaa kali na wanajiunga na CCM ili iwatoe. Chadema ni wajanja ambao ndio wenye hela na wana maisha mazuri mtakachokiona ni kundi kubwa la wana ccm kujiunga na chadema
 
CCM london ni kama akina Haruna Mbeyu, jestina George, na washamba wengine njaa kali ambao hawana kazi bali huzengea pilau la ccm wakifika viongozi, wao hushinda nje ya mahoteli kuwasubiri viongozi.
 
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini kabla ya jk kumfanyia uhuni na kuingilia uhuru wa mahakama Mh Godbless Lema, Amewasili mjini Londoni Uingereza.

Kuwasili kwa kamanda lema hapa uingereza na kukutana na Meya wa jiji hili la Londoni hapo j4 nikielelezo tosha kuwa kamanda huyo anafanya siasa za kimataifa kwasasa. Lema amewasili jana akitokea Tanzania.

Lengo lingine la safari hii ya kamanda Lema ni Uzinduzi wa M4C unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam tarehe 10/08/2012. Baada ya uzinduzi huwo Lema na Timu yake ya M4C vile vile inategemewa kwenda kwenye mataifa mbalimbali duniani kupeleka ujumbe wa M4C kwa watanzania waishio nje ya Tanzania, Lema atazindua matawi takribani saba nchini uingereza, atawasili jiji Dar es salaam siku ya alhamisi kwaajili ya uzinduzi huwo.

Vile vile Katibu wa Chadema toka Marekani anatarajia kuwasili nchini Tanzania siku ya kesho ambapo atapokewa na Mkt wa M4C Dar es salaam Bw Alex Mayunga na kamati yake pamoja na Katibu wa Chama Bw Kilewo.

Kuwasili kwa Katibu huyo toka nchi marekani ni muendelezo wa wageni mbalimbali toka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria tukio hilo kubwa na lakihistoria ukiachia lile la Arusha kipindi cha kampeni. Changia M4C kupitia Namba 111333 tulikomboe taifa letu, Lengo ni kukusanya 5 bil, inawezekana

samahani kwa swali hili LEMA ALITUMIA LUGHA GANI VILE!!!!!!!
 
TOpic yenyewe Matangazo tupuuu...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
ccm london ni kama akina haruna mbeyu, jestina george, na washamba wengine njaa kali ambao hawana kazi bali huzengea pilau la ccm wakifika viongozi, wao hushinda nje ya mahoteli kuwasubiri viongozi.

yaani katika matawi ya ccm yalio nje ccm london wapo makini mkuu
 
Jamani CDM ina uhaba wa wasomi? Kweli unapeleka mtu asie kua na elimu ukitegemea nini? Atazungumza nini na mayor wa london wakati hata kuongea kizungu ni tabu. Huyu kapata dili zuri kweli baada ya kutolewa ubunge.
 
Back
Top Bottom