Lema afichua njama CCM; Ametoa ufafanuzi kuwa Gervas Mgonja si katibu wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema afichua njama CCM; Ametoa ufafanuzi kuwa Gervas Mgonja si katibu wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 24, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  na Grace Macha, Arusha


  MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ametoa ufafanuzi kuwa Gervas Mgonja si katibu wake kama ilivyodaiwa na vyombo vya habari kwani alishamuachisha kazi tangu Juni 16, mwaka huu.


  Mbunge huyo alisema taarifa hiyo imetokana na mkakati wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutaka kumchafua kwa kumhusisha na ujambazi.


  Mgonja anashikiliwa na polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuhusika na ujambazi.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Lema alisema katibu wake hivi sasa anaitwa Lucia Fransisco na alishaandika barua kwa viongozi mbalimbali wa kiserikali ikiwemo jeshi la polisi kuwajulisha mabadiliko hayo.


  Lema alisema kuwa taarifa za kumuachisha kazi Mgonja alizitoa miezi mitatu lakini ameshtushwa na baadhi ya vyombo vya habari kuandika kwamba huyo bado ni katibu wake.


  Tanzania Daima, lilipata nakala ya barua ya Lema kwenda kwa mkuu wa polisi mkoa wa Arusha (RPC) na mkuu wa polisi wilaya ya Arusha (OCD), akiwajulisha juu ya kumsimamisha kazi Mgonja na uteuzi wa Lucia.


  Sehemu ya barua ya Lema iliandikwa hivi: “Kuanzia Juni 16, mwaka huu, Lucia ndiye katibu wangu na kama kutatokea mabadiliko yoyote nitawaarifu, kwa msingi huo Gervas Mgonja siyo katibu wangu tena kuanzia sasa.”


  Kwa mujibu wa Lema, katika siku za hivi karibuni ameanza kupata hisia kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia mbinu chafu kumhusisha na makosa ya kihalifu ili kumdhoofisha kisiasa.


  Alisema baada ya kusikia taarifa za gazeti hilo alimtumia ujumbe mfupi wa simu Mkuu wa Polisi mkoa wa Arusha (RPC) kusikitikia kitendo hicho.


  “Kamanda RPC, nakusalimia nimefuatilia magazeti asubuhi ya leo nimeona moja linasema katibu wa mbunge ahojiwa kwa ujambazi, ninatambua unayo barua kwa OCD na ngazi zote husika.


  “Mgonja siyo katibu wangu kwa muda mrefu sasa, kama taarifa hiyo ni ya polisi, basi nitakuwa mwenye huzuni kuwa sasa hata jeshi la polisi linafanya kazi kisiasa, hata hivyo haki na utu havijawahi kushindwa. Asante na siku njema.”
  Jana, gazeti moja, liliripoti kuwa katibu wa mbunge wa Arusha mjini, Gervas Mgonja, anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.


  Kwa mujibu wa gazeti hilo Mgonja anatuhumiwa kuhusika na matukio kadhaa ya ujambazi mkoani Arusha na gari lake binafsi linahusishwa kuwabeba watuhumiwa wa ujambazi.


  Wakati huohuo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Arusha Mjini kimesema kuwa Gervas Mgonja anayeshikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ujambazi si katibu wa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.


  Mwenyekiti wa wilaya hiyo, Ephata Nanyaro, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa Mgonja aliachishwa kazi kwenye ofisi ya mbunge toka Juni 16, mwaka huu, hivyo taarifa zilizotolewa zikimuelezea kuwa ni katibu wa Lema zilikuwa na lengo la kukichafua chama.


  Alisema ofisi zote za umma kwenye wilaya ya Arusha zimeshaandikiwa barua kujulishwa mabadiliko hayo ya uongozi katika ofisi ya Mbunge.


  “Tunalitaka jeshi la polisi kusimamia ukweli na haki, kamwe lisihusishe tukio la Mgonja na CHADEMA wala lisijihusishe na siasa; na tunaomba sheria ichukue mkondo wake na sisi tutatoa ushirikiano pale tutakapohitajika kufanya hivyo,” alisema Nanyaro.


   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hivi habari leo ni ya serikali kweli? Inashangaza na kufedhehesha chombo cha umma kutumika vibaya. Naungana na Mbunge wangu Mh. Lema kwamba pamoja na mbinu mbaya wanazotumia ccm kutaka kuichafua chadema na mbunge, hawataweza, badala yake ccm wanajipaka mavi wakisaidiwa na jeshi la polisi. Haki haijawahi kushindwa hata siku moja
   
 3. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Washapoteza muelekeo, wanatafuta jambo jipya ili wananchi wasahau upupu wao wanaoufanya.
  Kwa lugha nyepesi wanataka kubadili mada.
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Huu si wakati wa kuaminishana kwa maneno kama wanavyozani magamba huu ni wakati wa kuamini kwa kutumia ushahidi zaidi ya maneno na hili linajidhihirisha kila siku, na hongera cdm kwa kuwa makini na hawa magamba kamwe naamini hamtoyumbishwa na haya mawimbi ya kikombe cha chai
   
 5. O

  Oikos Senior Member

  #5
  Aug 24, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu Wananchi, mfa maji haachi kutapatapa. CDM iweni makini kwa hili ili hawa jamaa wasipunguze kasi yenu. Tuko pamoja mpaka kieleweke!
   
 6. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #6
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lets be serious tumsafishe Mbunge wetu.Kwa nini Mh.LEMA baada ya kutuhumiwa kuwa ni jambazi Hakwenda mahakamani wakati Zombe alisema anaushahidi.Mh.Lema ni mtu mkubwa sana ambaye si wa kutuhumiwa tuhuma nzito namna hii kisha akabaki kukanusha kwenye media bila ya kumtaka aliyeshutumu athibitishe.Hii inanikumbusha serikali wanapotuhumiwa kusema uongo bungeni na ikawa ni kweli wataomba uthibitisho kisha wanakaa kimya baada ya kuumbuka.Sasa hii ya aliyekuwakatibu wako tena eti na yeye ni jambaz.Hata kama unasingiziwa kwa nini tuhuma zilezile tena na watu wako wa karibu ama ndo network yenyewe.NINAWASISI SANA NA LEMA JUU YA HIZI SKENDO ZA UJAMBAZI HALAFU HATA KUOMBA ATHIBITISHIWE HATAKI...Tusiojua kitu tutabaki kuamini kwamba rafiki wa wa mwizi ni mwizi ama yawezakuwa tunaongozwa na Jambazi naomba Mungu isije ikawa hivyo.HON.LEMA prove to us that u a not(Kinachonsumbua Zombe kadai anaevidence kwa nini usiende mahakamani azioneshe ili umprove wrong?).Supporter wako niko njiapanda.Binafsi sifurahii jinsi watu wanavyoanza kukuita mbunge j...IF U ARE NOT MUNGU AKUPIGANIE MPAKA MUONGO ATAKAPOUMBUKA NA UTAKAPOKUWA PROVED INNOCENT.
   
 7. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Time is telling now. Kila lililofanyika mafichoni yatatokea.
   
Loading...