Lema aahidi kujenga Machinga Complex | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema aahidi kujenga Machinga Complex

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchakachuaji1, Dec 8, 2010.

 1. m

  mchakachuaji1 Senior Member

  #1
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Happy Lazaro, Arusha (Mwananchi)

  MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, anatarajia kujenga machinga Complex tatu na hospitali moja, ndani ya miaka mitatu, ili kusaidia wananchi kwa urahisi.

  Akihutubia mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi kwenye viwanja vya NMC, mjini hapa, Lema alisema hayo yatatekelezeka kwa urahisi kutokana na kushirikiana wa marafiki zake wa London, Uingereza.


  "Hawa vijana wa London wameona sasa kuna mtu wa kumpatia fedha zao, kwa sababu wana uhakika na mbunge aliyopo ndio maana wameamua kutoa fedha zao kwa kasi ya ajabu, kinachotakiwa kwangu ni uaminifu tu," alisema Lema.

  Lema alisema eneo la kujenga hospitali tayari lipo na sasa wanachofanya ni kutafuta maeneo ya wazi au yaliyochukuliwa na mafisadi, kuyarudisha mikononi mwa wananchi, kisha kujenga vitu vya kuwasaidia badala ya kunufaisha wachache.

  "Katika hili nasema tutafanikiwa, kwa sababu tayari Waziri Anna Tibaijuka, aliahidi kuvalia njunga maeneo yaliyotaifishwa na kumilikiwa na mafisadi na kuyarudisha mikononi mwa wananchi, hivyo tayari na mimi kwa kushirikiana na madiwani wengine, tumeandika barua ya kuorodhesha maeneo yaliyochukuliwa na mafisadi ambayo ya wazi," alisema Lema, huku akishangiliwa na umati wa watu.

  Alisema kazi nyingine ambayo ataizindua Juni 2011, ni taasisi ya kusaidia wanawake kwa kutoa mikopo ya riba nafuu, ili waweze kukidhi mahitaji yao ya uchumi wao.


  Pia, aliomba wananchi kuwa tayari kumsindikiza watakaposikia amefikishwa mahakamani na aliyekuwa mgombea mwenzake kupitia CCM, Dk Batilda-Salha Buriani.

  "Mnajua ndugu zangu bila umoja hatutafika kwani, ni wazi hata siku ya kutangaza matokeo msingekomaa manispaa, matokeo yalikuwa yanageuzwa kichwa chini miguu juu…hata mahakamani njooni msikie maana ni chama chenu kinafikishwa," alisema Lema.


  Alisema anaamini ataibwaga CCM na kuipatia aibu ya pili, kwani kila kitu kiko wazi na kila kituo kulikuwa na mawakala, hivyo anashangaa kuona Dk Buriani hakubali ukweli
   
 2. m

  mchakachuaji1 Senior Member

  #2
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya sasa wadau naona vijana wetu wanaanza kufanya kazi tulizowatuma, sasa kazi yetu ni kuwaunga mkono na kuwapa moyo katika utekelezaji wa majukumu yao.
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ameanza sasa. Hao mvijana wa London ni wakina nani? Kwa mtaji huu hatutafika kokote maana tunaendekeza tabia ya kutembeza vibakuli!

  Amandla....
   
 4. Elizaa

  Elizaa Senior Member

  #4
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hongera Lema, fanya kazi tuliyokutuma. Misaada iwafikie walengwa na siyo kuliwa na wachache.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Good move!...congrats!
   
 6. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Safi sana Godbless Lema huo ni mwanzo hakika siku ukiitwa mahakamni tuko pamoja kama tulivyofanya ile siku tukisubiri matokeo PEOPLES POWER! Napia sintaacha kukupa BIG UP Lema kwakuonyesha ukaribu wako na wananchi wa jimbo lako kunasiku ulikuja SHORE SHINE kwenye kijiwe pale kwenye baraza ya KCB (Bank) na kukaa na wananchi na kutaka kujua wananchi wa jimbo lako wana kero gani ya maendeleo! BIG UP kaza buti! :whoo:
   
 7. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  yetu macho .
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni COVER Mkuu............
   
 9. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwenye nyekundu - Mbunge anatakiwa alete maendele jimboni kupitia kodi zetu kwa maana ya kuisimamia serikali au kwa juhudi binafsi ikiwemo kutembeza bakuli?
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
Loading...