Legacy ya Rais Benjamin Mkapa ni nini kwa Watanzania?

Carlos Valderrama

JF-Expert Member
Dec 27, 2014
664
240
images-6.jpeg

Rais Mkapa, alikuwa na kazi moja kubwa, kuimarisha hatua zilizopigwa na awamu ya pili hasa katika kuendelea kuupanga na kuuimarisha uchumi wetu katika mfumo mpya tuliouchukua. Serikali ya Awamu ya tatu chini ya uongozi wa Mzee Mkapa ilijikita katika kuhakikisha kuna “transition” nzuri kutoka uchumi uloshikwa na dola awali kwenda uchumi huria ambao umeshikwa na watu katika sekta binafsi.

Wadau wa JF tupeni michango yenu.
 
Mkapa alimaintain mfumo wa bei sana, enzi za Mwinyi inflation ilifika zaidi ya asilimia 34 mtakumbuka Kanda Bongo Man aliwahi kufanya shoo kwa kiingilio cha nadhani zaidi ya laki moja, hiyo yote sababu hela ilikuwa imezagaa hovyo.
Mkapa alibana sana, japokuwa reflection kwa wananchi ilionesha maisha magumu kumbe hela kidogo iliyopatikana ilikuwa na thamani.
Japokuwa baadhi ya watu wanaona Mkapa alionekana kuperfom sababu aliuza mashirika, hivyo alipata fedha nyingi.
 
Huyu mzee alithibiti Mfumuko wa bei, nauli ilikaa shilingi 150 kwa muda mrefu sana

Alirudisha heshima ya mfanyakazi wa serikali.

Alitujengea uwanja wa Taifa, siku hizi wachezaji wetu hawashangai viwanja huko nje ya nchi.

Alianzisha taasisi nyingi.

Ben Mkapa safi, tatizo moja la kwake ni kuuza benki ya NBC kwa bei ya kutupwa!
 
wacha upotoshaji!

all in nall huyu mzee tutamkumbuka kw akulipa madeni ya nje!
magufuli anaujanja inabidi amuige mkapa badhi ya sera za uchumi, hasa za kubana mikanda na kuleta thamani ya hela.
 
Benjamin William Mkapa ndio Mtanzania pekee niliyewahi kumshuhudia kuwa na uwezo mkubwa sana sana sana wa kueleweka kwa wasomi. Anajua sana kujieleza. Ubora wa hotuba za Mwl Nyerere 1960s zilitokana na kazi ya Mwandishi huyu ila alikuwa haeleweki kwa Wapumbavu wengi wanaopenda kusikia yale mazuri yasiyotekelezeka mf. Igizo la ujamaa na kujitegemea.
Hakuwa na blaablaa za siasa kama kina Nyerere( Ujamaa na kujitegemea), Kikwete( Maisha bora kwa kila mtanzania na Magufuli( Nchi ya viwanda). Kisichowezekana anasema na kinachowezekana anasema. Huyu alikuwa Mtawala hasa kwa maana ya Power and Authority. "Hiyari ya jambo ipo kwenye kukubaliana ila kutekeleza mliyokybaliana kwa hiyari ni lazima"-Benjamin William Mkapa akizungumzia kuunga mkono michango ya hiyari Mashuleni
 
Ndo hivyo, na ndo maana nikasema wengine wanaamin hivyo. Lakin ni kweli kuwa Mkapa aliuza taasis nyingi sana serikali. Ubinafsishaji ni sera yake, pia clip iliwahi kuwekwa humu jf Sumaye akiongelea uuzwaji wa nyumba za serikali. Iko open kabisa.

wacha upotoshaji!

all in nall huyu mzee tutamkumbuka kw akulipa madeni ya nje!
magufuli anaujanja inabidi amuige mkapa badhi ya sera za uchumi, hasa za kubana mikanda na kuleta thamani ya hela.
 
Ule uliomhusu rais mwinyi changanya na huu wa mkapa umeingiliwa na watu wenye akili ndogo zinazowaza udini..kama unauwezo utaliona hili..
 
Huyu mzee alithibiti Mfumuko wa bei, nauli ilikaa shilingi 150 kwa muda mrefu sana

Alirudisha heshima ya mfanyakazi wa serikali.

Alitujengea uwanja wa Taifa, siku hizi wachezaji wetu hawashangai viwanja huko nje ya nchi.

Alianzisha taasisi nyingi.

Ben Mkapa safi, tatizo moja la kwake ni kuuza benki ya NBC kwa bei ya kutupwa!
kwa sakata la NBC hata Jk Nyerere alitokwa na chozi
 
Alikua na IGP mmoja matata sana.
Mahita,'kama wao ngangari basi sisi ni ngunguri'
 
Back
Top Bottom