Legacy ya Magufuli ni kutengeneza mifumo imara ya kudhibiti Ufisadi na rushwa.

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,925
41,499
Baada ya Magufuli kuingia kama kiongozi wa awamu ya tano; bila shaka na sote ni mashahidi kuwa ameleta changamoto kubwa sana katika public sector na Taifa zima kwa ujumla.

Nchi yetu ilikua ikiugua magonjwa mabaya ya wizi, ubadhirifu, rushwa, uvivu, kukosekana kwa uzalendo na mengine mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekua kikwazo cha maendeleo yetu kama Taifa.

Changamoto alizoleta Magufuli zimetokana na suluhisho la haraka kupitia tumbua tumbua.

Aina hii ya suluhisho ilisaidia kupunguza uvivu kwa watumishi wa uma, wizi, ubadhirifu na rushwa.

Kwa kiasi cha kuridhisha tu sasa idara za serikali zinaelekea kupona.

kiini cha andiko hili kinatokana na semi maarufu katika jamii yetu inayofahamika kama " mjasiri haachi asili" semi hii ni kama angalizo na kauli chochezi kwa mheshimiwa Magufuli ili achukue hatua haraka.

Katika pita pita yangu huko mtaani; maneno yaliyopo ni kuwa " tunavumilia miaka yake kumi iishe, then business as usual".

kauli hii ya wengi inamaanisha kwamba tabia za hapo awali kabla ya awamu hii, zinawavutia wengi na zimeshakua tamaduni za wengi.

wengi wanasubiri awamu hii ipite ili waendelee kutuibia kama kawaida yao.

mtu yoyote mwenye nia njema na Taifa lake hatopenda kuona hali ya sasa inafikia kikomo na hali ya zamani inarudi kwa kasi baada ya muda.

Njia pekee ya kuona kuwa haturudi tulikotoka ni kwa kutengeneza mifumo imara ambayo itakuwa inajisimamia yenyewe kwa kuwaadabisha wote wanao kwenda kinyume; na njia sahihi ya kufanya hivyo ni kupitia sheria.

Kuna haja ya kufuta baadhi ya sheria zinazotengeneza mianya ya ubadhirifu na kutunga ama kuongeza mpya zitakazohakikisha kuwa nchi inajiendesha yenyewe.

Kwa kua tumepata kiongozi mwenye maono mazuri nafikiri sasa ni wakati muafaka wa kufanya hivyo.
 
Niliwahi kuandika uzi huu siku si nyingi!
Bila shaka mh JPM amethubutu katika kushughulikia changamoto za ufisadi japo kuna "lose ends" nyingi!Tunakubaliana wote kuwa siku moja JPM hatakuwa Rais,na hii inaweza tokana na sababu kuu 4:
1.Kutochaguliwa 2020
2.Kukaa kando ya ulingo kikatiba 2025
3.Maradho\kifo(Mungu epushia mbali)
4.Nyinginezo kama kujiuzulu nk

Je,utapenda kuona yale uliyopambana nayo yakirejea???
Utawala huu wa JPM umenifunza kuwa katika nchi yetu,mambo makubwa na nyeti yanategemea maamuzi ya Rais au watu wanavyomtafsiri!Ndio maana pamoja na kashfa zote zilizowahi kutokea huko nyuma ilikuwa ni kama mambo ya kawaida tu!Ilifika kipindi mpaka nchi za watu wanatusaidia kuona kuwa tunaibiwa,refer sakata la radar!Lakini ndio kwanza sisi tulikuwa tunavuta shuka,mpaka wanaturudishia chenji wala hatuna habari!
Kuna guarantee gani kwamba hatutarejea huko?Umechukua hatua gani ili basi hata Rais anapokuwa dhaifu basi nchi hailipi gharama kwa udhaifu wake?Je,kuna mfumo unafikiria kuuweka ili basi hata Rais anaposema "pesa sio za umma" isiwe end of the story???
Au unataka upate credit tu kwa kipindi chako ,the rest tutajijua mbele ya safari?
Nakusihi sana uunde mfumo ambao hautarely sehemu moja katika kuresolve national issues
 
Sasa hiki si ndio kile ambacho kila siku unabisha na watu humu JF au kwa sababu wewe umesema?

Kila siku humu siunaambiwa kama kweli kuna uthubutu basi katiba ibadirishwe na baadhi ya sheria zibadirishwe ili kuwe na mfumo utaodumu kwa karne nyingi na utakaolinda maslahi ya taifa dhidi ya genge la wanyanga'nyi ambao CCM ndio pango lao..
 
Baada ya Magufuli kuingia kama kiongozi wa awamu ya tano; bila shaka na sote ni mashahidi kuwa ameleta changamoto kubwa sana katika public sector na Taifa zima kwa ujumla.

Nchi yetu ilikua ikiugua magonjwa mabaya ya wizi, ubadhirifu, rushwa, uvivu, kukosekana kwa uzalendo na mengine mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekua kikwazo cha maendeleo yetu kama Taifa.

Changamoto alizoleta Magufuli zimetokana na suluhisho la haraka kupitia tumbua tumbua.

Aina hii ya suluhisho ilisaidia kupunguza uvivu kwa watumishi wa uma, wizi, ubadhirifu na rushwa.

Kwa kiasi cha kuridhisha tu sasa idara za serikali zinaelekea kupona.

kiini cha andiko hili kinatokana na semi maarufu katika jamii yetu inayofahamika kama " mjasiri haachi asili" semi hii ni kama angalizo na kauli chochezi kwa mheshimiwa Magufuli ili achukue hatua haraka.

Katika pita pita yangu huko mtaani; maneno yaliyopo ni kuwa " tunavumilia miaka yake kumi iishe, then business as usual".

kauli hii ya wengi inamaanisha kwamba tabia za hapo awali kabla ya awamu hii, zinawavutia wengi na zimeshakua tamaduni za wengi.

wengi wanasubiri awamu hii ipite ili waendelee kutuibia kama kawaida yao.

mtu yoyote mwenye nia njema na Taifa lake hatopenda kuona hali ya sasa inafikia kikomo na hali ya zamani inarudi kwa kasi baada ya muda.

Njia pekee ya kuona kuwa haturudi tulikotoka ni kwa kutengeneza mifumo imara ambayo itakuwa inajisimamia yenyewe kwa kuwaadabisha wote wanao kwenda kinyume; na njia sahihi ya kufanya hivyo ni kupitia sheria.

Kuna haja ya kufuta baadhi ya sheria zinazotengeneza mianya ya ubadhirifu na kutunga ama kuongeza mpya zitakazohakikisha kuwa nchi inajiendesha yenyewe.

Kwa kua tumepata kiongozi mwenye maono mazuri nafikiri sasa ni wakati muafaka wa kufanya hivyo.
Kwani waliyoiweka ni wakina nani na wapo wapi kwa sasa? Na je wakati wanaiweka Magufuli alikuwa wapi na anafanya nini?
 
Niliwahi kuandika uzi huu siku si nyingi!
Bila shaka mh JPM amethubutu katika kushughulikia changamoto za ufisadi japo kuna "lose ends" nyingi!Tunakubaliana wote kuwa siku moja JPM hatakuwa Rais,na hii inaweza tokana na sababu kuu 4:
1.Kutochaguliwa 2020
2.Kukaa kando ya ulingo kikatiba 2025
3.Maradho\kifo(Mungu epushia mbali)
4.Nyinginezo kama kujiuzulu nk

Je,utapenda kuona yale uliyopambana nayo yakirejea???
Utawala huu wa JPM umenifunza kuwa katika nchi yetu,mambo makubwa na nyeti yanategemea maamuzi ya Rais au watu wanavyomtafsiri!Ndio maana pamoja na kashfa zote zilizowahi kutokea huko nyuma ilikuwa ni kama mambo ya kawaida tu!Ilifika kipindi mpaka nchi za watu wanatusaidia kuona kuwa tunaibiwa,refer sakata la radar!Lakini ndio kwanza sisi tulikuwa tunavuta shuka,mpaka wanaturudishia chenji wala hatuna habari!
Kuna guarantee gani kwamba hatutarejea huko?Umechukua hatua gani ili basi hata Rais anapokuwa dhaifu basi nchi hailipi gharama kwa udhaifu wake?Je,kuna mfumo unafikiria kuuweka ili basi hata Rais anaposema "pesa sio za umma" isiwe end of the story???
Au unataka upate credit tu kwa kipindi chako ,the rest tutajijua mbele ya safari?
Nakusihi sana uunde mfumo ambao hautarely sehemu moja katika kuresolve national issues

Humu JF kungekuwa na watu 10 tu kama wewe na nchi ya Tanzania ingekuwa na watu kama wewe 50 mambo yangeenda sawa na maendeleo yangeonekana

Ila nchi imejaa wajinga kila kona
 
Baada ya Magufuli kuingia kama kiongozi wa awamu ya tano; bila shaka na sote ni mashahidi kuwa ameleta changamoto kubwa sana katika public sector na Taifa zima kwa ujumla.

Nchi yetu ilikua ikiugua magonjwa mabaya ya wizi, ubadhirifu, rushwa, uvivu, kukosekana kwa uzalendo na mengine mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekua kikwazo cha maendeleo yetu kama Taifa.

Changamoto alizoleta Magufuli zimetokana na suluhisho la haraka kupitia tumbua tumbua.

Aina hii ya suluhisho ilisaidia kupunguza uvivu kwa watumishi wa uma, wizi, ubadhirifu na rushwa.

Kwa kiasi cha kuridhisha tu sasa idara za serikali zinaelekea kupona.

kiini cha andiko hili kinatokana na semi maarufu katika jamii yetu inayofahamika kama " mjasiri haachi asili" semi hii ni kama angalizo na kauli chochezi kwa mheshimiwa Magufuli ili achukue hatua haraka.

Katika pita pita yangu huko mtaani; maneno yaliyopo ni kuwa " tunavumilia miaka yake kumi iishe, then business as usual".

kauli hii ya wengi inamaanisha kwamba tabia za hapo awali kabla ya awamu hii, zinawavutia wengi na zimeshakua tamaduni za wengi.

wengi wanasubiri awamu hii ipite ili waendelee kutuibia kama kawaida yao.

mtu yoyote mwenye nia njema na Taifa lake hatopenda kuona hali ya sasa inafikia kikomo na hali ya zamani inarudi kwa kasi baada ya muda.

Njia pekee ya kuona kuwa haturudi tulikotoka ni kwa kutengeneza mifumo imara ambayo itakuwa inajisimamia yenyewe kwa kuwaadabisha wote wanao kwenda kinyume; na njia sahihi ya kufanya hivyo ni kupitia sheria.

Kuna haja ya kufuta baadhi ya sheria zinazotengeneza mianya ya ubadhirifu na kutunga ama kuongeza mpya zitakazohakikisha kuwa nchi inajiendesha yenyewe.

Kwa kua tumepata kiongozi mwenye maono mazuri nafikiri sasa ni wakati muafaka wa kufanya hivyo.

Kwani aliyesababisha yote hayo yuko wapi au wako wapi??

Na kama yupo kwanini wasifikishwe kwenye vyombo vya kisheria

Mpaka sasa kila kitu ni zero hakuna kilichofanyika
 
Sasa
Kwani waliyoiweka ni wakina nani na wapo wapi kwa sasa? Na je wakati wanaiweka Magufuli alikuwa wapi na anafanya nini?
Sasa ulitaka ajiuzulu kwa sababu hakubaliani nao? Sasa tungempatia wapi!!! Kuwa raisi
 
Huwezi kujenga mfumo imara kwa maneno tu ya rais au kwa kuzuia upinzani kufanya siasa, na ndio maana sisi wengine tunaona anachofanya ni blah blah tu, sababu hagusi vitu vilivyopelekea hayo yatokee.
 
Baada ya Magufuli kuingia kama kiongozi wa awamu ya tano; bila shaka na sote ni mashahidi kuwa ameleta changamoto kubwa sana katika public sector na Taifa zima kwa ujumla.

Nchi yetu ilikua ikiugua magonjwa mabaya ya wizi, ubadhirifu, rushwa, uvivu, kukosekana kwa uzalendo na mengine mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekua kikwazo cha maendeleo yetu kama Taifa.

Changamoto alizoleta Magufuli zimetokana na suluhisho la haraka kupitia tumbua tumbua.

Aina hii ya suluhisho ilisaidia kupunguza uvivu kwa watumishi wa uma, wizi, ubadhirifu na rushwa.

Kwa kiasi cha kuridhisha tu sasa idara za serikali zinaelekea kupona.

kiini cha andiko hili kinatokana na semi maarufu katika jamii yetu inayofahamika kama " mjasiri haachi asili" semi hii ni kama angalizo na kauli chochezi kwa mheshimiwa Magufuli ili achukue hatua haraka.

Katika pita pita yangu huko mtaani; maneno yaliyopo ni kuwa " tunavumilia miaka yake kumi iishe, then business as usual".

kauli hii ya wengi inamaanisha kwamba tabia za hapo awali kabla ya awamu hii, zinawavutia wengi na zimeshakua tamaduni za wengi.

wengi wanasubiri awamu hii ipite ili waendelee kutuibia kama kawaida yao.

mtu yoyote mwenye nia njema na Taifa lake hatopenda kuona hali ya sasa inafikia kikomo na hali ya zamani inarudi kwa kasi baada ya muda.

Njia pekee ya kuona kuwa haturudi tulikotoka ni kwa kutengeneza mifumo imara ambayo itakuwa inajisimamia yenyewe kwa kuwaadabisha wote wanao kwenda kinyume; na njia sahihi ya kufanya hivyo ni kupitia sheria.

Kuna haja ya kufuta baadhi ya sheria zinazotengeneza mianya ya ubadhirifu na kutunga ama kuongeza mpya zitakazohakikisha kuwa nchi inajiendesha yenyewe.

Kwa kua tumepata kiongozi mwenye maono mazuri nafikiri sasa ni wakati muafaka wa kufanya hivyo.

Work done is equal to 0 / bashite
 
Sasa

Sasa ulitaka ajiuzulu kwa sababu hakubaliani nao? Sasa tungempatia wapi!!! Kuwa raisi
Kwahiyo unamaanisha ilibidi akubaliane na ufisadi na wizi ili apate Urais?
Definitely na wezi au mafisadi atakuwa anawajua si ndio?
 
Bila katiba ya Warioba haya anayoyafanya Pombe ni kazi bure akisepa madarakani atakaekuja anakuja na lake ataendeleza dili na sie wengine tutazipiga hizo dili kama kawaida
 
Legacy yake ni kuteka taasisi ili aonekane yeye as an individual.

Ni hasara kubwa sana kwa taifa.

Zaidi ya mahakama ya mafisadi kila kitu kilikuwepo. Tathmini ya mahakama hii itakuja akimaliza muda wake.
 
Kwani amepatikana kupitia wapi? Na huo ufisadi/wizi upo wapi?
Ndo anaushghulikia na hii inamaanisha hakuwa anakubaliana nao Ila hakukuwa na jinsi. Onyo upinzani msiweke mgombea 2020 mana atapata alimia 20 tu. Jpm atakuwa umeshamaliza wizi wote serikalin na maendeleo makubwa mnl
 
Kwahiyo unamaanisha ilibidi akubaliane na ufisadi na wizi ili apate Urais?
Definitely na wezi au mafisadi atakuwa anawajua si ndio?
Ndo maana anasisitiza kuwa wezi wote anawajua hivyo kuwa ndani UA serikali corrupt ilimsaidi na inamsaidia ngoja asafishe kila kona
 
Funny, yaani fisadi na mla rushwa anasemwa kwamba anapambana na ufisadi na rushwa? Je, keshatubu juu ya ufisadi wake? Je, ameshachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria? Kama bado, hakika anachofanya ni kejeli na usanii! Hakuna mpinga rushwa na ufisadi hapo!
[HASHTAG]#magufuliisaphony[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom