Leave them to us will teach them a lesson"

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Kutokana na hali ya siasa inavyokwenda sasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kweli hii sasa ni "cancer" ambayo balozi Seif Iddi kwa upana wake ameielezea kuwa ni lazima ikatwe kama bado tunapenda kuendelea kuishi, lakini balozi alisahau kuwa "cancer" imo katika Chama chake na Serikali zake, kwasababu haingii akilini kuwa sasa Serikali za CCM zimejionesha wazi kuwa zimo kwenye juhudi kubwa ya kuvunja kabisa upinzani na kuua demokrasia nchini sina haja ya kutoa mifano kwasababu iko mingi na kila mtu anaona na anajua kinachotendeka sasa.
Tanzania iliingia rasmi katika mfumo wa vyama vingi 1992 na kwa hakika serikali za CCM hazikukubali mfumo huo bali Mwalimu Nyerere kwa kujua kitachotokea mbele yetu akalazimisha mfumo wa vyama vingi na akawaambia kuwa vyama vingi vinakuja wanachama wa vyama hivyo hawatotoka Mbinguni ila ni hawa hawa wananchi waliopo kwa hivyo akawatahadharisha CCM kuwa wajidhatiti kuongoza nchi vizuri ili watu waridhike na uongozi wao na waendelee kukiunga mkono Chama Chao.
Kinyume chake baada ya kufa Mwalimu CCM walivuruga zaidi mfumo Chama wakakikabidhi matajiri wanyonge na masikini wakakihama Chama na kujiunga na vyama vya upinzani. Wakati huo kukawa na NCCR Mageuzi na CUF.
Baada ya kuona wimbi kubwa sana linakihama Chama Chao CCM wakaanza kupata kiwewe na kubuni njia mbadala kuweza kuwarejesha wanachama ili waendelee kuunga mkono CCM lakini juhudi hizo zilivogonga mwamba hasa katika uchaguzi wa 2015 ambapo CCM walipoteza mwelekeo Tanganyika na Zanzibar na ingelikuwa si kutumia nguvu na ubabe wa watu wa Ulinzi na Usalama basi leo tungelikuwa tunazungumza mengine hapa Tanganyika.
Kwa upande wa Zanzibar nguvu ya vikosi vya ulinzi na Usalama ilishindwa na nguvu ya umma na hawakuwa na chaguo lingine ila kwa kutumia akili yao ya mwisho ni kutumia amri ya kufuta uchaguzi na uchaguzi ukafutwa baadae kajatayarishwa uchaguzi mwengine mpya 2016 ambapo CCM ilishindwa kwa asilimia mia. Sasa hio ndio "cancer" iliyowapata Tanzania kwa sasa na hakuna njia nyengine ila ni lazima ikatwe kabisa kwasababu kwa mionzi haitotibika.
Kuna juhudi kubwa sana zimefanyika na zinaendelea kufanyika ili "cancer" hii iondoke imejaribiwa mionzi haikuondoka, imetumika "chemotherapy" bado sasa njia pekee iliyobaki ni hii ya kukata kabisa na Daktari kasema haya maradhi yameathiri mguu na ziwa kwa hivyo tutakata ziwa na mguu ili isisambae mwilini na hivi ninavokwambia mgonjwa yuko katika chumba cha upasuaji na madaktari wapo tayari na "nurses" wanatayarisha vifaa ili kazi ianze kukinusuru kiiwiliwili (Zanzibar ) kisi athirika.
Katika juhudi hizo za madaktari tayari wajumbe wao wapo hapa kwa mgonjwa kutoka Marekani , EU, UN, The Commonwealth na Liberal Parties International na hawa Liberal waliwahi kusema mwaka jana September 2017 kuwa wao CUF ni mwanachama wao kwa hivyo hawako tayari kuona demokrasi inachezewa bila ya kufata mkondo wake nitanukuu kidogo kipande cha maneno waliyotamka hao liberals mwaka jana kilisema hivi nanunua. " As the head of the Liberal Party International I would like to have the highest leadership in Tanzania on the side of the ruling party to ensure that the issue of the agreement is properly managed and timely to do so is to put faith in the principles of justice and equity in response to the option. Many believe that justice will take place" by Nick Gainer. The President of Liber Party. 18/09/1917.
Sasa Abdalla Juma Mabody katika Moja ya hotuba zake alisema kuwaambia CUF kuwa ^Ukiujua huu sisi tunajua huu" hapa ni "challenge" kwa Tanganyika kukubali cancer " iwachwe hivi hivi isambae mwili mzima au kumuachia hutu mtoto wake (ZANZIBAR ) akatwe mguu na ziwa kunusuru kiwiliwili. Hapa Maalim Seif na CUF hawana tena maneno ila ni kutii maneno ya wafadhili wakuu wanatufadhili walipoiambia CUF kuwa "Leave them will teach them a lesson "
 
Mungu wabariki Wazungu,Mungu mbariki Maalim Seif,shujaa wetu wa Zanzibari
 
Back
Top Bottom