Learn the Law: Nini kilitangulia kati ya makosa na sheria

The Alchemist

Senior Member
Jun 15, 2016
177
148
Wakati mwenye shida na uhitaji akiniuliza maswali mbalimbali ya ufahamu wa sheria ningependa tujadili;

1) Kati ya sheria na makosa, ni kipi kilitangulia?

2)Unadhani Tanzania sheria kuna heshima ya sheria?

3) Legitimacy ya sheria inatoka wapi?
 
3) Legitimacy ya sheria inatoka

Wakati mwenye shida na uhitaji akiniuliza maswali mbalimbali ya ufahamu wa sheria ningependa tujadili;

1) Kati ya sheria na makosa, ni kipi kilitangulia?

2)Unadhani Tanzania sheria kuna heshima ya sheria?

3) Legitimacy ya sheria inatoka wapi?
Sheria ndio ilitangulia. Huwezi kubaini au kuadhibu kosa iwapo hakuna sheria.
Hata dhambi, kama sio sheria kusingekuwa na dhambi. Lakini likiwapo katazo au amri basi kosa hutokea kutokana na hiyo.
 
Wakati mwenye shida na uhitaji akiniuliza maswali mbalimbali ya ufahamu wa sheria ningependa tujadili;

1) Kati ya sheria na makosa, ni kipi kilitangulia?

2)Unadhani Tanzania sheria kuna heshima ya sheria?

3) Legitimacy ya sheria inatoka wapi?

1--- Yalitangulia makosa, ndipo sheria na kanuni na miongozo ikaletwa na Mungu kupitia manabii wake ili ituongoze.

2---- Swali no 2 sijalielewa vyema, lakini nitajaribu; Tz wapo watu wanaoheshimu sheria na wapo watu wanaovunja sheria na ndio maana kuna vyombo vya kushughulika na mambo hayo mfano Polisi, mahakama, magereza, Waziri wa sheria nk.

3---- Legitimacy ya sheria kimsingi imetokea katika religious doctrines and Sacred books of God. Uhalali wa sheria zote zinazo govern human lives duniani pote msingi wake ni kutoka kwa Mungu, hata ukiangalia zile sheria za "International declarations of human rights"---- they, to a great extent, comply with Quranic laws.
 
1. Note: Hapatakuwa na kosa(uvunjifu wa sheria) endapo sheria haijakataza hilo jambo.(Utatambua vipi mtu amefanya kosa endapo hakuna utaratibu au sheria inayotoa muongozo kuwa mambo yafanyike hivi na Sio tofauti na hapo).

Hii kusema lazima sheria iwepo ili kuwepo na uvunjifu wa sheria(makosa).

Japo kuwa, Hali ya Maisha, mabadiliko ya teknolojia na Mazingira pia kwa ujumla hupelekea kufanya mabadiliko ya sheria either kupunguza,kuongeza au kuboresha sheria fulani.

2. Mambo ya heshima ya sheria kama ulivyouliza. Hii task nakupa mwenyewe tena, angalia vitu vifuatavyo endapo hujaviona bado.
1.Abusive of power.
2.Assumption of powers
3. Kujaa kwa kesi mahakamani.
4. Uwepo wahalifu mtaani na wafungwa jela .
N.k
 
Kwanza embu tafakari muasisi wa sheria wa kwanza ambaye ni Mungu mwenyewe alifanyaje. Dhambi ilianza ndio zikaja amri au amri ndio zilitangulia?
 
maswali mawili yamejibiwa vizuri sina cha kuongezea ila la mwisho uhalali wa sheria ni haki(justice
kama sheria itafata haki(justice) sheria hiyo ni halali
kama sheria haitofata haki(justice) sheria hiyo siyo halali
 
Social Contract Theory
Nitakujibu swali lako kupitia hii theory ipa itafute uisome maana nitailezea partially...ila itakusaidia kujibu maswali yako.

Hapo zamani binadamu aliishi anavyotaka yeye (Free will)...Mtu angeweza kumuua yeyote bila kuulizwa na mwingine ( Maisha yalikua ni ya kikatili sana ) ...Mali hazikua salama sababu mwenye nguvu angeweza kuchukua mali ya mnyonge na asimfanye nk....kifupi binadamu aliishi katika uhuru wake wa asili (Natural freedom) kama waishivyo wanyama wengine tu porini....lakini baada ya madhira ya muda mrefu,binadamu kama viumbe wenye akili waliona umuhimu kujadiliana kuhusu ku Surrender their natural freedom...as zinaleta madhara makubwa kwenye society wakakubaliana kufanya hivyo na hii ndiyo "Social Contract" yenyewe.

Tatizo likaja...je itakuwaje kama mtu akiamua kukiuka utaratibu tuliojiwekea? Na hapo ndipo zilpokuja sheria kwa mtu atakaye kiuka utaratibu walojiwekea binadamu.

Likaja tatizo jingine,je ni nani atazisimamia hizo sheria? Na hapo ndipo utawala ulipoanzishwa ...yaani alipatikana kiongozi(King/Queen) ili kusimamia hizi sheria...
Nadhani kufikia hapo umeelewa kipi kilianza kati ya sheria na makosa...kifupi hakuna kosa bila sheria...though kwenye issue za human rights kesi ni tofauti...huku kosa linakuwepo hata kama sheria haipo...Thanx
 
Labda nikuulize, unaweza kuwa na sheria inayokataza au kusimamia jambo ambalo halipo?

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Kwenye sheria zetu,je unaweza kuadhibiwa kwa kosa ulilotenda kabla ya sheria hiyo kutungwa? jibu ni hapana.

Mfumo unakua...Tatizo linabainika(bado si kosa)...Sheria inafuata...then ukikiuka sheria iliyotungwa kudhibiti tatizo hilo ni kosa.
 
Social Contract Theory
Nitakujibu swali lako kupitia hii theory ipa itafute uisome maana nitailezea partially...ila itakusaidia kujibu maswali yako.

Hapo zamani binadamu aliishi anavyotaka yeye (Free will)...Mtu angeweza kumuua yeyote bila kuulizwa na mwingine ( Maisha yalikua ni ya kikatili sana ) ...Mali hazikua salama sababu mwenye nguvu angeweza kuchukua mali ya mnyonge na asimfanye nk....kifupi binadamu aliishi katika uhuru wake wa asili (Natural freedom) kama waishivyo wanyama wengine tu porini....lakini baada ya madhira ya muda mrefu,binadamu kama viumbe wenye akili waliona umuhimu kujadiliana kuhusu ku Surrender their natural freedom...as zinaleta madhara makubwa kwenye society wakakubaliana kufanya hivyo na hii ndiyo "Social Contract" yenyewe.

Tatizo likaja...je itakuwaje kama mtu akiamua kukiuka utaratibu tuliojiwekea? Na hapo ndipo zilpokuja sheria kwa mtu atakaye kiuka utaratibu walojiwekea binadamu.

Likaja tatizo jingine,je ni nani atazisimamia hizo sheria? Na hapo ndipo utawala ulipoanzishwa ...yaani alipatikana kiongozi(King/Queen) ili kusimamia hizi sheria...
Nadhani kufikia hapo umeelewa kipi kilianza kati ya sheria na makosa...kifupi hakuna kosa bila sheria...though kwenye issue za human rights kesi ni tofauti...huku kosa linakuwepo hata kama sheria haipo...Thanx
Hii hoja yako haiko vizuri kisheria na hata kimantiki. Umetumia social contract ( tena kwa upande mmoja) ukielezea ni kipi kati ya sheria na kosa kinachomtangulia mwenzake. Kumbuka social contract ni ya karne ya ya 16 na 17 hapo. Ila kumbuka kumekuwepo na sheria tena kali kabisa kabla ya hiki kipindi cha enlightenment ambapo social contract ndipo ilipotokea. Kuna sheria kama Twelve Tables law ya Roma na Code of Hammurabi ya Babylon (mojawapo ya sheria kali kuwahi kuwepo), hizi unazieleza vipi katika muktadha wa social contract ambayo ilikuja baadae??
Huwa tunajifunza kuwa lengo ni kurekebisha tabia na mienendo katika jamii. Kwa municipal laws, makosa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha sheria kutungwa au kufanyiwa marekebisho.
 
Wakati mwenye shida na uhitaji akiniuliza maswali mbalimbali ya ufahamu wa sheria ningependa tujadili;

1) Kati ya sheria na makosa, ni kipi kilitangulia?

2)Unadhani Tanzania sheria kuna heshima ya sheria?

3) Legitimacy ya sheria inatoka wapi?
1. Makosa - Mastery of observation
2. Sheria - Mastery of self
 
Hii hoja yako haiko vizuri kisheria na hata kimantiki. Umetumia social contract ( tena kwa upande mmoja) ukielezea ni kipi kati ya sheria na kosa kinachomtangulia mwenzake. Kumbuka social contract ni ya karne ya ya 16 na 17 hapo. Ila kumbuka kumekuwepo na sheria tena kali kabisa kabla ya hiki kipindi cha enlightenment ambapo social contract ndipo ilipotokea. Kuna sheria kama Twelve Tables law ya Roma na Code of Hammurabi ya Babylon (mojawapo ya sheria kali kuwahi kuwepo), hizi unazieleza vipi katika muktadha wa social contract ambayo ilikuja baadae??
Huwa tunajifunza kuwa lengo ni kurekebisha tabia na mienendo katika jamii. Kwa municipal laws, makosa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha sheria kutungwa au kufanyiwa marekebisho.
Sijajua umeangalia kwa muktadha upi? anyway,achana na hiyo theory,unajua kama kabla ya sheria hakuna kosa?

Unaweza kushitakiwa kwa sheria isiyo exist?

Unaweza shitakiwa kwa kula mirungi kenya?

Kabla ya kutungwa sheria Tanzania kutumia Kuber ilikua ni kosa?,na baada ya kutungwa sheria ni kosa au si kosa?
 
Na unaweza kuwa na sheria ambayo makosa yaliyopo hayapo katika jamii husika?
 
Aisee mbona mgumu kuelewa sana?
Offense ni kubreak the law iliyowekwa kwenye society husika....hakuwezi kuwa na offense kama hakuna sheria kwani ni mpaka uvunje hiyo sheria ndo unakuwa umefanya kosa...hicho unachotaka kukielezea hapo kabla ya sheria siyo kosa kuna jina lake,jus do your homework.
Pia unaweza kuwa na sheria hata kama kosa halifanyiki kwenye jamii husika,ili kuzuia lisifike kabisa kutokana na hatari ya kosa hilo kama likifika kwenye jamii husika.
 
Wewe bado unahitajika kuiva vizuri kwenye jurisprudence ya sheria.
 
Back
Top Bottom