Learn From History: Kama Waziri Huyu Alitunga Uongo Huu, Kuwa Waandishi Wametishia Kumuua!, Then..

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,464
113,537
Wanabodi,

Declaration of interest: Mimi ni mpenzi wa somo la historia, ambalo ni somo la mambo ya zamani, kuwianisha na mambo ya sasa, ili kujua mambo yajayo. Hivyo kila nipatapo fursa, hupekua kwenye historia ya mambo ya zamani na kulinganisha ni hiki kinachoendelea sasa, ili kujua nini kitakachokuja kutokea siku za baadae.

Leo nimekikumbuka kisa cha waandishi fulani wawili wa habari, ambao walishitakiwa kituo cha polisi Mabatini kwa kosa la kutishia kumuua, waziri fulani.

Kisa chenyewe ni kwa waziri huyo, baada ya kuandikwa vibaya na gazeti hilo, aliamua kubuni kesi ya kizushi, kwa kutunga uongo kuwa waandishi hao wa habari, wamemtishia maisha kuwa watamuua!, akaenda kuripoti uongo huo kituo cha polisi cha Mabatini ili kuwakomoa waandishi hao washughulikiwe!, na kweli waandishi wale walishughulikiwa kwa kuitwa polisi na kuhojiwa, kisha kuachiwa kwa dhamana kusubiria muendelezo wa hiyo kesi.

Kilichofuata Waziri hakurudi tena kituoni kuthibitisha madai yake, kwa vile yalikuwa ni madai ya uongo!, hivyo kesi ikafa natural death. Thanks God Watanzania ni watu wema, hutunza kumbukumbu ya mema tuu huku wakiwa wapesi wa kusameme na kusahau mabaya yote ya nyuma. Hata hili bandiko sio la kukumbushana mabaya, no harm intended, just to keep history alive.

Sasa kama tuhuma hii ni kweli, mtu anaweza kumzushia binadamu mwenzake tuhuma nzito kama hii, then this leaves much to be desired in the present situation and in future!. Mkumbuke, binadamu anaweza kubadili tuu tabia, lakini hulka huwa haibadiliki, anaweza tuu kuificha, lakini siku ya siku hulka huibuka!.

Soma mkasa wa kifisadi na kitapeli uliowahi kufanywa Waziri fulani kama unavyosimuliwa na mwandishi wa Raia Mwema:
Kitu ambacho pengine sikukieleza katika makala hiyo ni kwamba waziri mmoja naye amepata kuandamwa na kashfa ya ufisadi. Kwa hiyo, si kweli kwamba yeye ni mwadilifu kwa asilimia 100!
Labda nitoe mfano mmoja tu ninaoukumbuka kwa haraka unaohusu namna alivyosimamia kifisadi zoezi lile la uuzwaji wa nyumba za serikali lililoasisiwa na utawala wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Mwaka 2006 gazeti la Rai liliwahi kuandika habari kadhaa za uchunguzi kuhusu namna waziri huyo alivyomuuzia ndugu yake na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];kidosho' wake mmoja nyumba mbili za NHC zilizokuwepo Ubungo ilhali wawili hao hawakuwa wafanyakazi wa serikali au NHC. Tena waliuziwa kwa bei poa.
Nakumbuka ya kwamba baada ya habari ya kwanza kuchapishwa, waziri alisihi tusiendelee kuandika habari hiyo, lakini ushawishi wake uliposhindikana alifanya jambo la kipuuzi ambalo mpaka leo tunalikumbuka sisi tuliokuwa Habari Corporation na sasa Raia Mwema.
Jambo lenyewe la kipuuzi ni kwamba waziri huyo aliamua kwenda kituo kidogo cha Polisi cha Mabatini kilichopo Kijitonyama, Dar es Salaam na kufungua madai ya uongo kwamba eti alikuwa anatishiwa kuuawa na wahariri wa gazeti la Rai.
Kwa sababu ya madai hayo ya uongo, aliyekuwa Mhariri Mtendaji, John Bwire na mhariri wa gazeti hilo ambaye ndiye aliyekuwa akiandikia habari hizo za uchunguzi, Muhingo Rweyemamu, wakafikishwa katika kituo hicho cha polisi kwa tuhuma nzito za kutaka kumuua waziri huyo!
Nakumbuka ya kwamba siku hiyo ilikuwa ni Ijumaa (mchana) na ilikuwa ni mpango wa waziri huyo kuwakomoa wawekwe ndani wikiendi nzima hadi Jumatatu! Hata hivyo, polisi wa kile kituo walipofahamu kwamba chanzo ni skandali hiyo ya waziri iliyokuwa ikiandikwa na gazeti la Rai, wakayapuuza madai hayo ya waziri, na hivyo kuwaruhusu wahariri hao kujidhamini wenyewe.
Madai hayo ya hatari yalikuja kufa baadaye kifo cha asili baada ya waziri mwenyewe kutolifuatilia tena suala hilo kwenye kituo hicho cha Polisi. Mpaka leo tukilikumbuka tukio hilo huwa tunacheka; maana kote duniani ni waandishi wa habari ndio wanaotolewa roho na wanasiasa na watawala, na wala si watawala ndiyo wanaotolewa roho na waandishi!
Kwa hiyo, hata waziri huyo si msafi kihivyo. Tukio hilo la mwaka 2006 ninalolizungumzia si la uzushi au kutunga. Bahati nzuri nakala za magazeti hayo ya Rai yaliyoandika kuhusu ufisadi wake huo bado zipo kule New Habari Corporation.
Na bahati nzuri pia ni kwamba wahariri hao wawili bado wapo hai &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; waulizwe kama mimi ninayeandika haya ninadanganya. Kwa sasa, John Bwire ni mkurugenzi mwenzangu katika gazeti hili la Raia Mwema na Muhingo Rweyemamu ni Mkuu wa Wilaya ya Makete &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; waulizwe.


- See more at: Raia Mwema - Soma Kisa na Mkasa cha Waandishi Walioshitakiwa kwa Kutishia Kumuua Waziri Fulani?

NB. Hili ni bandiko la ma GT, hivyo naombeni sana tusitaje taje majina.
Angalizo: Kwa wasio fahamu essence ya somo la Historia, naombeni sana, mjipitie tuu kwenye uzi huu na kujiendelea zenu na safari zenu, pia naomba nisiulizwe jambo lolote kuhusu mkasa huu kwa sababu jukumu langu ni kuwaletea historia tuu.

Kitendo cha kuripoti kitu cha uongo kwenye kituo cha polisi ni kosa la jinai, na makosa ya jinai, hayana time limitation, hivyo kesi hiyo ya kuripoti uongo kwenye kituo cha polisi, ingekuwa ni nchi nyingine za watu ma mainder, kesi hiyo ingeweza kuibuliwa at the most oportune time na kuitumia kama msingi wa pingamizi, thanks to Watanzania kwa upendo wa agape miongoni mwetu.

Hivyo tujifunze kutoka historia, Kama Waziri Huyu Aliweza Kutunga Uongo Huu, Kuwa Waandishi Wametishia Kumuua!, Then...

Paskali
Update.
Kama nilivyoomba mimi nisiulizwe chochote maana sikuwepo, bahati nzuri kumejitokeza members waliokuwepo na waliojua nini kilikuwa kinaendelea.

Kumbe zilikuwa ni siasa!. Sio vibaya mkimsoma member huyu kwa ufafanuzi.
Paskali unatakiwa kuwa mkweli maana historia ni Mwalimu. Usipotoshe! Huwezi kuleta hadithi (news story) husika bila kuainisha mukhtadha wa kisiasa uliokuwepo mwaka 2006. Ulitakiwa kusema pia, kuwa huyo waziri unayemsema kuwatishia waandishi alikuwa akiwindwa na 'wana-mtandao' wa waliokuwa wamemwingiza Kikwete madarakani lakini wakakosa vyeo. Cheo cha uwaziri alichokuwa amepewa waziri huyo kilitakiwa kutolewa kwa mtu mwingine miongoni mwa wanamtandao. Hiyo ndio iliyokuwa vita yenyewe. Kila silaha ilitafutwa na kutumika kuhakikisha waziri huyo anaondolewa katika baraza la mawaziri kwa kuwa hakuwa mwana-mtandao. Gazeti la Rai lilikuwa tayari limetekwa na kutumiwa na wana-mtandao katika vita hiyo. Tunafahamu kuwa hata wakati Jakaya Kikwete akitangaza baraza lake la mawaziri, Novemba 2005, jina la waziri huyo halikuwa kwenye orodha ya awali aliyokuwa ame-share kabla na waziri mkuu Lowasa, bali Rais Kikwete 'alilisoma' jina la waziri huyo kutoka kichwani mwake! Halikuwa kwenye karatasi! Waziri Mkuu Lowasa, wakati huo, ndiye aliyekuwa hataki waziri huyo awepo kwenye baraza la mawaziri akihofia, pamoja na sababu nyingine, kuwa overshadowed na kasi ya utendaji wa waziri huyo. Na kwa ajili ya kuweka kumbu kumb sawa, hebu tuangalie matukio yaliyotokea mara baada ya uchaguzi Mkuu 2005:-
  1. Habari Corporation ilikufa kutokana na ugomvi baina ya wakurugenzi wake [wana-mtandao] dhidi ya majority shareholder (Twaha Khalifani) na kisha kampuni hiyo kununuliwa na kingpin wa wanamtandao wa Kikwete (Rostam Aziz). Twaha hakuwa mwana-mtandao; hakuunga mkono kampeni za Kikwete/alipingana na wana-mtandao. Aliuunga mkono kampenini za Dk. Salim Ahmed Salim.
  2. Irene Bwire-Kakiziba, mke wa John Bwire, mhariri mtendaji wa Rai, alipewa kazi ofisi ya waziri mkuu kuwa miongoni mwa waandishi wa habari wa waziri mkuu.
  3. Salva Rweyemamu, aliyekuwa mkurugenzi Mtendaji wa habari Corporation, alipewa kazi Ikulu ya Rais Kikwete akiwa na cheo cha ukurugenzi wa mawasiliano ya Rais.
  4. Mihingo Rweyemamu alipewa cheo cha Ukuu wa Wilaya (DC). Hiyo ndio vitailiyokuwepo baina ya waziri huyo na wanamtandao.

Sincerely Paskali, please speak the truth. Usipotoshe ukweli.
Mkuu Sophist, asante kwa hii imput.
Kumbe baadhi ya media na wanahabari wenzetu walitumia kalamu zao kisiasa, ila kiukweli ililipa! .

Kwa kumbukumbu zangu za mafundisho tuliyofunzwa chuoni, waandishi tunapaswa kuwa non partisan kwenye politics hatupaswi kuegemea upande wowote. Tunapaswa kuwa kuandika with truthfulness, objectivity, impartiality with fairness and balance kama ambavyo mimi ninafanya.

Paskali
 
Wanabodi,

Declaration of interest: Mimi ni mpenzi wa somo la historia, ambalo ni somo la mambo ya zamani, kuwianisha na mambo ya sasa, ili kujua mambo yajayo. Hivyo kila nipatapo fursa, hupekua kwenye historia ya mambo ya zamani na kulinganisha ni hiki kinachoendelea sasa, ili kujua nini kitakachokuja kutokea siku za baadae.

Leo nimekikumbuka kisa cha waandishi fulani wawili wa habari, ambao walishitakiwa kituo cha polisi Mabatini kwa kosa la kutishia kumuua, waziri fulani.

Kisa chenyewe ni kwa waziri huyo, baada ya kuandikwa vibaya na gazeti hilo, aliamua kubuni kesi ya kizushi, kwa kutunga uongo kuwa waandishi hao wa habari, wamemtishia maisha kuwa watamuua!, akaenda kuripoti uongo huo kituo cha polisi cha Mabatini ili kuwakomoa waandishi hao washughulikiwe!, na kweli waandishi wale walishughulikiwa kwa kuitwa polisi na kuhojiwa, kisha kuachiwa kwa dhamana kusubiria muendelezo wa hiyo kesi. Kilichofuata Waziri hakurudi tena kituoni kuthibitisha madai yake, kwa vile yalikuwa ni madai ya uongo!, hivyo kesi ikafa natural death.

Sasa kama tuhuma hii ni kweli, mtu anaweza kumzushia binadamu mwenzake tuhuma nzito kama hii, then this leaves much to be desired in the present situation and in future!. Mkumbuke, binadamu anaweza kubadili tuu tabia, lakini hulka huwa haibadiliki, anaweza tuu kuificha, lakini siku ya siku hulka huibuka!.



NB. Hili ni bandiko la ma GT, hivyo naombeni sana tusitaje taje majina.
Angalizo: Kwa wasio fahamu essence ya somo la Historia, naombeni sana, mjipitie tuu kwenye uzi huu na kujiendelea zenu na safari zenu, pia naomba nisiulizwe jambo lolote kuhusu mkasa huu kwa sababu jukumu langu ni kuwaletea historia tuu.

Kitendo cha kuripoti kitu cha uongo kwenye kituo cha polisi ni kosa la jinai, na makosa ya jinai, hayana time limitation, hivyo kesi hiyo ya kuripoti uongo kwenye kituo cha polisi, inaweza kuibuliwa wakati wowote na mhusika akapandishwa kizimbani!.

Hivyo tujifunze kutoka historia, Kama Waziri Huyu Aliweza Kutunga Uongo Huu, Kuwa Waandishi Wametishia Kumuua!, Then...

Paskali
Waziri wa ujenzi wakati huo,aliyezaa na Sundi Malomo,,,,,,,Nyakati zimeenda wapi,,,mzee wa Kebbys,,,,,,,Wapi Sizonjeeeee
 
Back
Top Bottom