chuse tbr
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 483
- 545
hata mie Pasco leo kanistua mada nzito sana hii kwa kweli Pasco jiangalie braza zama zimebadilika sanaPaskali kaka yangu naona unajilipua leo! Duuh mimi naiogopa hiii mada.
hata mie Pasco leo kanistua mada nzito sana hii kwa kweli Pasco jiangalie braza zama zimebadilika sanaPaskali kaka yangu naona unajilipua leo! Duuh mimi naiogopa hiii mada.
Kwa mara ya kwanza umemwita mtu wenu Fisadi! Kweli kabla hujafa hujaumbika.Anaweza akawa ni fisadi lakini alitubu....tatizo mafisadi wengine hadi leo hawajawahi kutubu na zaidi yanaendelea na utapeli kwa kuwatapeli watanzania na kuwatetea mafisadi wengine.
Kweli hata mimi nimestuka kweli kweli. Kuna jambo linaendelea na inawezekana "Bwana Njaa" kaamua kujitoa mhanga!Mkuu Pascal embu kwa vitu vingine uwe unatumia ile ID nyingine bhana.....
Hatutaki kumpoteza hata mmoja wetu humu.......
Hali ni tete..pongezi na maandamano ya pongezi kila kona..wew unaleta hizi to the public?
Pls .....
kujua tabia na hulks ya mzalendo wetu. ili kujua dhamira halisi ya anachokifanya.what is the essence of this thread Paskali?
Ukienda mbali zaidi, utaona kuwa pengine hata yule dada adui yake mkubwa mitandaoni yaweza kuwa asilimia kubwa ya yale asemayo kuhusu former minister yaweza kuwa na ukweli.Kinachonitisha ni kwamba huyo former minister ni mnafiki anaeweza kusema uongo mpaka akauapia ili uwe ukweli.... hutumia nguvu sana kujinasibu yu Msafi kumbe fisadi tuuu....
Siku niliyoenda kwao akatuomba tumtolee sadaka mamake ndo siku niliyobaini dhahiri huyu ni fisadi aliyevaa miwani ndani ana macho ya kondoo
Wanabodi,
Declaration of interest: Mimi ni mpenzi wa somo la historia, ambalo ni somo la mambo ya zamani, kuwianisha na mambo ya sasa, ili kujua mambo yajayo. Hivyo kila nipatapo fursa, hupekua kwenye historia ya mambo ya zamani na kulinganisha ni hiki kinachoendelea sasa, ili kujua nini kitakachokuja kutokea siku za baadae.
Leo nimekikumbuka kisa cha waandishi fulani wawili wa habari, ambao walishitakiwa kituo cha polisi Mabatini kwa kosa la kutishia kumuua, waziri fulani.
Kisa chenyewe ni kwa waziri huyo, baada ya kuandikwa vibaya na gazeti hilo, aliamua kubuni kesi ya kizushi, kwa kutunga uongo kuwa waandishi hao wa habari, wamemtishia maisha kuwa watamuua!, akaenda kuripoti uongo huo kituo cha polisi cha Mabatini ili kuwakomoa waandishi hao washughulikiwe!, na kweli waandishi wale walishughulikiwa kwa kuitwa polisi na kuhojiwa, kisha kuachiwa kwa dhamana kusubiria muendelezo wa hiyo kesi. Kilichofuata Waziri hakurudi tena kituoni kuthibitisha madai yake, kwa vile yalikuwa ni madai ya uongo!, hivyo kesi ikafa natural death.
Sasa kama tuhuma hii ni kweli, mtu anaweza kumzushia binadamu mwenzake tuhuma nzito kama hii, then this leaves much to be desired in the present situation and in future!. Mkumbuke, binadamu anaweza kubadili tuu tabia, lakini hulka huwa haibadiliki, anaweza tuu kuificha, lakini siku ya siku hulka huibuka!.
NB. Hili ni bandiko la ma GT, hivyo naombeni sana tusitaje taje majina.
Angalizo: Kwa wasio fahamu essence ya somo la Historia, naombeni sana, mjipitie tuu kwenye uzi huu na kujiendelea zenu na safari zenu, pia naomba nisiulizwe jambo lolote kuhusu mkasa huu kwa sababu jukumu langu ni kuwaletea historia tuu.
Kitendo cha kuripoti kitu cha uongo kwenye kituo cha polisi ni kosa la jinai, na makosa ya jinai, hayana time limitation, hivyo kesi hiyo ya kuripoti uongo kwenye kituo cha polisi, inaweza kuibuliwa wakati wowote na mhusika akapandishwa kizimbani!.
Hivyo tujifunze kutoka historia, Kama Waziri Huyu Aliweza Kutunga Uongo Huu, Kuwa Waandishi Wametishia Kumuua!, Then...
Paskali