FredKavishe
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,090
- 318
Kwanza ningeomba mods waibakishe mada yangu kwenye hili jukwaa la siasa maana linaingia kwenye siasa pia.
Mwezi uliopita nilitoa maoni jinsi ya kufanya baraza dogo la mawaziri lisizidi mawaziri 20 kupunguza gharama kwa serikali na wananchi pia kwa ujumla http://t.co/g8GxTQMm.
Baada ya maoni hayo wengi walihoji kwanini kwenye mada zangu nyingi za maendeleo nasimamia chuo cha research kama serikali yetu ikiamua kutujengea hiki chuo nina uhakika tutaiona tanzania ikitawala SADC,EAC yote hii kwa biashara mbali mbali.
Nini mantiki ya chuo cha research tumeona vijana wengi mtaani wakitengeneza magari,helicopter,mitambo ya kusagia,idea nzuri za kilimo lakini hawana sehemu ya kwenda kuziboresha idea zao ziwe za kitaifa ziweze kulisaidia taifa wanaishia kuganga njaa mtaa tu.
Mfano serikali yetu ikasikia hiki kilimo changu na mchakato ukaanza kwenye bajeti ya mwakani nina imani mpaka 2015 ujenzi utakua umefika mbali hata 2016 chuo kikafungulia na kuanza kupokea watu wajuzi mbali mbali pale.
Tukumbuke tu hii project inahitaji hela nyingi sana kutoka kwa serikali kuu mafanikio hayaji kesho yanaweza kuja baada ya miaka 10.
Mfano kijana aliyeweza kutengeneza helicopter anapelekwa kwenye hiki chuo pewa support yote huku akisaidiwa na ma eng kuweza kutengeneza helicopter nzuri zaidi na imara.
Mfano kijana mbunifu kabuni TV,Radio tunampeleka huko idea yake inaboreshwa baadaye tunaanza tengeneza tv nyingi kwa ajili ya biashara hapa nchini na nchi jirani.
Hiki chuo cha research kinaweza zalisha viwanda vikubwa zaidi ya 100 kama tukiwa makini kwenye uchunguzi wetu.
Lakini tunahitaji kuwekeza sana kununua wataalamu kutoka nchi kama israel hawa kwenye Eng wapo vizuri sana.kununua wataalamu kutoka India hapa kwenye Udaktari wako vizuri kama tunataka kuwa watengenezaji wa dawa no 1 africa.
Hii inawezekana kuwapata hawa wataalamu kama tukiamua na tukijitolea kuwalipa vizuri mishahara minono na bonasi kibao waje hapa nchini watufundishie vijana wetu pia wawe kwenye timu ya chunguzi mbali mbali.
Leo kwenye bbc nchi za ukanda wa gaza zimeungana kutengeneza research center yao kwenye madawa na ugunduzi wa magonjwa ina maana ndani ya miaka 3 mtambo ukifanikiwa huduma za afya vitaboreka.
Je hiki chuo kijengwe wapi ushauri hiki chuo kijengwe mtwara kwanini nimechagua mtwara nina sababu zifuatazo
1.Kuifungua kusini
2.Kuitumia gas izalishe umeme sababu chuo hiki kitahitaji umeme mkubwa sana
3.Kuikomboa kusini na kutengeneza ajira.
Je kama tukifanya hayo na kutafuta wataalamu waliobobea tutegemee nini baada ya miaka 5-10 maana tutakua na maeng wetu mbalimbali.
Serikali ianze kujenga viwanda vikubwa.
1.Tuifufue Nyumbu
Maana sasa tutakua na utaalamu zaidi tunaweza hata tengeneza luxury cars zikatumika nchini kwa bei rahisi zaidi
Tunaweza tengeneza mabasi makubwa ya kubeba abiria hakuna kitu nachukia kama kuona Yutong barabarani wakati sisi tuna uwezo.
2.Tujenge kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa kiwe tabora au kigoma
Baada ya kufanyia uchunguzi wa dawa mbali mbali sasa tunazitengeneza hizo dawa hiki kiwanda kiwe na jukumu kubwa moja kuliteka africa na dwa zetu.
3.Tujenge kiwanda cha radio na Tv
Kama tutaweza tengeneza tv na radio zetu na zikauzwa kwa bei rahisi tutakua na soko kubwa sana hapa africa tv na radio nyingi zinatoka china.
4.Tujenge satellite yetu mnamo mwaka 2025-2030 iruke hewani najua wengi mtashangaa tukiweza hili tutakuwa one of power house country in the world.
Kwa hiki chuo cha research tunatoa viwanda vingi sana kama tukiamua kweli tuache siasa tujenge hii nchi ifike huku.
Tunaweza tuna uranium,gas,mafuta,makaa ya mawe,chuma,madini mbalimbali, kwanini tusiweze wenzetu nawabeba madini wanaenda tengenezea kwao na kuturudisha sisi tunanua wakati ni sasa either tufurai maendeleo na panya kwa miaka 50.
Au tujenge uchumi wa tembo ndani ya miaka 20 nchi ambayo haina maviwanda makubwa haina kitu kwenye uchumi huu wa sasa lazima tuchukue maamuzi magumu.
Hii project ya chuo cha research inahitaji bilioni 150-200 kuanza ujenzi kwa kipindi chama miaka 4 chuo kitakua tayari na vifaa zaidi ya bilioni 500 itahitajika kununua zifaaa.
Ikitoka hapo serikali iwekeze bilioni 50-100 kila mwaka kwenye chuo na ujenzi wa viwanda uwe umeanza.
Haiwezekani kabisa hata vitambaa vinatoka china,vijiti vya meno vinatoka china na bado watu wanacheka kwenye mikutano tumefanya mambo makubwa gani sasa kama hatujaweza hata zalisha hata kiji radio tu.
Nigeomba nafasi siku nitaandaa huu mradi vizuri nikutanishwe na wadau ambao watakua tayari kuutumia niwape vizuri na picha za mradi utakavyokua.
Lazima tuamue kua baba wa viwanda EAC,SADC na africa kwa ujumla.
Fred kavishe