Lazima tufungue Chuo cha Research kama tunataka uchumi wetu upae

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
318
Kwanza ningeomba mods waibakishe mada yangu kwenye hili jukwaa la siasa maana linaingia kwenye siasa pia.

Mwezi uliopita nilitoa maoni jinsi ya kufanya baraza dogo la mawaziri lisizidi mawaziri 20 kupunguza gharama kwa serikali na wananchi pia kwa ujumla http://t.co/g8GxTQMm.

Baada ya maoni hayo wengi walihoji kwanini kwenye mada zangu nyingi za maendeleo nasimamia chuo cha research kama serikali yetu ikiamua kutujengea hiki chuo nina uhakika tutaiona tanzania ikitawala SADC,EAC yote hii kwa biashara mbali mbali.

Nini mantiki ya chuo cha research tumeona vijana wengi mtaani wakitengeneza magari,helicopter,mitambo ya kusagia,idea nzuri za kilimo lakini hawana sehemu ya kwenda kuziboresha idea zao ziwe za kitaifa ziweze kulisaidia taifa wanaishia kuganga njaa mtaa tu.

Mfano serikali yetu ikasikia hiki kilimo changu na mchakato ukaanza kwenye bajeti ya mwakani nina imani mpaka 2015 ujenzi utakua umefika mbali hata 2016 chuo kikafungulia na kuanza kupokea watu wajuzi mbali mbali pale.

Tukumbuke tu hii project inahitaji hela nyingi sana kutoka kwa serikali kuu mafanikio hayaji kesho yanaweza kuja baada ya miaka 10.

Mfano kijana aliyeweza kutengeneza helicopter anapelekwa kwenye hiki chuo pewa support yote huku akisaidiwa na ma eng kuweza kutengeneza helicopter nzuri zaidi na imara.

Mfano kijana mbunifu kabuni TV,Radio tunampeleka huko idea yake inaboreshwa baadaye tunaanza tengeneza tv nyingi kwa ajili ya biashara hapa nchini na nchi jirani.

Hiki chuo cha research kinaweza zalisha viwanda vikubwa zaidi ya 100 kama tukiwa makini kwenye uchunguzi wetu.

Lakini tunahitaji kuwekeza sana kununua wataalamu kutoka nchi kama israel hawa kwenye Eng wapo vizuri sana.kununua wataalamu kutoka India hapa kwenye Udaktari wako vizuri kama tunataka kuwa watengenezaji wa dawa no 1 africa.

Hii inawezekana kuwapata hawa wataalamu kama tukiamua na tukijitolea kuwalipa vizuri mishahara minono na bonasi kibao waje hapa nchini watufundishie vijana wetu pia wawe kwenye timu ya chunguzi mbali mbali.

Leo kwenye bbc nchi za ukanda wa gaza zimeungana kutengeneza research center yao kwenye madawa na ugunduzi wa magonjwa ina maana ndani ya miaka 3 mtambo ukifanikiwa huduma za afya vitaboreka.

Je hiki chuo kijengwe wapi ushauri hiki chuo kijengwe mtwara kwanini nimechagua mtwara nina sababu zifuatazo
1.Kuifungua kusini
2.Kuitumia gas izalishe umeme sababu chuo hiki kitahitaji umeme mkubwa sana
3.Kuikomboa kusini na kutengeneza ajira.

Je kama tukifanya hayo na kutafuta wataalamu waliobobea tutegemee nini baada ya miaka 5-10 maana tutakua na maeng wetu mbalimbali.

Serikali ianze kujenga viwanda vikubwa.
1.Tuifufue Nyumbu
Maana sasa tutakua na utaalamu zaidi tunaweza hata tengeneza luxury cars zikatumika nchini kwa bei rahisi zaidi
Tunaweza tengeneza mabasi makubwa ya kubeba abiria hakuna kitu nachukia kama kuona Yutong barabarani wakati sisi tuna uwezo.

2.Tujenge kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa kiwe tabora au kigoma
Baada ya kufanyia uchunguzi wa dawa mbali mbali sasa tunazitengeneza hizo dawa hiki kiwanda kiwe na jukumu kubwa moja kuliteka africa na dwa zetu.

3.Tujenge kiwanda cha radio na Tv
Kama tutaweza tengeneza tv na radio zetu na zikauzwa kwa bei rahisi tutakua na soko kubwa sana hapa africa tv na radio nyingi zinatoka china.

4.Tujenge satellite yetu mnamo mwaka 2025-2030 iruke hewani najua wengi mtashangaa tukiweza hili tutakuwa one of power house country in the world.

Kwa hiki chuo cha research tunatoa viwanda vingi sana kama tukiamua kweli tuache siasa tujenge hii nchi ifike huku.

Tunaweza tuna uranium,gas,mafuta,makaa ya mawe,chuma,madini mbalimbali, kwanini tusiweze wenzetu nawabeba madini wanaenda tengenezea kwao na kuturudisha sisi tunanua wakati ni sasa either tufurai maendeleo na panya kwa miaka 50.

Au tujenge uchumi wa tembo ndani ya miaka 20 nchi ambayo haina maviwanda makubwa haina kitu kwenye uchumi huu wa sasa lazima tuchukue maamuzi magumu.

Hii project ya chuo cha research inahitaji bilioni 150-200 kuanza ujenzi kwa kipindi chama miaka 4 chuo kitakua tayari na vifaa zaidi ya bilioni 500 itahitajika kununua zifaaa.

Ikitoka hapo serikali iwekeze bilioni 50-100 kila mwaka kwenye chuo na ujenzi wa viwanda uwe umeanza.

Haiwezekani kabisa hata vitambaa vinatoka china,vijiti vya meno vinatoka china na bado watu wanacheka kwenye mikutano tumefanya mambo makubwa gani sasa kama hatujaweza hata zalisha hata kiji radio tu.

Nigeomba nafasi siku nitaandaa huu mradi vizuri nikutanishwe na wadau ambao watakua tayari kuutumia niwape vizuri na picha za mradi utakavyokua.

Lazima tuamue kua baba wa viwanda EAC,SADC na africa kwa ujumla.

Fred kavishe
 
Kwani vyuo vikuu vilivyopo si vinafanya research?

Hakuna chuo cha maana hiyo tz hakuna kabisa yaani inakua center kabisa sasa hivi ndani ya hivi vyuo research ni ndogo sana na pesa hawapewi kabisa
 
Hakuna chuo cha maana hiyo tz hakuna kabisa yaani inakua center kabisa sasa hivi ndani ya hivi vyuo research ni ndogo sana na pesa hawapewi kabisa
Kumbe basi bora waboreshe hivi vilivyopo, watoe na ela za kutosha kuliko kuanza kujenga kipya...
 
Hakuna chuo cha maana hiyo tz hakuna kabisa yaani inakua center kabisa sasa hivi ndani ya hivi vyuo research ni ndogo sana na pesa hawapewi kabisa

Fungua chuo cha kuwafundisha wanasiasa umuhimu wa integration between research and development. Ukiweza hapo utakuwa umemaliza kila kitu. Mwanasiasa anayeamini katika tafiti atavilazimisha vyuo vikuu kumpatia tafiti mbalimbali kabla ya kufanya maamuzi yake. Vyuo vilivyopo vinatosha sana kufanya tafiti lakini watumiaji wa tafiti hizo hawapo.
 
Kumbe basi bora waboreshe hivi vilivyopo, watoe na ela za kutosha kuliko kuanza kujenga kipya...

Ni wazo tu ndugu na jiulize kwanini research nyingi za vyuoni zinaisha kwenye mavitabu makubwa
 
Fungua chuo cha kuwafundisha wanasiasa umuhimu wa integration between research and development. Ukiweza hapo utakuwa umemaliza kila kitu. Mwanasiasa anayeamini katika tafiti atavilazimisha vyuo vikuu kumpatia tafiti mbalimbali kabla ya kufanya maamuzi yake. Vyuo vilivyopo vinatosha sana kufanya tafiti lakini watumiaji wa tafiti hizo hawapo.

Ukuu asante kwa ushauri mzuri sana utaijenga hoja yangu vizuri
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, bila kujenga kituo kikubwa cha tafiti vituo vya tafiti kwa ujumla na tafiti hizo kufanyiwa kazi mambo yataenda kwa kubabaisha kama ilivyo sasa.

Miezi kadhaa iliyopita kulikuwa kuna habari ya ujenzi au kutafuta uwezekano wa ujenzi wa research center kuhusiana na mambo ya mabadiliko ya kiklimatorolojia na kwa habari ile niliyoisoma ilikuwa imependekezwa ujenzi uwe Moshi (Mlima Kilimanjaro) sijui imeishia wapi, naona kimya kimya siku zinaenda. Hatuwezi kukwepa umuhimu wa tafiti kwenye maendeleo ya nchi, la sivyo tutakuwa tunaongea na kuzunguka hapo hapo, au tunajenga na tunaendelea midomoni.
 
Kwani vyuo vikuu vilivyopo si vinafanya research?

Ni kweli kwenye vyuo vikuu tafiti zinafanyika, lakini tunapozungumzia kituo cha utafiti ni zaidi ya tafiti zinazofanyika vyuoni.
Kituo cha utafiti ni vizuri kikatenganishwa na siasa za kwenye vyuo vyetu, kijitegemee na kiwe cha kishindani kwa ajili ya maendeleo na manufaa ya nchi.
 
Tuna vituo kadhaa vya utafiti Tanzania, ukiacha vyuo vikuu... Labda tuanze kwa kuangalia kama vinafanya yale yanayotarajiwa vifanye. Kama havifanyi, then tuangalie kwanini, na lipi liboreshwe?
 
tafiti bila utekelezaji ni yale yale,tafiti zimefanyika nyingi tatizo siasa uchwara za Tanzania,halafu wakati mwingine tafiti zinafanyika tatizo linakuja kwa anayepewa jukumu la kutekeleza wengine hawana hata uelewa wa tafiti zenyewe.
 
Kama utakua umepitia bandiko langu utaelewa vizuri. Kwamba baada ya tafiti ndo tunaanza uzalishaji wa hiko kitu
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, bila kujenga kituo kikubwa cha tafiti vituo vya tafiti kwa ujumla na tafiti hizo kufanyiwa kazi mambo yataenda kwa kubabaisha kama ilivyo sasa.

Miezi kadhaa iliyopita kulikuwa kuna habari ya ujenzi au kutafuta uwezekano wa ujenzi wa research center kuhusiana na mambo ya mabadiliko ya kiklimatorolojia na kwa habari ile niliyoisoma ilikuwa imependekezwa ujenzi uwe Moshi (Mlima Kilimanjaro) sijui imeishia wapi, naona kimya kimya siku zinaenda. Hatuwezi kukwepa umuhimu wa tafiti kwenye maendeleo ya nchi, la sivyo tutakuwa tunaongea na kuzunguka hapo hapo, au tunajenga na tunaendelea midomoni.

Shukurani mkuu upo umuhimu tena waharaka sana
 
Nelsoma Mandela is a researching institution; Tropical Pesticide Research Institute, Ifakara Research Institute, AMREF and many more
 
Fred nakubaliana na wewe 100% ingawa wasiwasi wangu ni namna watakavyotekeleza. Serikali yetu imekuwa ikipelekewa mapendekezo mengi yaliyotokana na tafiti za vyuo na wataalam wa mashirikia au taasisi binafsi kuhusu masuala mbalimbali lakini imekuwa ikiyatia kapuni. Kwa hiyo wakati naungana kukubaliana ulichokisema, ningeshauri kuwe na namna ya kufuatilia utekelezaji wa matokeo ya research zetu.
 
Shukurani ufuatiliaji ni jambo la muhimu sana
 
Nakubaliana na wewe mkuu kwa 100%,

Mataifa ya wenzetu yaliweza kukua baada ya kukazie elimu ya vtendo, na kila kijana hupelekwa kusomea kile kipaji chake kinachochipuza awali kabisa!

Taifi nyingi za wanafunzi vyuoni zinaishia makabatini tu hazimsaidii kijana huyu kuikulia tafiti yake!

Safi sana mkuu, wahusika wa elimu wachukue ushauri wako mzee!
 
Shukurani mkuu hope wataufanyia kazi
 
Back
Top Bottom