Lazima mke ashuke tu kwa mumewe vinginevyo hakuna ndoa

Haaa jamani siyo nyie mnaosemaga kwamba mkiwa mnatongoza ile mara ya kwanza mnakuwa hamjatupenda bali mnakuwa mmetutamani tu halafu upendo wenu utategemea na tabia za hao wanawake mliowatongoza?
Yeap, uko sahihi mwanafunzi wangu maana naona unaanza kunielewa, sasa ukishaingia ndani ukaolewa hapo andiko linakuwa limitimia kwa100%

Yaani wewe unakuwa umependwa,ni wewe kutimiza wajibu wako wa kutii na kula mema ya mmeo.
 
Hongera kutambua hilo Kaka, ngoja tuwaombee Marioo watokwe na upofu ili warudishe hadhi ya uanaume ktk jamii.
Wapumbavu Kama Hawa

Ngoja wanyooshwe kwa vile kila mtu atabeba msalaba wake shaur yao
tapatalk_1560276590971.jpeg
 
Yeap,uko sahihi mwanafunzi wangu maana naona unaanza kunielewa ,sasa ukishaingia ndani ukaolewa hapo andiko linakuwa limitimia kwa100%
Yaani wewe unakuwa umependwa,ni wewe kutimiza wajibu wako wa kutii na kula mema ya mmeo.
Wacha we haya bwana
 
Wapumbavu Kama Hawa

Ngoja wanyooshwe kwa vile kila mtu atabeba msalaba wake shaur yao View attachment 1125813
Haya sasa unakuta na mwanaume kama huyo naye anataka mke wake amtii hivi ni haki hiyo kweli? Uanaume siyo jinsia na nafasi mlizopewa tu jamani bali pia uanaume ni uwezo wa kubeba na majukumu mliopewa juu ya wake zenu na watoto wenu bila kutegemea wake zenu wawasaidie waambieni wanaume wenzenu hao mwanamke kumheshimu mwanaume kama huyo yataka moyo siyo kidogo hebu vaeni viatu vyetu muone jamani
 
Mwanaume yupo juu siku zote na atabaki kuwa juu.
Mwanaume amepewa nafasi ya kuwa kichwa katika familia .
Mwanamke ameagizwa utii kwa mumewe
Mwanaume ameagizwa kuishi na mwanamke wa akili.,pia kumpenda mkewe
Tatizo huja pale wanaume wengi wanapokosa akili za kuishi na wake zao,,,hawawezi kusimama katika nafasi zao ipasavyo.

Shida huanzia kwa Mwanaume...
Mipango yote huanzia kichwani...
Kichwa huamua Nini mguu ufanye na Nini usifanye ,,Nini mkono ufanye Nini usifanye
Kama kichwa hakina maamuzi mazuri hata mwili pia utakaa vibaya

Vivyohivyo kiburi kwa mwanamke Ni matokeo ya mumewe kishindwa kusimama vema kwenye nafasi yake Kama kichwa
Mm hili jambo silikubali kwa 100%... HV hakuna wanawake viburi naturally??
HV hakuna wanawake wenye Tania mbaya naturally??
Iweje mke akiwa na tabia mbaya mseme n lazma mume kahusika kumfanya awe na tabia mbovu??
 
Mm hili jambo silikubali kwa 100%... HV hakuna wanawake viburi naturally??
HV hakuna wanawake wenye Tania mbaya naturally??
Iweje mke akiwa na tabia mbaya mseme n lazma mume kahusika kumfanya awe na tabia mbovu??
Aisee mbona wanaume kwenye kuchepuka wote huwa mnasingizia wake zenu ndo chanzo kwani hakuna wanaume malaya naturally? Yaani hii dunia bwana
 
Mm hili jambo silikubali kwa 100%... HV hakuna wanawake viburi naturally??
HV hakuna wanawake wenye Tania mbaya naturally??
Iweje mke akiwa na tabia mbaya mseme n lazma mume kahusika kumfanya awe na tabia mbovu??
Hizo Ni exceptions ambazo zinaweza kutokea kwa pande zote 2,na hii itakuwa nje ya mada

Hayupo mwanamke anayemdharau mwanaume anayempenda mwanamke huyo kwa dhati na anayesimama kwenye nafasi yake vizuri.

Ukiona unampenda kweli na unasimamia nafasi yako vzr na bado anakudharau nenda kaongee vizuri na Mungu
 
Kwahiyo una maana kuwa huo utandawazi mbovu umewakumba watoto wa kike tu? Si wapo na wa kiume ambao umewakumba au kwa watoto wa kiume ukiwakumba ni sawa?

Halafu unaposema eti ni lazima mwanamke ukitaka kumuoa umkuta anajua kufanya kazi za nyumbani zote unamaanisha nini? Unamaanisha kwamba hauwezi kumvumilia mwanamke ambaye hatatimiza majukumu yake si ndiyo?

Kwahiyo unataka kusema kwamba na sisi wanawake tusiolewe na wanaume ambao hawajui kutafuta pesa tusubiri wakishatafuta wakapata ndo tukaolewe nao si ndiyo? Maana hata sisi hatuwezi kuwavumilia wanaume ambao hawataweza kutimiza majukumu yao

Kwa mitazamo hii acha tu na sisi wanawake tuendelee kutafuta wanaume wenye pesa tu kwa kweli haiwezekani wanaume mshindwe kutimiza majukumu yenu kwa kisingizio cha kuwa hamna uwezo halafu mnataka wake zenu watimize majukumu yao yote tena wawasaidie na ya kwenu kabisa halafu nyie kuwasaidia ya kwao hamtaki mnaita umume bwege
Kila mwanamke ana akili zake......hata mkiongea sana hii battle hakuna atakayeshinda.....mwisho wa siku maisha yataendelea...ndoa n kusaidiana,kuvumiliana na kupendana.
 
Yaani mnavyoongeaga hizo kauli mnajikutaga miungu wenyewe mnadhani mnamkomoa nani sasa? Kwa Mungu mwanaume malaya na mwanamke malaya wote wana dhambi

Na kama ni kwenye jamii sidhani kama siku hizi wanawake tunajali tena jinsi tutakavyoonekana kwenye jamii yaani wanawake wa hivyo wamebaki wachache mno na ndo hao ambao wako tayari kuwa hata watumwa kwa wanaume ili tu waolewe lakini wengine tushashituka siku hizi

Ndoa anapanga Mungu na siyo binadamu na Mungu hakumleta mwanamke duniani aje ateseke wala kuwa mtumwa wa mwanaume na wala Mungu hakutaka ndoa zile za mwanamke kujifanya mjinga hata kama mumewe kakosea vipi

Dunia imeshabadilika siku hizi wanaume kubalianeni tu na hali halisi na kama mnaona kuwa hao wanawake mnawatumia endeleeni kujidanganya maana sidhani kama unaweza kusema eti unamtumia mtu ambaye anafanya kitu kwa raha zake
Ila wewe n moja ya wapenda 50-50%...... Mungu atakupa kulingana na stahili yako
 
Mkuu siyo kila anayetetea vichaa basi na yeye ni kichaa hivyo basi siyo kwa sababu nimewatetea wanawake walioolewa na marioo basi na mimi nimeolewa na marioo kwanza kabisa mimi sijaolewa na mpenzi wangu naweza kusema anajitahidi sana katika kusimamia nafasi yake na kutimiza wajibu wake kwangu lakini nimeamua niwaseme wale wanaume ambao siku hizi nao wanatafuta wanawake ambao wana akili ya maisha au ambao wanajua kutafuta pesa

Ili wawasaidie hao wanaume kutafuta pesa na kuhudumia familia kumbe mnajua kuwa wanaume wa design hiyo wapo na ndo hao marioo sasa mbona hamuwasemi kutwa kutusema wanawake tu niamini mimi mwanamke akishaanza kuingilia majukumu ya mume wake lazima tu atakuwa na dharau huyo mume atake asitake na kama hataki basi ndo atimize majukumu yake yote kama mwanaume bila kusubiri mke amsaidie
Natamani niongee kitu ila nahis huwez kunielewa.....akili yako yote ushaidirect ktk kubishana badala ya kueleweshana .....punguza jazba then come and discuss with proper knowledge
 
Kila mwanamke ana akili zake......hata mkiongea sana hii battle hakuna atakayeshinda.....mwisho wa siku maisha yataendelea...ndoa n kusaidiana,kuvumiliana na kupendana.
Kumbe mnalijua hilo mbona mnawasemea wanaume wenzenu wanaoteseka kwenye ndoa hadi mnatukashifu wanawake? Waacheni hivyo hivyo maana kila mtu si ana akili zake
 
Ila wewe n moja ya wapenda 50-50%...... Mungu atakupa kulingana na stahili yako
Kwanini nipende 50/50? Tatizo wanaume mnapenda wale wanawake wa kila kitu "ndiyo mume wangu" hao ndo mnawaona wanyenyekevu sisi wengine ambao tunawarekebisha kwenye baadhi ya mambo mnayokosea mnaona tunapenda usawa.

Na yote hiyo ni kwa sababu hampendi kuambiwa na kuukubali ukweli mmeshazoea wale wanawake kama wa zamani ambao hata mfanye kosa gani wanawavumilia na kuwasamehe tu huku wao wanaumia ndani kwa ndani maana hawawezi kuwakosoa waume zao sababu wanaogopa wataonekana wajeuri.
 

Similar Discussions

57 Reactions
Reply
Back
Top Bottom