Lazima mke ashuke tu kwa mumewe vinginevyo hakuna ndoa

Ndo haya mashindano na wanaume mnayoambiwa lakini hamsikii kama mna laana vile.
Huwezi ukaheshimiwa Kama hujakaa vema kwenye nafasi yako
Ukiona mwanamke anakudharau Rudi jitathmini wapi unakosea

Sipo hapa kwa ajili ya kutetea wanawake lakini naongea ukweli
Mwanaume aliyesimama vema katika nafasi yake hawez kumpa mwanya mwanamke wake amdharau
 
Huwezi ukaheshimiwa Kama hujakaa vema kwenye nafasi yako
Ukiona mwanamke anakudharau Rudi jitathmini wapi unakosea

Sipo hapa kwa ajili ya kutetea wanawake lakini naongea ukweli
Mwanaume aliyesimama vema katika nafasi yake hawez kumpa mwanya mwanamke wake amdharau
Mbona unachanganya mambo.
 
Tukiwaambia "haki sawa" ni mchochezi wa kuvunja ndoa wabishi kama mawe yapigwayo na mawimbi baharini lkn hayatakati kamwe!

Wazazi wa kizazi hiki wanalea watoto kimayai mayai bila kujua wanawaanda wake za Watu kizazi cha kesho.

Mwanamke anamaliza form six hajui kupika, kufua nguo wala kudeki nyumba zaidi ya kufuga kucha kama paka shume.

Binti yuko darasa la 3 kashajua kila aina ya mitandao inayohamasisha ngono na kujibu Watu hovyo hovyo matusi bila aibu wala hofu.

USA & ULAYA kiujumla wameshavunja ndoa sana kupitia hilo pepo la "haki sawa" hadi kuongoza idadi kila mwaka duniani na kuamua wafunge ndoa za mikataba ambazo ni kinyume na Mungu.

Wanaume wenye hekima sasa hivi wanaogopa Wanawake wasomi na wenye ajira zao kama ebola, hujiulizi kwanini ndoa nyingi sana zenye changamoto ktk maelewano ni hao hao wasomi?


Mungu atusaidie sana tuliojaliwa upeo kuona mbele zaidi athari za ulimbukeni wa kuiga iga utandawazi toka nchi za magharibi unaochangia kiasi kikubwa sana kuathiri mila na desturi zetu Waafrika hadi kuharibu matunda mazuri ya ndoa bora.

Naomba muitunze hii sms kuwa ushuhuda ili miaka 10 ijayo iwe ushahidi Mungu akipenda tuwe hai.
 
Back
Top Bottom