Lazima kuna sababu za msingi sana kwa Msumbiji kuomba msaada wa kijeshi Rwanda kukabili waasi badala ya Tanzania ambao wana undugu nao wa damu

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
Kuna wakati Tanzania ilijulikana kwa umahiri katika mapambano ya kivita, na jeshi letu JWTZ liliaminika sana katika uwanja wa mapambano. Hata waasi sehemu kama DRC walikuwa wakisema wazi, kwamba hawakuogopa kukabiliana na jeshi jingine lolote isipokuwa JWTZ ndio waliwaogopa sana. Tulijenga sifa pia upande wa vikosi vya Umoja wa Mataifa kwamba tuna jeshi linalotumainika na kutegemeka.

Lakini baada ya hivi karibuni Msumbiji kupata matatizo na waasi, wamekimbilia Rwanda kuomba msaada, na sio Tanzania. Najiuliza sana, kulikoni tena Msumbiji wamegeukia Rwanda na sio Tanzania tena? Na habari kutoka Msumbiji zinasema jeshi la Rwanda limefanya maajabu Msumbiji na kukomboa sehemu iliyokuwa ikikaliwa na waasi.

Ukweli ni kwamba fursa za jeshi letu kutoa msaada wa kijeshi pale unapotakiwa ni fursa nzuri sana ya kulipa mazoezi halisi ya kivita. Wakati wa vita na Idd Amin, sababu moja iliyofanya tumpige kirahisi ilikuwa kwamba jeshi letu lilikuwa na uzoefu wa vita katika mapambano ya kupigania uhuru kusini mwa Afrika. Kwa hiyo Idd Amin alichokoza nchi ambayo wanajeshi wake walikuwa wamebobea vita, wakati wanajeshi wa Uganda walikuwa wameoteana vitambi na uzoefu wao ilikuwa kupiga raia wasio na silaha. Sasa nachelea sababu za Msumbiji kuamua kwenda Rwanda safari hii. Au wameona tuko busy na mabishano ya katiba mpya na kupambana na wapinzani wa siasa mitaani?

Reference: Rwandan, Mozambican troops capture rebel stronghold in Cabo Delgado
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
1628699333162.png
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,895
2,000
Kulinda amani au kupigana na waasi sioni kama ni fursa, huo naona ni msaada. Afrika kuna nchi zaidi ya 50, kwa nini Tanzania ndio unataka tuwe na kiherehere kila vita ikitokea.

-Mozambique tumekaa miaka na miaka uko kipindi cha Samora Machel
-Zimbabwe hadi walikuwa na kambi hapa
-Uganda rais wao tumemlea sisi
-DRC kipindi cha M23
-Angola wale kina MPLA tena vita yao ilihusisha superpowers
-Visiwa gani pale bahari ya Hindi kipindi cha Kikwete tulienda zuia mapinduzi
-Tumelinda amani Darfur

Kuna faida gani tunapata, kuna hasara gani tunapata tusipoenda Mozambique. Hawajaomba msaada kwetu, ulazima wa wao kuja kwetu ni upi. Kwenye ranking za majeshi bora hakuna kigezo cha kulinda amani kuwa ishara ya jeshi imara. Mbona ule ni utashi.

Ujerumani ina miaka haishiriki mission yoyote, Japan tangu 1945 haijatoa mwanajeshi wake nje ya mipaka, Taiwan tangu iwe huru haijashiriki vita au mapigano yoyote, Switzerland tangu karne ya 16 uko haijaingia vitani na yeyote wakati jirani zake wameingia vita kibao. Sasa kapigane nao kisa huwa unafukuza majambazi msituni uone kama haujaangushwa.
 
Jesuitdon

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
3,211

Nakuungakono
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,895
2,000
Kwanza kutoiita Tanzania imekaa kisiasa zaidi na ni sahihi. Rwanda iko mbali na Mozambique hata ikiwa na mipango hasi itazuilika kirahisi, Tanzania majirani tuna watu wetu uko tukitaka kuihujumu Msumbiji si ni kama kunywa maji. Hata Rwanda ikipata shida usitarajie kuona inakimbilia Tanzania, ni kuepuka influence za lazima
 
diranqhe

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
1,464
2,000
"Ukweli ni kwamba fursa za jeshi letu kutoa msaada wa kijeshi pale unapotakiwa ni fursa nzuri sana ya kulipa mazoezi halisi ya kivita".

Hii ni point ya ovyo. Nchi haitoi wanajeshi kiholela kuna mambo mengi mno ya kuzingatiwa.
 
KOLOKOLONI

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
2,037
2,000
Kuna wakati Tanzania ilijulikana kwa umahiri katika mapambano ya kivita, na jeshi letu JWTZ liliaminika sana katika uwanja wa mapambano. Hata waasi sehemu kama DRC walikuwa wakisema wazi, kwamba hawakuogopa kukabiliana na jeshi jingine lolote isipokuwa JWTZ ndio waliwaogopa sana. Tulijenga sifa pia upande wa vikosi vya Umoja wa Mataifa kwamba tuna jeshi linalotumainika na kutegemeka.

Lakini baada ya hivi karibuni Msumbiji kupata matatizo na waasi, wamekimbilia Rwanda kuomba msaada, na sio Tanzania. Najiuliza sana, kulikoni tena Msumbiji wamegeukia Rwanda na sio Tanzania tena? Na habari kutoka Msumbiji zinasema jeshi la Rwanda limefanya maajabu Msumbiji na kukomboa sehemu iliyokuwa ikikaliwa na waasi.

Ukweli ni kwamba fursa za jeshi letu kutoa msaada wa kijeshi pale unapotakiwa ni fursa nzuri sana ya kulipa mazoezi halisi ya kivita. Wakati wa vita na Idd Amin, sababu moja iliyofanya tumpige kirahisi ilikuwa kwamba jeshi letu lilikuwa na uzoefu wa vita katika mapambano ya kupigania uhuru kusini mwa Afrika. Kwa hiyo Idd Amin alichokoza nchi ambayo wanajeshi wake walikuwa wamebobea vita. Sasa nachelea sababu za Msumbiji kuamua kwenda Rwanda safari hii. Au wameona tuko busy na mabishano ya katiba mpya na kupambana na wapinzani wa siasa mitaani?

Reference: Rwandan, Mozambican troops capture rebel stronghold in Cabo Delgado
Yamefanyika hayo siyo sababu za udhaifu wa Jeshi letu bali mbinu za kimapambano tu. Taarifa za kiintelijensia zilitaka litumike Jeshi hilo kwa Usalama wa Serikali ya Kigali na Usalama wa Serikali ya Dodoma.
 
Nyonzo bin mvule

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
1,063
2,000
Kulinda amani au kupigana na waasi sioni kama ni fursa, huo naona ni msaada. Afrika kuna nchi zaidi ya 50, kwa nini Tanzania ndio unataka tuwe na kiherehere kila vita ikitokea.

-Mozambique tumekaa miaka na miaka uko kipindi cha Samora Machel
-Zimbabwe hadi walikuwa na kambi hapa
-Uganda rais wao tumemlea sisi
-DRC kipindi cha M23
-Angola wale kina MPLA tena vita yao ilihusisha superpowers
-Visiwa gani pale bahari ya Hindi kipindi cha Kikwete tulienda zuia mapinduzi
-Tumelinda amani Darfur

Kuna faida gani tunapata, kuna hasara gani tunapata tusipoenda Mozambique. Hawajaomba msaada kwetu, ulazima wa wao kuja kwetu ni upi. Kwenye ranking za majeshi bora hakuna kigezo cha kulinda amani kuwa ishara ya jeshi imara. Mbona ule ni utashi.

Ujerumani ina miaka haishiriki mission yoyote, Japan tangu 1945 haijatoa mwanajeshi wake nje ya mipaka, Taiwan tangu iwe huru haijashiriki vita au mapigano yoyote, Switzerland tangu karne ya 16 uko haijaingia vitani na yeyote wakati jirani zake wameingia vita kibao. Sasa kapigane nao kisa huwa unafukuza majambazi msituni uone kama haujaangushwa.
Nakubaliana na wewe, na inajulikana wazi kabisa kagame mtu wa sifa so chochote anachofanya lazima dunia ijue, kama ni operation tushafanya nyingi tu
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,920
2,000
Wale makomandoo wanaovunja matofali kwa vichwa hawana muda wa kupigana na Al Shabab.
Wanaujua moto wao.
Kenya waliwagusa Al Shabab hadi leo wananuka damu.
 
Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
9,485
2,000
Kwanza kutoiita Tanzania imekaa kisiasa zaidi na ni sahihi. Rwanda iko mbali na Mozambique hata ikiwa na mipango hasi itazuilika kirahisi, Tanzania majirani tuna watu wetu uko tukitaka kuihujumu Msumbiji si ni kama kunywa maji. Hata Rwanda ikipata shida usitarajie kuona inakimbilia Tanzania, ni kuepuka influence za lazima
Nimekusoma Mara mbili uko kwenye military circles umeongea Jambo kubwa kirahiiisi.
 
luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
4,297
2,000
Ndugu mtoa mada yakupasa utambue ya kuwa MZA yenyewe awali ili kataa msaada wa kijeshi tokea ktk nchi za SADEC na rais filepe nyusi aliomba msaada tokea USA na Ureno.

Ureno walipeleka jeshi lao kwa kipindi kifupi wakarejeshwa na nafikir USA hawakupeleka kabisaa

Felipe nyusi kwa aibu yake akaenda Rwanda kuomba msaada wa jeshi pia aliomba msaada tokea Angola defence force

Nafikir sasa SADEC wameona watoe msaada maana hata jeshi la marekan kupitia kamandi yake ya Africa mkuu wake alikuwepo hapa Tz kama majumaa kadhaa huenda ikawa na wao wametia ubani kuiomba chonde chonde JWTZ ipeleke wanaume wa kazi
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
4,017
2,000
Kuna wakati Tanzania ilijulikana kwa umahiri katika mapambano ya kivita, na jeshi letu JWTZ liliaminika sana katika uwanja wa mapambano. Hata waasi sehemu kama DRC walikuwa wakisema wazi, kwamba hawakuogopa kukabiliana na jeshi jingine lolote isipokuwa JWTZ ndio waliwaogopa sana. Tulijenga sifa pia upande wa vikosi vya Umoja wa Mataifa kwamba tuna jeshi linalotumainika na kutegemeka.

Lakini baada ya hivi karibuni Msumbiji kupata matatizo na waasi, wamekimbilia Rwanda kuomba msaada, na sio Tanzania. Najiuliza sana, kulikoni tena Msumbiji wamegeukia Rwanda na sio Tanzania tena? Na habari kutoka Msumbiji zinasema jeshi la Rwanda limefanya maajabu Msumbiji na kukomboa sehemu iliyokuwa ikikaliwa na waasi.

Ukweli ni kwamba fursa za jeshi letu kutoa msaada wa kijeshi pale unapotakiwa ni fursa nzuri sana ya kulipa mazoezi halisi ya kivita. Wakati wa vita na Idd Amin, sababu moja iliyofanya tumpige kirahisi ilikuwa kwamba jeshi letu lilikuwa na uzoefu wa vita katika mapambano ya kupigania uhuru kusini mwa Afrika. Kwa hiyo Idd Amin alichokoza nchi ambayo wanajeshi wake walikuwa wamebobea vita, wakati wanajeshi wa Uganda walikuwa wameoteana vitambi na uzoefu wao ilikuwa kupiga raia wasio na silaha. Sasa nachelea sababu za Msumbiji kuamua kwenda Rwanda safari hii. Au wameona tuko busy na mabishano ya katiba mpya na kupambana na wapinzani wa siasa mitaani?

Reference: Rwandan, Mozambican troops capture rebel stronghold in Cabo Delgado
Vita haipiganiwi mtandaoni

Mkuu unaaamini kabisa, Msumbiji wakienda kuomba msaada kutoka Rwanda, badala ya jirani zake Tanzania na Afrika kusini?

Yaani tuamini majeshi ya South Afrika na Tanzania yaliogopa,ndio Rwanda akaenda?don't be naive! Bro hao waasi walikuwa wameisha malizwa, Rwanda ameenda hatua za mwisho tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom