Sikumbuki kama kuna wiki imepita Tanzania hii bila kusikia habari za vifo vya ndugu zetu wengi wanaopoteza maisha sababu ya uzembe wa drivers wa mabasi na matajiri wao. Kila siku watoto wanapoteza wazazi, wake wanapoteza waume zao na waume wanapoteza wake zao. Tunapoteza kaka na dada zetu, shangazi na wajomba, bibi na babu zetu. Nguvu kazi inapotea kila siku.Kwanini ndugu zetu wapotee kila siku?
Hivi kweli mamlaka zote hazioni kwamba hili halivumiliki tena? Kwanini familia ziwe kwenye machungu kila siku? Kwanini wanasheria wetu hawalioni hili na kufungua kesi za madai kwa ndugu na familia wanaopoteza ndugu zao katika ajali hizi za kijinga ambazo nyingi zina epukika kabisa? Kesi za madai zitawafanya matajiri wa mabasi walipe na kufilisiwa kabisa na ndiyo njia pekee ya matajiri hawa kuhakikisha wanaajiri drivers ambao wana-qualify kubeba abiria.
Jana jumapili watu 11 wamekufa huko Morogoro, leo jumatatu watu 30 wamekufa kwa ajali ya kijinga kabisa "eti drivers wa kampuni moja walikuwa wakiyumbisha mabasi wakisalimiana walipokutana barabarani huko Singida." We have reached the point now we have to say enough is enough, and something must be done. If this means we have to go back to speed governors, let it be. We have to do anything that will limit the speed of busses on the road.
Hili ni lazima liende sambamba na uboreshaji wa maslahi ya drivers. Mungu azilaze roho za marehemu wa ajali ya leo Singida mahali pema peponi na kuwafariji wafiwa.
AMEN.