Lazaro Nyalandu: Nikiwa na mtoto Doreen Mshana tulipomtembelea hospitali

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Anaandika Mbunge wa Singida Mhe Lazaro Nyalandu,
Nikiwa na Dkt. Urio, Mkuu wa Hospitali ya Mt Meru, na mtoto Doreen Mshana tulipomtembelea alasiri leo kumwona yeye pamoja na watoto wenzake wawili wanaoondelea na matibabu kutokana na ajali ya Karatu.

Wazazi (akina Mama) wote watatu wa watoto hawa wanaelekea Dar es Salaam jioni ya leo kwa maandalizi ya kupata hati ya kusafiria na baadae kuomba visas kwa ajili ya kuwasindikiza watoto wao kwenye matibabu zaidi Nje ya nchi kama alivyoeleza Mh Makamu wa Rais wakati wa kuwaaga wenzao waliotangulia kutokana na mkasa wa ajali hiyo. Tuendelee kuwaombea Mungu aifanikishe safari hiyo kwa utukufu wake mwenyewe. Iwe heri na salama kwao!

tmp_30576-FB_IMG_1494526536680-1667873048.jpg


=======UPDATES

Tumefanikiwa kupata ndege aina ya DC 8 kutoka Shirika la Samaritan Purse linaongozwa na mtoto wa Billy Grahm, aitwaye Franklin Grahm kwa ajili ya kuwasafirisha watoto Doreen, Sadia, na Wilson pamoja na wazazi wao watatu (Mama zao), ikiwa ni pamoja na Muuguzi Simphorosa Silalye, na Daktari Elias Mashalla wa Mt Meru hospitali.

Ndege hii inaondoka jioni ya leo kutoka mji Mkuu Charlotte, Jimbo la North Carolina nchini Marekani na inatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Kilimanjaro majira ya jioni, Jumamosi, Mei 13. Endapo upatikanaji wa visas utafanikiwa hapo kesho kama tunavyo tarajia, wasafiri wataondoka asubuhi ya Jumapili, Mei 14 kuelekea Amerika.

Ndege hii aina ya DC 8 itatarajiwa kutua Mjini Charlotte, NC, na wagonjwa pamoja na waliowasindikiza wataingia katika ndege nyingine maalumu ya kubeba wagonjwa (Air Ambulance) hadi mji wa Sioux City, Iowa ambako watapokelewa na Uongozi wa Hospitali na Mercy na Shirika la STEMM.
Watoto hao ambao hali zao si nzuri ni Doreen, Saidia na Wilson na watakwenda Marekani kwa ajili ya matibabu pamoja na wazazi wao
 
AMEN, nimefurahi sana kusikia habari za watumishi wa Mungu na wasamaria wema sana Bill Graham na Mwanae.

Ila sioni hata sababu za wao kuzungushwa na hizo process za Visa mpaka kusema

"kama ikipatikana" hata kama ndio protokali

Hii ni urgent issue na hao ni majeruhi.
 
AMEN, nimefurahi sana kusikia habari za watumishi wa Mungu na wasamaria wema sana Bill Graham na Mwanae.

Ila sioni hata sababu za wao kuzungushwa na hizo process za Visa mpaka kusema

"kama ikipatikana" hata kama ndio protokali

Hii ni urgent issue na hao ni majeruhi.
Umeandika ukweli kabisa nakuunga mkono hili jambo la dharura linatakiwa kushughulikiwa kwa haraka sana.
Ila sioni hata sababu za wao kuzungushwa na hizo process za Visa mpaka kusema
 
Nyalandu wewe si kiongozi tu ila ni baba Bora, Allah akusimamie katika harakati zako zote kuna watu wakubwa tu nchi hii wameshawasahau hawa watoto lakini wewe bado moyo wako unaonyesha kua nao kwa kuwafatilia kila hatua watakayopita ili kuokoa maisha yao
Allah Mjaalie huyu mja
 
Najiuliza tu kwa mfano na nia njema......kama wale wazungu wasinge tokea siku ile...kingetokea nini?

Kuna ajali nyingi zimetokea baada ya ile....... Jamani waziri husika pigana huduma ziwe bora.....kinacho wezekana kwa wenzentu na kwetu kiwepo pia hata hospital chache tu basi.

Mungu awatangulie wafike salama na wafanikishe matibabu yao salama. Mungu awabariki pia wafadhili hao kwa moyo wa kipekee.
 
Back
Top Bottom