jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Dk. Slaa amshukia mbunge mwenzake
2008-07-15 11:09:29
Na Elisante John, PST Singida
Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, amemshukia mbunge mwenzake, Bw. Lazaro Nyalandu (CCM-Singida Kaskazini) akimtuhumu kumuoa Miss Tanzania kwa kutumia michango ya wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule.
Akitoa tuhuma hizo, Dk. Slaa ambaye pia ni kiongozi wa Kamati ya Bunge ya Kukagua Hesabu za Serikali za Mitaa, alidai kuwa, hivi karibuni, zilitolewa Sh. 40,000 kwenye fungu la ujenzi huo na kuchangia harusi ya Mbunge huyo.
Hata hivyo, Bw. Nyalandu alipoulizwa juu ya madai hayo, alikanusha kupewa.
Dk. Slaa, alitoa onyo hilo mjini hapa jana wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Singida Mjini katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi.
Akihutubia kwa niaba ya ushirikiano wa vyama vitano vya siasa vya upinzani nchini, aliwataka wakazi wa Singida kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vyama vya upinzani katika mapambano dhidi ya mafisadi, badala ya kuendelea kuing`ang`ania CCM huku wakijiita wakereketwa.
Dk. Slaa, alisema wakazi wa mkoa huo wanaona sifa na ufahari mkubwa kuitwa `Singida ni Mkoa wa CCM`, lakini bila kujua wananyonywa na mafisadi waliowaweka madarakani, huku wao wakiambulia kuvaa kofia, tisheti na khanga za mabango au dumu moja la pombe na kutoa kura kwa mtu akaibe mabilioni.
Akitoa mfano, Dk. Slaa alitoa nakala ya muhtasari wa kikao cha kamati ya maendeleo ya kata ya Kinyeto, wilayani Singida, kilichokaa Desemba, mwaka jana, kupitisha matumizi ya fedha za ujenzi wa sekondari, badala yake zimetumiwa isivyo halali.
Alitaja baadhi ya matumizi hayo kuwa ni pamoja na kuchangia harusi ya Mbunge wa Jimbo hilo, Sh. 40,000, posho kwa wajumbe wawili kwenda benki Sh. 40,000, posho kwa ajili ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Sh. 30,000, kufuatilia mbao Sh. 20,000 na kufuatilia kibali wilayani Sh. 85,000.
``Kwa kweli haya ni matumizi mabaya kabisa ya michango ya wananchi ambao wamelazimika kuchangishana ili kujenga shule ya sekondari watoto wao wasome, lakini bila sababu za msingi mafisadi, wezi, wamekula fedha hizo,`` alidai Dk. Slaa.
Aliongeza ``haiwezekani jasho la wananchi litumiwe na mtu mmoja�Eti ili tu kumfurahisha Mbunge aweze kumuoa miss Tanzania�angalia jinsi watu wa Singida mnavyochekwa na wenzenu, huku mnajiita ni mkoa wa CCM.``
Dk. Slaa alisema kuwa iwapo mkoa huo ungekuwa na Diwani hata mmoja tu anayetoka chama cha upizani, angesaidia kukemea maovu mbali mbali yanayotokea katika mkoa huo, lakini kutokana na kujiita mkoa wa CCM, ndiyo maana maovu mengi yanachelewa kufichuliwa hadi wao watoke mbali.
Aidha, Dk. Slaa, alikemea tabia ya baadhi ya Watendaji wa Serikali kuwaandikia barua za vitisho watendaji wa kata na vijiji wasioiunga mkono CCM.
Alisema kuwa ana ushahidi wa kutosha juu ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Benadetta Kinabo, aliyehamishiwa Manispaa ya Moshi, juu ya kujihusisha na tabia hiyo ambayo ni kinyume na maadili ya kazi yake.
Ili kuhakikisha tabia hiyo inakomeshwa, Dk. Slaa alisema kuwa kwa kushirikiana na vyama vya upinzani bungeni, atahakikisha Mkurugenzi huyo anaitwa na kuhojiwa, ili iwe fundisho kwa watendaji wengine wa serikali wanaodhoofisha vyama vya upinzani nchini.