Lazaro Nyalandu: Kwa sasa, mipango ya kumsafirisha Lissu kwenda nje itasimama kutokana na ushauri wa Madaktari

Nimeshangaa kwa kweli.Chadema mnataka Lissu Afe ?Hainiingii akilini kuwa maDr wa Nairobi wakatae kuandika ruhusa ya kupelekwa Marekani.Kuna kitu hapa tunafichwa.Halafu bado Chadema mnaendelea kuomba michango.Hivi ruzuku zinafanya kazi gani?Jamani eeeeh Africa ni Africa tu tena East Africa Nairobi bora hata ingekuwa South.Lissu anahitaji matibabu nje ya Africa please.
Wangekuwa wamekubali ushauri wa kumpeleka Muhimbili National Hospital, angalikuwa yuko South Africa au India long time ago. Madaktari wa Nairobi Hospital huwezi kuwapelekesha kutoa rufaa ya kutibiwa sehemu nyingine kama tulivyozoea kuwapelekesha madaktari wetu wa Muhimbili hata kwa magonjwa ya mafua. Kuwaomba madaktari kutoa rufaa ya kutibiwa sehemu nyingine, ni dharau kubwa kwa madaktari hao wanaokutibu. Ni kuonyesha kuwa hauna imani nao sana ukilinganisha na wa kule unakotaka mgonjwa wampeleke. Na mara nyingi huwa huwajui kwa kina uwezo wa hao madaktari unaotaka uwapelekee mgonjwa wako. Wakati mwingine hao madaktari unaotaka uwapelekee mgonjwa wako ni wanafunzi wa hawa madaktari unaotaka kuwaacha.

Tatizo kubwa la wanasiasa wetu ni kuingilia maamuzi hata ya professions. Wanajiona kuwa wao ndiyo wajuaji wa mambo yote na kuongea maneno kama ' Critical but stable' maneno ambayo professionally they don't make any sense. Your life cannot be in a critical state (at the edge of losing it) while at the same time be in a stable state (no chance of losing it)!
 
Huyu nyarandu anatoa taarifa kama nani ? Kwanini asibaki kuwa mpenzi mtazamaji ? Atulie kwanza
Soon utasikia nape au bashe wamekuwa wasemaji yaani hawa jamaa hawana utaratibu kabisa kimekuwa PPP(POCKET POLITICAL PARTY)
 
Binafsi nimeishi Kenya miaka mitatu nawajua watu wa Kenya wanavyopenda pesa especially Kikuyu ,yanapokuja masuala ya kupiga pesa wao utu uweka pembeni.tunaomba viongozi wakiongozwa na mbowe walitazame suala hili kwa makini sana.kama kuna ulazima wa lissu kuendelea kubaki hospital ya Nairobi ni sawa ila kama mnaona anaweza kusafirishwa Us ni better zaid maana lissu ni wetu sote.Tunampenda.
 
amekwenda mbali sana na kuanza kutoa conclusions ambazo zinachafua lengo lake jema kama lipo.
 
Nyalandu amekua msemaji ama mpashahabari wa wagonjwa siku hizi!

Yeye ndio mtoa taarifa za wagonjwa...
Kuna tatizo kufanya hivyo? Mbona hukuuliza hili swali wakati ule anawasaidia wahanga wa ajali ya Arusha?
Tuthamini jitihada za watu! Ipo siku anaweza kukusaidia wewe ama ndugu zako!
Tunapochangia kwenye majukwaa haya, ni vizuri kujali maadili na uungwana, hata kama tupo kwa ajili ya kuwafurahisha watu fulani!
 
Nimeshangaa kwa kweli.Chadema mnataka Lissu Afe ?Hainiingii akilini kuwa maDr wa Nairobi wakatae kuandika ruhusa ya kupelekwa Marekani.Kuna kitu hapa tunafichwa.Halafu bado Chadema mnaendelea kuomba michango.Hivi ruzuku zinafanya kazi gani?Jamani eeeeh Africa ni Africa tu tena East Africa Nairobi bora hata ingekuwa South.Lissu anahitaji matibabu nje ya Africa please.
Unataka ruzuku itumike kwa matibabu ya mgonjwa? Una akili timamu wewe?
Spika mwenyewe kagwaya kumtibu Lissu kwa gharama za Serikali kwa sababu anajua matokeo yake! Leo unawashauri CHADEMA watumie ruzuku za chama?
Unayajua masharti ya matumizi ya fedha zitokanazo na ruzuku? Hilo hata CCM hawawezi kulifanya!
 
Ongera mh nyarandu kwa kuwasimamia hao mabwana ili mgonjwa apate kupona kwa wakati, wanavichwa vigumu SNA bila uwepo wako hapo wangekimbilia huko marikani richa ya mgonjwa kuendelea vizuri
 
Kesha pona kwa ripoti ya madaktari wanawashangaa Mbowe na Nyalandu kutaka apelekwe Marekani.
Ni sawa Mama mjamzito kajifungua salama Muhimbili anasuburi discharge halafu unasema unataka umpeleka akajifungulie Afrika Kusini. Madaktari lazima wakushangae.
Mungu kamponya Lissu watafuta kiki wamwache amalizie matibabu
Acha ushetani wako. Mlilolitaka limetimia nasikia hali haiwezekani tena. Mmemuua mtu wa Mungu.
 
Back
Top Bottom