Lazaro Nyalandu azuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Namanga baada ya kukosa nyaraka muhimu

strategist22

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
656
594
Mh lazaro NYALANDU amezuiliwa namanga akiwa anaelekea Kenya kutafuta hifadhi. Amezuiliwa namanga. Kufika mwakani tutabaki mimi na wewe

------
Aliyekuwa Mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini, (Chadema) Lazaro Nyalandu amezuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga baada ya kukosa nyaraka muhimu.

Akizungumza na Mwananchi leo, November 9, Mkuu wa wilaya Longido, Frank Mwaisumbe amesema mwanasiasa huyo alikuwa akitaka kuondoka nchini lakini hakukuwa na nyaraka zinazohitajika.

"Ni kweli maofisa wa uhamiaji mpakani wamemzuia kutoka nchini, kwani alikuwa hana nyaraka kadhaa ikiwamo za gari na vitu vingine ambavyo alikuwa anaondoka navyo,"amesema.

Amesema kwa sasa vitu alivyotaka kuvuka navyo bado vinashikiliwa mpaka wa Namanga na ametakiwa kuwasilisha nyaraka zake .

"Tumemtaka alete nyaraka muhimu zinazohitajika na tumemuachia akalete, lakini akishindwa atafikishwa mahakamani,"amesema.

Tukio hili limekuja wakati pia kukiwa na taarifa za aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kukamatwa nchini Kenya baada ya kuingia nchini humo bila kufuata taratibu huku ikidaiwa kuwa alikwenda kutafuta hifadhi kwa madai ya usalama wake.

Chanzo: Mwananchi
 
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini, (CHADEMA)Lazaro Nyalandu amezuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga baada ya kukosa nyaraka muhimu.

Akizungumza na Mwananchi leo, November 9, Mkuu wa wilaya Longido, Frank Mwaisumbe amesema mwanasiasa huyo alikuwa akitaka kuondoka nchini lakini hakukuwa na nyaraka zinazohitajika.

"Ni kweli maofisa wa uhamiaji mpakani wamemzuiwa kutoka nchini, kwani alikuwa hana nyaraka kadhaa ikiwamo za gari na vitu vingine ambavyo alikuwa anaondoka navyo,"amesema.

Amesema kwa sasa vitu alivyotaka kuvuka navyo bado vinashikiliwa mpaka wa Namanga na ametakiwa kuwasilisha nyaraka zake.

"Tumemtaka alete nyaraka muhimu zinazohitajika na tumemuachia akalete, lakini akishindwa atafikishwa mahakamani,"amesema.

Tukio hili limekuja wakati pia kukiwa na taarifa za aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kukamatwa nchini Kenya baada ya kuingia nchini humo bila kufuata taratibu huku ikidaiwa kuwa alikwenda kutafuta hifadhi kwa madai ya usalama wake.
 
Show zimeanza. Popcorn is ready. Na mimi pipa langu wasijenizuia kupanda aisee naondoka weekend. Watu smart wote sa hivi wanakimbia nchi.

Uchumi unakua thamani ya Tzs inashuka. Hii miaka mitano aisee muombe sana kwa miungu yote mnayoijua hadi ya miti. Ngoja nikamsalimie Joe Biden tutaonana 2025.
 
Nakuwa mgumu sana kuamini mtu kama Nyalandu anaweza kusafiri nje ya nchi halafu aache vitu vya muhimu, kwani hiyo ni safari yake ya kwanza? au alikuwa na haraka za nini mpaka akaviacha? hofu ya usalama wake au?

Nahisi kuna jambo baya limejificha hapa, muda sio mrefu litajulikana tu, wapinzani wa nchi hii kwa hakika wanapitia nyakati ngumu sana kwa sasa.
 
CHADEMA ni wapuuzi sana, huu n mchezo wameshaplan kuucheza, na nahis watakuwa wanaongozwa na mabeberu, walete hali ya sintofahamu ionekane Tz kuna shida kuwa upinzani kumbe sio, Lipumba, mrema, cheyo wapo Tz miaka nenda rudi na hkuna baya liliwatokea, hawa CDM wakubali matokeo tu.
 
Nakuwa mgumu sana kuamini mtu kama Nyalandu anaweza kusafiri nje ya nchi halafu aache vitu vya muhimu, kwani hiyo ni safari yake ya kwanza? au alikuwa na haraka za nini mpaka akaviacha? hofu ya usalama wake au?

Nahisi kuna jambo baya limejificha hapa, muda sio mrefu litajulikana tu, wapinzani wa nchi hii kwa hakika wanapitia nyakati ngumu sana kwa sasa.
Nyie si mmegoma kuandamana??? Sasa waacheni viongozi wenu waandamane kwenda balozini na nje huko

Kwahiyo hawa jamaa wote passport hawana?
wamepoteza ? Hawajui taratibu za kusafiri kutoka nje ya nchi? Walikuwa wanakimbizwa na wauaji wame sahau?
Wanatafuta attention na lazima kipo wanachokitarajia toka kwa hilo
 
Back
Top Bottom