Uchaguzi 2020 Lazaro Nyalandu amejiandaa zaidi kuwa mgombea kuliko wenzake

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,531
8,616
Nikitazama mwenendo wa kampeni za ndani kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA ] ambako kuna Wagombea wengi, unaona wazi kuwa Mgombea Lazaro Nyalandu amejipanga zaidi kiakili na uwezo kugombea Urais mwaka huu 2020.

Kwa namna anavyoandaa mikutano yake ya ushawishi, aina ya kampeni anazofanya, utulivu na mipango unaona kabisa huyu ni Mgombea Urais anayepanga kuonyesha weledi na kubadili aina ya kampeni tulizozizoea nchi hii; juzi ameelekea Mwanza kuzindua LAZARO2020 ONLINE PLATFORM na kutafuta uungwaji mkono.

Wagombea wengine waliojitokeza ni wazuri lakini hawaonyeshi mipango yao. Mfano Tundu Lissu anafaa sana lakini anakabiliwa na mambo mengi ya kisheria. Freeman Mbowe japo wananchi na wazee ndani ya chama wamemtaka afanye hivyo, haonyeshi tamaa ya kutaka kuwa mgombea na kimsingi hakujiandaa kuwa Mgombea kabisa bali kajiandaa kuratibu kampeni za chama chake kama alivyosema.

Ni vyema sasa wana MIKAKATI wa Chadema wakutane na kuweka sawa karata zao.

Alamsiki
 
Sawa kajiandaa lkn kwa siasa za awamu hii zinazotegemea boss kaamkaje kwake itamuwia vigumu, anaweza kuwa mgombea mwenza mzuri sana.
 
Back
Top Bottom